Siasa ni hisia, watu huhisi tofauti

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,611
67,091
Nakumbuka mwaka 2015 wakati wa uchaguzi basi kila shabiki alikuwa na maneno yake, wengine walimpenda aliye piga push ups, wengine walimpenda mwenye nywele nyeupe wakisema na moyo ni mweupe, tuliona hata mambo ya ugonjwa, familia na tabia mbali mbali zilizo husisha hisia za kibinadamu tu, zikiwa na mchango mkubwa kwa washabiki wa wana siasa mbali mbali kipindi hiko.
Siasa hasa za uchaguzi siku zote ni hisia, ndio maana kuna watu walimpenda sana Rais Kikwete kwa sababu tu ni handsome. Kuna siku niliskia kwenye kampeni mwenye hisia mmoja aki waambia watu "msimchague yule ni mgonjwa ata fia ikulu" hizi nazo zilikuwa hisia tuu, utajuaje kama mwenzio atakufa akiwa sehemu fulani!? Mwisho wa siku watu ndio walipiga kura kwa hisia zaid.

Uchaguzi ukiisha watu hubaki na hisia zao, mtu aliye mpenda mpiga push ups siku zote ata ona ni kazi yake kumtetea mpiga push up regardless nini kina endelea kwenye utendaji sikuzote ata andamwa na vile vi ji hisia alivyo kuwa navyo siku alipokuwa kwenye booth ya kura, huyu ata acha kumpenda mpiga push up mpaka aathiriwe yeye mwenyewe ki hisia.

Ataona kuna vijana maelfu kwa maelfu hawaja ajiriwa, ataona kuwa hospitali hazina dawa, ata ona kuwa nchi ina kodi hata zisizo na sababu, ata ona sekta binafsi nyingi zina kufa, ataona wanasiasa wana kandamizwa, na wana nchi wana fungwa bila makosa, ataona sekta kama utalii na biashara ndogo ndogo zina kufa, lakini ata tafuta sababu za kumtetea mtu aliye mpenda kwa kupiga push ups, pengine kwa kuwa haja athirika yeye binafsi, au pengine hisia bado zina mtawala na ana hisi mpiga push ups ana mipango yake kabambe na nchi itakuja kukaa sawa.
Mtu kama huyu hata ukimpinga mpiga push ups, utaskia kejeli nyingi na misemo kama vile 'umelewa', 'we ni mjinga' au 'huna akili' na misamiati mingine mingi, mtu huyu ukimwona msamehe ni wa kumuacha kwa sababu hisia za kumpenda mpiga push ups zinaendelea, siku na yeye ubovu au ukatili wa mpiga push up ukimfikia hisia huondoka na huwa anakuja kujua baadaye kuwa, mambo haya nilisha ambiwa. Na pia kuna wale wenye hisia kali na pia wanalipwa wamtetee mtu wanaye mpenda au wanadhani kwa hisia zao, mpiga push ups atawapa nao ulaji akiwaona wanavo mtetea, hawa ndio hatari zaidi.

Mwaka mmoja sasa umepita watu wenye hisia zao za mapendo lazima wata sifia mambo yanayo fanyika kwa sababu bado mpiga push ups yuko mioyoni mwao, wata taka kuto kubali kuwa kama taifa tulifanya kosa mwaka 2015, wata taka kutuonesha kuwa mpiga push ups ana jua anacho kifanya.

Watu wenye hisia wana nikumbusha kuna wimbo msanii Jay Moe alisema "wacha kupiga mayowe, waache wayaone wenyewe" nashauri tuendelee kuzungumza nao lakini pia tuwaache waje wayaone wenyewe

*si hawa wa push ups tu hata wale wenzao wana hisia kali wao ukiwaambia wajirekebishe wanakuita 'msaliti' au 'pandikizi' hawa nao waache watakuja kuyaona wenyewe, ila hawa kwa kuwa hawajashika nchi siyo priority yetu kwa sasa na naona kidogo hawa wana ka uafadhali.
 
Nakumbuka mwaka 2015 wakati wa uchaguzi basi kila shabiki alikuwa na maneno yake, wengine walimpenda aliye piga push ups, wengine walimpenda mwenye nywele nyeupe wakisema na moyo ni mweupe, tuliona hata mambo ya ugonjwa, familia na tabia mbali mbali zilizo husisha hisia za kibinadamu tu, zikiwa na mchango mkubwa kwa washabiki wa wana siasa mbali mbali kipindi hiko.
Siasa hasa za uchaguzi siku zote ni hisia, ...
*si hawa wa push ups tu hata wale wenzao wana hisia kali wao ukiwaambia wajirekebishe wanakuita 'msaliti' au 'pandikizi' hawa nao waache watakuja kuyaona wenyewe, ila hawa kwa kuwa hawajashika nchi siyo priority yetu kwa sasa na naona kidogo hawa wana ka uafadhali.
Hali ya uchumi kuwa tete na ugumu wa maisha pia ni hisia au uhalisia?

Kwa sababu wapika namba wanasema uchumi unakuwa kwa mwendokasi, wadanganyika wao wanalalamika kwamba maisha yamekuwa ya "kishetani".
Je hizi ni nazo ni hisia au uhalisia?

Hivi kuna mtu anayeweza kuwakumbusha TRA na watakwimu kwamba wamesahau kutangaza nambari zao na takwimu zao za mwendokasi tokea mwezi wa novemba?

Mtumbuaji pia amesahau kuwatumbua hawa kwa kushindwa kutuburudisha kwa twakimu za mwendokasi? Au hawataki tu-enjoy wote?

Au mapato yameongezeka sana kiasi ambacho bado wanahisabu vile vitu vya Kaizari?

Novemba mpaka Januari, siku zinakimbia kwa mwendokasi lakini namabri za TRA zimeshindwa kuendana na kazi aitakayo hapana kazi tu.

Jamaa wa serikalini nao uhalisia wana uweka pembeni, wana tumia hisia za woga, kujipendekeza n.k
So nadhan ni mwendelezo wa hisia ule ule bila kujali uhalisia
 
Back
Top Bottom