Siasa ni Hesabu. Anayebisha Amuangalie Lowassa Halafu Awaulize Sitta na Nnape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa ni Hesabu. Anayebisha Amuangalie Lowassa Halafu Awaulize Sitta na Nnape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NdasheneMbandu, Oct 27, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Nianze kwa kuomba radhi kwa wanaJF wenye allergy na EDWARD N. LOWASSA. Najua wapo wadau wengi humu jamvini ambao wakisikia LOWASSA wanakumbuka UFISADI na wakitamka UFISADI wanakumbuka LOWASSA. Watu waliopo kwenye kundi hili, ndiyo ninaowaomba radhi. Wanisamehe sana maana sidhani kama kuna namna unayoweza kuzungumzia siasa za kisasa za Tanzania bila kumgusa LOWASSA.

  Katika vipindi vyote au wengine wanavyoita awamu zote za uongozi wa nchi yetu tangu uhuru, hakuna wakati ambapo wananchi tumeshuhudia siasa ikitamalaki kama wakati huu. Mazingira ya sasa nchini kisiasa pengine ni magumu kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hivi sasa, kila mwanachama w chama fulani na hata raia tu asiye na chama anajisikia kuwa anaweza kuwa rais wa Tanzania. Hali hii ni tofauti na zamani na hii inaweza kuwa imetokana na namna nchi inavyoongozwa kiholela kwa kiwango kisichoweza kutarajiwa. Kwa wanaJF wenye umri wangu, hivi ni wana-ccm gani enzi za Mwl. Nyerere ambao angalau hata walifikiria wakati huo kurithi mikoba ya uongozi kutoka kwa Nyerere? Bila shaka, walikuwa wachache sana na sidhani kama walikuwa wanajionesha waziwazi. Wapo wanaJF wanaoweza kuiongelea hali hii kwa mtazamo hasi kwamba Nyerere alikuwa kiongozi wa kiimra na kwamba hakujenga "mazingira rafiki" ya wanachama kujisikia huru kutangaza nia yao ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais. Mtazamo huo unaweza kuwa na ukweli to some extent lakini upande chanya pia unaweza kuwepo kwamba baadhi ya wanachama ulipofika wakati wa uchaguzi walijitazama kwa undani na kujilinganisha na Mwl. Nyerere kiuzalendo, kiuadirifu, kiutendaji, n.k. wakajiona kuwa wanapwaya na hatimaye tamaa za urais zikaishia mioyoni mwao tu pasipo mtu yeyote kujua. Hao nadhani walikuwa wengi. Lakini, kama nilivyoeleza hapo juu, leo hii biashara imepiga u-turn.

  Hivi sasa, hata wenzangu na mimi wasio na taranta na rekodi ya uongozi zaidi ya kuwa wamebahatika kupata ubunge na kisha uwaziri, tayari wanajiona wana uwezo wa kukalia kiti kikubwa kabisa cha uongozi wa nchi yetu. Kwamba mimi kama NdasheneMbandu, hatma ya nchi yangu iwe mikononi mwangu kwa sababu tu nimeonja radha ya uongozi baada ya binamu yangu, baba yangu, mjomba wangu n.k. kuniteua kushika wadhifa wa uwaziri!!!

  Katika mazingira hayo ya kila mwanachama wa chama cha kisiasa kujisikia na kuhangaikia urais, ndipo mnyukano wa kisiasa ndani na nje ya vyama vya kisiasa unapokuwa mkubwa kwani prospective candidates ni wengi, tofauti na ilivyokuwa zamani. Leo hii kwa mfano, ni mtanzania gani katika nchi hii anayefuatilia msuala ya siasa asiyejua kwamba Mzee Sitta kwa udi na uvumba anataka kuwa rais wa nchi hii? Bila shaka, hakuna. Halikadhalika, nani asiyejua kuwa akina Bernald Membe, Frederick Sumaye na wengine wengi wanautaka urais kwa udi na uvumba? Bila shaka, hakuna. Sasa, katika hali ya kisiasa kama hii, ndipo linapokuja suala la HESABU. Mwanasiasa anayeweza kuruga vigingi na kupenya kwenye kina kirefu cha maji yenye mamba wengi lazima awe mpiga hesabu mzuri. Bila hivyo, hafiki mbali. Mfano mzuri wa mwanasiasa wa aina hiyo ni EDWARD NGOAYI LOWASSA. Jamani tutake tusitake huyu jamaa ni mpiganaji na kama ni hesabu za kisiasa basi hapo ndipo zilipolala na kuamkia.

  Mazingira ya kashfa ya RICHMOND iliyomwondoa madarakani Lowassa mpaka leo yamebaki kuwa tatanishi japo yeye binafsi ilifikia hatua aliona liwalo na liwe akaamua kuweka ukweli mezani. Kupitia kinywa chake mwenyewe kwenye kikao rasmi na kizito cha ccm, Lowassa alitamka waziwazi pasipo kupepesa macho huku akimtazama usoni Mwenyekiti wake kwamba ni jambo gani alilofanya kuhusiana na RICHMOND ambalo Mwenyekiti hakulifahamu na hakulitolea maagizo. Hiyo ilikuwa ni hatua na tiba muhimu sana ya Lowassa kisiasa na nadhani aliamua kusema hivyo baada ya uvumilivu kumshinda. Wengi wetu tulihabarishwa pembeni kwamba baada ya maneno hayo ya Lowassa, Mwenyekiti alifunga agenda na kuamuru nyingine ifuate. Suala la RICHMOND limekuwa ni turufu kubwa kwa wanasiasa wengine wenye malengo yanayofanana na Lowassa ya kukalia kile kiti cha enzi.

  Wanasiasa kama akina Sitta na wafuasi wao akina Nnape walidhani huo ungekuwa mwisho wa Lowassa. Walijua huo ulikuwa ndiyo msumali wa mwisho kwenye jeneza la Lowassa kisiasa. Lakini wapi, mwenzao aliamua kupiga hesabu za chini chini kwa ku-integrate na ku-differentiate na jitihada hizo hatimaye zimeanza kujibu. Hivi sasa, baada ya chaguzi ndani ya ccm, asilimia kubwa ya "wenye maamuzi kichama" ya nani awe mgombea wa ccm wa urais, ipo upande wa Lowassa. Wapo watakaosema chaguzi ziliendeshwa kwa rushwa lakini ukweli ni kwamba uchaguzi umekwisha na viongozi tayari wamepatikana na hesabu tayari zimejibu. Kilichobaki sasa, tuombe uzima tushuhudie nomination ya candidate wa ccm wa urais wa 2015 kama hamtasikia Dodoma ikirindima na jina Lowassa!

  Najua wapo pia watakaosema, ccm ikikosea ikamteua Lowassa itakuwa imejimaliza yenyewe na kwa mara ya kwanza urais utaangukia mikononi mwa vyama vya upinzani. Hao nao wasidhani mambo yatakuwa ni mteremko maana huyu jamaa anayeitwa Lowassa anaona mbele na kupiga hatua kabla wapinzani wake hawajafikiria hata kunyanyua mguu. Kwa maneno mengine, Lowassa ni mzuri sana kwa RISK ANALYSIS. Unachokifikiria wewe leo mwenzio alikifiria juzi na kukitolea uamuzi. Mkono wake mpaka sasa tayari umegusa maeneo yote nyeti na akipita yeye anafunga mlango. Hakuna mwingine anayeweza kupita. Mwenye ufahamu, na ayashike maneno haya.

  Hayo ndiyo mahesabu makali ya Lowassa. Wenye uwezo wa kumwelezea Lowassa jinsi alivyo mzuri wa kukokotoa hesabu za kisiasa, ni akina Mzee Sitta na Nnape Nauye ambao walijipambanua kukabiliana nae na sasa bila shaka wanatweta baada ya kuishiwa pumzi huku wakishuhudia mwenzao akichanja mbuga.

  Thanks!
   
 2. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Lowassa = Ufisadi, full stop!
   
 3. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mtasema yote lakini kama alivyosema Ndashenembandu, Lowasa ataendelea kuchanja mbuga!
   
 4. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  na achanje mbuga.

  Binafsi namkubali sana. Si kwa lolote bali ni kwa utendaji wake. Yuko vema
   
 5. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi hamchoki? Anawalipa kiasi gani kutwa???
   
 6. zenmoster

  zenmoster JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  lowasa mie mwenywe namkubali ila chama alicho ni cha ajabu
   
 7. t

  twijuke JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uko sahihi na hili halihtaji miwani.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  aisee nime give up..nimeshasoma topic za lowassa mpaka nimeanza kukinai...yaani topic zake zinaanzishwa upya kila baada ya nusu saa humu ndani....daah hamchoki??
   
 9. J

  JFMatumbulu Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  toeni thread za huyu mtu tumechoka!
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Huu mkakati maalumu huu....
   
 11. g

  green_marwa Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lowass ndiye Rais wetu ajaye....maeneo yote nyeti yameshamkuibali!
   
 12. peri

  peri JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  njaa mbaya sana, mnamwaga povu jiingi kumsafisha lowasa wakati hata mtoto wa primary anajua lowasa ni fisadi.

  Nyerere alimjua na akamwambia ukweli, mbona mpaka leo hajaeleza alivyopata mali zake?

  Kwanini kwenye richmond hakuenda kuanika ukweli mbele ya media ili wenye maswali wamuhoji?

  Anaenda kuzungumza kwenye kikao cha mafisadi wenzake, anategemea nani atamchaleng?

  Lowasa ni mchafu na ananuka ruswa, hamuwezi kumsafisha hata mkitumia tindikali.

  Ktk historia ya tanzani, lowasa ndio mwanasiasa pekee aliyeweza kutengeneza mtandao mpana wa rushwa ndani na nje ya ccm.
   
 13. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anafaa sana kuiongoza familia yako ili awe anakutolea hela ya kununulia sabuni , mafuta na chumvi
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Lowassa alipokuwa waziri wa ardhi alikuwa anatumia madaraka hayo kuwanyang'anya viwanja wahindi huku akitangaza RTD kuwa kafanya hivyo kwa fiada ya umma lakini baadaye akawa anapokea hela nyingi sana kutoka kwa hao hao aliotanganza kuwanyang'anya viwanja, na baadaye akawarudishia viwanja hivyo kimya kimya. Hicho ndicho kilichokuwa chanzo cha utajiri wa Lowassa. Alipokuwa Waziri Mkuu, alitumia madaraka hayo kulazimisha RichMondulian kupewa tenda ya umeme wa dharura bila kufuata taratibu, jambo ambalo limeiingiza Tanzania katika matatizo makubwa sana ya kisheria kimataifa. Alifanya yote hayo akiwa ni waziri anayewajibika kwa rais. Je mtu huyu akiwa ndiye rais mwenyewe mwenye uamuzi wa mwisho ataacha kufanya lipi kwa manufaa yake binafsi na kulisahau taifa hili? Kikwete mwenyewe ambaye ni nafuu kidogo bado kaliangamiza taifa hile je Lowassa atatuachia nini?

  Uongozi wa mwisho unahitaji sana hekima maadili, ambayo nadhani Lowassa hana kabisa. Ni mtaalamu wa kufukuzia mali na kuwashinda wengine kwenye madili ya fedha; akiwa na madaraka atafukuzia sana na kuwazuia watanzania wengine wote wanaoingia katika njia yake ya mali. Inanitisha sana Tanzania tunakoenda!
   
 15. C

  Concrete JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Unayajua maeneo nyeti wewe?
  Naona unaropoka tu.
   
 16. M

  Mwanasazi JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  aisee huyu ndio lowasa kama uzi ulivyosema, yaani ana mahesabu makali ya kisiasa, hata hii JF kashaipigia mahesabu kisiasa na ndio maana thread zake haziishi humu ndani.
   
 17. C

  Concrete JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Utendaji upi huo?
  Sote tunajua siku zote amekuwa akitenda kifisadi.
   
 18. C

  Concrete JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kwamba ni fisadi mkuu.
   
 19. C

  Concrete JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Unamkubali kivipi?

  Inakuwaje umkubali Lowassa halafu ushindwe kuikubali CCM.
  Hivi hujui kuwa Lossawa kisiasa amezaliwa, kalelewa, anatunzwa, analindwa na kuwezeshwa kila kitu na CCM?
   
 20. M

  Mwanasazi JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  aisee huyu ndio lowasa kama uzi ulivyosema, yaani ana mahesabu makali ya kisiasa, hata hii JF kashaipigia mahesabu kisiasa na ndio maana thread zake haziishi humu ndani.
   
Loading...