Siasa Ni Fikra Shindanishi

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
Siku tutakapojua siasa ni itakadi yaani vile mnavyoamini katika uchumi katika siasa na katika jamii ndipo Tanzania itapata maendeleo ya watu sio vitu

Siasa sio mabavu ni fikra shindanishi japo Yericko Nyerere “husema siasa ni nguvu atafutazo mtu au kundi kupata madaraka kutekeleza kile alichonacho na akishapata hutumia nguvu hiyo kulinda madaraka “ hoja zote mbili zinashabiana kwasababu asili yake ni fikra inayopelekea mtu au kundi kuamini ktk siasa ,uchumi na jamii mfano CHADEMA wanasema itakadi yao ni mrengo wa kati na wanaonesha kwa vitendo wanaamini katika uchumi wa soko huria lenye kudibitibiwa na sera sio soko holela inaamini ili tuapate maendeleo ya watu inabidi kuwe na serikali za majimbo zitakaweza kiwa karibu na watu ndio maana wao wana kanda kumi za kiuongozi kuonesha namna ya uendeshaji ulivyomadhubuti.

Tatizo hutokea baada ya nguvu kuipata jinsi unavyoyatumia madaraka yaweza kuwa mazuri pia mabaya mfano Adolf Hitler alianza kujenga ushawishi kwa umma na alipopata madaraka akaanza kueneza fikra zake zilizowachukiza wengi katika utawala wake.

CCM wanasema wao itakadi yao ni ujamaa ambao uchumi unashikiliwa na serikali kwa kivuli cha mali ya umma na wameongoza taifa hili kwa zaidi ya nusu karne sasa tujuulize je wanaiishi hii itakadi?
Je ujamaa haupendi siasa shindani?
Je ujamaa haupendi uhuru wa habari?

Hapo ndipo utajua itakadi gani inafaa kuliongoza Taifa hili.
Baba wa Taifa ukisoma kitabu chake cha “uongozi wetu na hatma ya Tanzania “maudhui yake alikuwa anashambulia mifumo ya kiuongozi ndio maana aliposoma katiba ya chadema aliona tumaini kwa Tanzania na kukitabiria kutokana na kuja na tiba ya makosa ya ujamaa wa kiafrika.

Leo tumekuwa na siasa za ajabu kabisa kwa Taifa badala hoja kujibiwa zinapigwa na rungu
Mathalani cdm na upinzani walishauri juu ya namna ya kuukabili gonjwa lililoikumba dunia la korona badala ya kutazama ushauri wakageuzwa wasaliti mara wanatumiwa na mabepari mara hawataki uchuguzi ukiangalia unabaki kujiuliza ujamaa haujali utu au unajali serikali ambayo kiasili ni kikundi kidogo kwenye jamii hapo ndipo hoja ya Yericko Nyerere inapoakisi baada kuipata nguvu ya madaraka namna unavyoyatumia .

Tunalizimishwa kuamini anachosema mtu mmoja basi Tanzania nzima tuamini mzee wa msoga alituambia za kuambiwa changanya na zako.

Itikadi moja husahisha itakadi nyingine ndivyo ilivyo kuna vijana wamehama upinzani na kurudi ccm hoja zao ni kukua kisiasa kwenye nn itakadi au masilai binafsi muda mwingine unajiuliza walishajiuliza kwa vijana wenzao walioenda kabla washakua kisiasa yuko wapi David Kafulila Felix Mkosamali shimbwe shitambala hapo ndipo tunarudi kwenye hoja cdm tunahitaji elimu elimu elimu sio kumiliki vyeti maana eneo ambalo halipo sawa kwenye Taifa hili ni elimu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom