Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
SIASA NI AJIRA, KUZUIA MIKUTANO NI KUNYIMA KUNDI FULANI ULAJI
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Moja ya mambo ambayo nilipishana na JPM Kwenye utawala wake ni suala la kuzuia mikutano ya Kisiasa ya nje hasa Kwa wapinzani huku CCM wakiendelea na mikutano kwa mwamvuli wa kukagua miradi ya serikali iliyoandikwa kwenye ilani ya CCM.
Naona Jambo lile lile linataka kutendeka katika uongozi wa Rais Samia Suluhu.
Hii nchi Ajira zimekuwa ngumu na viongozi tayari wameshaonyesha uwezo mdogo wa kushughulikia suala hili.
Siasa ni Ajira, Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.
Wapo watu wamesoma mpaka Degree nne za masuala ya Siasa.
Siasa pia ni hobby, Siasa wakati mwingine Kwa wengine ni Mchezo na burudani.
Unazuia mikutano ya nje ya Siasa alafu unaacha mikutano ya injili, mikutano ya Wasanii ambayo huitwa matamasha ya muziki, Kwa kweli ni kuwanyima haki kundi la wanasiasa.
Wanasiasa waachwe wafanye kazi zao ikiwemo mikutano ya nje ili kujenga vyama vyao na kutafuta wanachama wapya kama ilivyo kwa mikutano ya Dini ambapo madhehebu hutumia Kueleza Imani yao ili kupata ushawishi Kwa watu na kujipatia waumini wapya.
Kuzuia mikutano ya nje ni kuzuia ukuaji wa vyama husika moja Kwa moja.
Wakati upande wa CCM inajitangaza kupitia serikali kutokana na kuwa yenyewe ndio imeunda serikali.
Nafikiri serikali iachane na mpango huo wa kubana haki ya Uhai wa vyama vingine. Kuzuia mikutano ya nje ya Kisiasa ni kuzorotesha ukuaji WA vyama husika.
Hata hivyo, mikutano mara nyingi haifanyiki nyakati za mchana ambao ni muda wa kazi. Hufanyika jioni kabisa kuanzia mida ya saa tisa mpaka saa kumi na mbili.
Sio sababu ya maana ya kuzuia mikutano ya nje ya Kisiasa labda sababu za hila na ukandamizaji.
Wengine watasema, kuruhusu kuendelea Kwa mikutano ya nje ya Kisiasa kutaathiri na kuichanganya serikali, kwani wapinzani wataishambulia na kuikosoa serikali huku wakiitoa serikali katika shabaha ya kuleta maendeleo.
Hiyo sio kweli kwa sababu serikali au CCM hakitakuwa na ulazima wa kuhofia kusikiliza hoja za upande wa pili ikiwa wao wenyewe wanafanya na kutekeleza hoja na mambo ya msingi yanayotakiwa ndani ya jamii. Lakini endapo upande wa pili utakuwa na hoja za manufaa zaidi ya CCM basi ni dhahiri shahiri hofu lazima ikae juu yao, na ndio maana wataona hatari ya mikutano hiyo.
Katiba mpya ni muhimu ikiwa bado kuna changamoto za namna hii ndani ya nchi yetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Kinole, Morogolo