Siasa ndo inaendesha maisha. Kubali ukatae huu ndio ukweli

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Wanajamvi habari za muda huu? Naamini mko salama.

Leo nimeona nije na mada hii kwamba siasa ndo inarun maisha kwa kuwa kila tunapobadilisha viongozi wa kisiasa kila kitu kinabadilika. kwa hiyo kwa uelewa wangu siasa ndo kila kitu.

Kwanza ukiangalia mifumo ya maisha wanasiasa ndio wanaobuni. Tafadhali naongelea Tanzania ila kwa wengine wataalam wanasikilizwa.

Pili Atunaishi kwa matakwa ya wanasiasa

Tatu ukija kwenye suala la mifumo ya biashara, elimu, kilimo uvuvi kila kona wanasiasa ni kutoa amri tu. Wataalam wanaishia kunung'unika ukileta za kuleta job yako inaota mbawa.

Kiukweli mimi naona tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka tutakapopata wanasiasa watakao washiriksha wataalamu.

Mimi nasema siasa ndo inarun maisha; penda usipende, bisha usibishe, huu ndo ukweli.
 
Hii ni kwa Africa tu na baadhi ya Nchi. Hasa hasa Tanzania Nchi ya wajinga. Jamaa akiongeza tu mishahara na kutoa ajira mwaka huu TUSHASAHAU KILA KITU na ndio maana wanatuchezea sana sharubu.
 
Hii ni kwa Africa tu na baadhi ya Nchi. Hasa hasa Tanzania Nchi ya wajinga. Jamaa akiongeza tu mishahara na kutoa ajira mwaka huu TUSHASAHAU KILA KITU na ndio maana wanatuchezea sana sharubu.
siasa inamuakila kitu hata wasichojua wanaropoka tu na mfano mbunge anaenda china kuangalia au kujifunza jinsi wanavyoendesha viwanda viwanda vidogo zinavyosaidia badala ya kupeleka wataamu mbunge mwenyewe kaishia kidato cha nne huyo ni msomi kwa nchi yetu akirudi wala hana mpango wowote wa kuwasaidia watu. Lakini alipoenda serikali ilimlipia hela ndefu. shida sana
 
Back
Top Bottom