Siasa ndani ya CCM, hatimaye Nape Nnauye amalizwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa ndani ya CCM, hatimaye Nape Nnauye amalizwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 3, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Date::11/2/2008
  Siasa ndani ya CCM, hatimaye Nape Nnauye amalizwa
  Na Saa Mohamed
  Mwananchi

  KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imechukua maamuzi mazito baada ya kupangua majina ya wagombea wa nafasi za uongozi wa ngazi ya taifa wa jumuiya zake, ukiwemo Umoja wa Vijana (UV-CCM) katika jitihada za kurejesha mshikamano.

  Duru za habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam zinasema aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UV-CCM, Nape Nnauye, ametupwa nje.

  Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu, wagombea uenyekiti wa UV-CCM ambao waligawanya wanachama wa CCM, wameenguliwa na badala yake nafasi hiyo imekwenda kwa Wazanzibari, wakati katika Jumuiya ya Wazazi, wakili maarufu, Nimrod Mkono ameenguliwa.

  Majina yaliyopendekezwa yatawasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu kilichopangwa kufanyika Dodoma Novemba 8 na 9 .

  Alisema majina yaliyopitishwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa UV-CCM ni Hamad Masauni, Suleiman Hajji na Adila Vuai ambao wote wanatokea zanzibar.

  Katika nafasi ya makamu mwenyekiti, waliopitishwa ni Beno Malisa, Hussein Bashe na Zainabu Kawawa wakati Nape Nnauye ameachwa kwa kigezo cha umri ambao imeelezwa kuwa hadi Novemba 26 atakuwa anatimiza umri wa miaka 31.

  Kwa mujibu wa kanuni za UV-CCM, mgombea anatakiwa asizidi umri wa miaka 30.

  Nape aliingia kwenye malumbano makubwa na vigogo wa CCM wakati alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti kwa kuwarushia tuhuma baadhi ya vigogo kwa ufisadi na moto aliouanzisha ulizimwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati.

  Nape alisababisha tafrani hiyo baada ya kutuhumu kuwa mkataba wa uwekezaji kwenye jengo la makao makuu ya UV-CCM haukuwa na manufaa kwa umoja huo na kwamba haukupitishwa na vikao halali vya jumuiya hiyo.

  Kauli yake, ambayo pia ilishambulia baadhi ya vigogo, akiwemo waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mwenyekiti wa umoja huo, Emmanuel Nchimbi, ilisababisha mvutano na baadaye mwanasiasa huyo akavuliwa uanachama katika kikao cha Baraza Kuu la UV-CCM, jambo ambalo lilikuwa kama kutia mafuta kwenye moto.

  Kwa mujibu wa habari kutoka kwenye kikao hicho, maamuzi hayo yanaweza kurudisha amani iliyoanza kutoweka miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu, wakiwemo wanasiasa vigogo ambao walishaeleza kuwa wanasubiri suala la Nape liwasilishwe kwenye kikao hicho ili walishughulikie.

  "Ni kweli hata mimi nimefurahi kwani hali ya kisiasa ndani ya chama chetu ilikuwa inaelekea kuwa mbaya kwa sababu ya mvutano ndani ya jumuiya zetu," alisema mtoa habari wetu.

  Mtafaruku katika jumuiya nyingine ni ule baina ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa UWT, Sophia Simba na Janeth Kahama ambao waliripotiwa kugombana kwa maneno wakati wa kikao cha Umoja wa Wanawake cha mkoa jijini Dar es salaam.

  Habari zinasema kuwa majina hayo mawili pamoja na la Joyce Masunga yamepitishwa katika kugombea nafasi ya uenyekiti huku Halima Mamuya, ambaye aliwahi kuwa katibu wa jumuiya, akitolewa katika kinya'ganyiro hicho.

  Kutokana na uamuzi huo, nafasi ya mwenyekiti inatarajiwa kuwa na upinzani mkali na hivyo kufanya kikao cha Halmashauri Kuu kuwa kwenye wakati mgumu wakati wa kujadili suala hilo.

  "Nina wasiwasi wakati wa uchaguzi wa UWT kwa sababu kila mmoja anajiona ni zaidi ya mwenzie," alisema mtoa habari wetu. "Lakini kutakuwa na kinyang'anyiro kikali."

  Majina ambayo yamependekezwa na Kamati Kuu ya wagombea uenyekiti wa Wazazi ni Abdallah Bulembo, Athumani Muhina na Ester Nyawaza, wakati Nimrod Mkono akiachwa katika kinya'ganyiro hicho.

  Chanzo chetu kilisema pia kuna hatihati ya kujadiliwa kwa agenda ya uchaguzi wa udiwani na ubunge wa Jimbo la Tarime baada ya CCM kuangushwa vibaya na Chadema.
   
 2. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Fitina mbaya Sana.
   
 3. pecial

  pecial JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2017
  Joined: Apr 4, 2017
  Messages: 595
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  hii habari ya lini au unacomment tuu bila kuangalia mazingira na muda wa hyo habar
   
 4. pecial

  pecial JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2017
  Joined: Apr 4, 2017
  Messages: 595
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  mhhh kweli ww mpenda pombe
   
 5. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2017
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,310
  Likes Received: 3,079
  Trophy Points: 280

  Siijaelewa; labda ni namna ya uandishi wa habari wa Tanzania, au mkoroganyo CCM.

  Yaani, Mwenyekiti wa UV-CCM anaruhusiwa kuwa na umri zaidi ya miaka 30, ila Makamu Mwenyekiti UV-CCM haruhusiwi kuzidi miaka 30, au?

  Na kama issue ni umri, kumalizwa kwa Nape kunaingiaje hapa? Umri wa kustaafu Tanzania ukiwa miaka 60, nikaomba kazi ya u-Director (strategic position) nikiwa na miaka 59 nikakataliwa, nimemalizwa au ni suala la common sense?

  Tatizo ni kwamba Tanzania common sense is not common to all the waandishi wa habari.
   
Loading...