Siasa na Vitimbi vya Kombe la Dunia Lilipotua Bongo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa na Vitimbi vya Kombe la Dunia Lilipotua Bongo!!

Discussion in 'Sports' started by BAK, Nov 19, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Thursday Nov 19, 2009

  [​IMG] President Jakaya Kikwete lifts the FIFA World Cup trophy at the National Stadium in Dar es Salaam few hours ago. The trophy is on a 52 nation tour of Africa in the run-up to the 2010 FIFA World Cup tournament arrived in the country today. (Photo by John Lukuwi)
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Date::11/19/2009Kikwete:Tusipobadilika tutakuwa watazamaji milele.
  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete, akiwa na kombe la dunia katika uwanja wa Taifa, baada ya kulipokea kombe hilo mjini Dar es salaam Alhamisi.Na Dorice Maliyaga

  RAIS Jakaya Kikwete jana alilipokea Kombe la Dunia la fifa na Coca-Cola kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku kuwalaumu wadau wa soka kwa kukwamisha maendeleo ya mchezo hapa nchi.

  Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea kombe hili Rais Kikwete alisema kuwasili kwa taji hilo ni jambo la kihistoria, imeleta changamoto kubwa kwenye maendeleo ya michezo hapa nchini.

  "Kutwaa Kombe la Dunia ni ndoto ya kila mchezaji na kufika kwa taji hili Tanzania ni bahati ya pekee kwa kutimiza malengo yetu ya soka," alisema.

  “Itatuchukua miaka elfu moja kabla yaTanzania kufuzu kwa kombe la Dunia kama tusipobadilika kwenye mfumo wetu wa soka,” alisisitiza rais.

  Rais alishutumu shirikisho la soka la Tanzania 'TFF' kwa kushindwa kubaini vigezo vinavyosababisha kuzototesha mchezo huo hapa nchini.

  "TFF iachane na tabia ya kutilia mkazo suala la mapato na ushabiki kwenye kupanga ratiba zake kama kweli wanataka kuendeleza soka."
  Alisema; ''Kama TFF itaachana na mambo hayo na kutilia suala la ukuzaji wa soka ya vijana kwa kuhakikisha klabu zote zinakuwa na timu za vijana.''

  Rais alilipigia vita suala la adhabu zinazotolewa na kamati zake TFF kwani kwa kiasi kubwa zinachangia kuua vipaji vya wachezaji.

  "Ni jambo la kushangaza kuona TFF inawafungia wachezaji miezi sita au mitatu si sawa kawaida mchezaji angetakiwa kufungiwa michezo mitatu kama anafanya kosa kubwa."

  Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa ziara ya kombe hilo kwenye uwanja wa Taifa jijini jana, Kikwete alisema kamwe Tanzania haitoweza kusonga mbele kisoka kama viongozi na wadau wote wa soka wasipokubali kubadilika.

  Alisema ni lazima kufanywe jitahada za makusudi ya kujenga shule za soka kwa vijana na kuachana na tabia ya kusajili wachezaji hao wazee ambao watacheza kwa msimu amoja na mwingine huachwa kutokana na umri wake.

  ''Watafutwe walimu wengi wa michezo kwenye mashule, vijijini mitaani na sehemu zote ili kuwapa nafasi na kuutambulisha mchezo huo kwa wingi.''

  Alisema ujio wa kombe hilo ni deni kwa Taifa kuhakikisha wanaongeza bidii na kuacha kuwa watazamaji kila siku.

  Hata hivyo Kikwete alizitaka klabu kuachana na tabia ya kuwa na malumbano ya kila kukicha kwani ni moja ya sababu ya kudidimiza soka kwa kuwa zenyewe ndiyo mizizi ya fitina.

  Alisema ili kuuendeleza mchezo huo lazima kupata walimu wenye uzoefu na hodari wa mpira na kuwaepuka wachambuzi wa soka uchwala ambao wao kazi yao kila siku kusubili makosa ilikukosoa.

  "Tuwasikia wakisema kocha hafai kwanini asingemtumia mchezaji furani wakati hawana wanalojua."

  Rais alisifu uteuzi wa vijana kwenye timu taifa ya Tanzania kwani unasaidia kuibua vipaji vipya ambao wataweza kusaidia nchi siku za usoni.

  Kombe hilo liliwasili nchini majira ya saa 10:30 jioni na kupokelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendela kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa.

  Kombe hilo lilopo kwenye safari ya kuelekea Afrika Kusini ilikuwa hapa nchini kwa siku mbili, leo walitakuwa visiwani Zanzibar na kesho Jumamosi ilitakuwa uwanja wa Taifa na kushudia na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa soka hapa nchini. Watu waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege walibaki wakiduwa wasijue nini kinaendelea baada ya ndege kuwasili, na kushitukia tayari limeshangia kwenye magari maalumu yalioandaliwa na msafara kuanza ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Helkopta.

  Source:Mwananchi
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,261
  Trophy Points: 280
  Rais mwenyewe anamkubali Maximo nyie mtapiga kelele hadi mfe ,kasema jana wachezaji hutengenezwa kwenye klabu zao na sio timu ya Taifa
   
 4. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Tuwasikia wakisema kocha hafai kwanini asingemtumia mchezaji fulani wakati hawana wanalojua."
  FISADI hashangai GHARAMA tunazopoteza.lol.....
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  walau jana aliongea ya maana,

  maana tff ni wazushi tupu

  kocha nae ni wa kubadilisha hana maana kabisa
   
 6. h

  herikujua Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Coca cola watapenda sana hii picha....
   
 7. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jamani hivi kweli hili kombe ni urijino??!! I dont know why i am wondering it is not......
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  I hate football.

  Mwenzako Mkapa alibeba pande la dhahabu la size hiyohiyo-Kalagabaho!
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  JK akajaribu kumpa mamsapu wake naye alibebe kombe hili. Jamaa yule mzungu/mwarabu wa FIFA akamkatalia! Alimwaibisha kidogo Rais wetu mbele ya kadamnasi.
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  na hili nalo siasa?
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Timu ya Taifa sio mahali pa kufundisha wachezaji jinsi ya kupiga kona na penati...kwa mtaji huu hata aje Mourinho hatufiki popote! Timu ya Taifa inajengwa na wachezaji ambao tayari wako katika kiwango cha juu waliosukwa kuanzia mashuleni, kwenye vilabu wanavyochezea, shule maalum nk...
  Tunaendekeza mno u-SIMBA na u-YANGA wakati kiukweli timu hizi mafanikio yake yanaishia hapa nchini na labda afrika mashariki na kati, zaidi ya hapo hakuna kitu!!
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  labda kwakuwa kalishika kikwete maana ninyi hamkawii kuanzisha issue out of it.
   
 13. GP

  GP JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  jamani makisimo ni noma, katuletea kombe mara mbili mfululizo bila kushiriki, du!!!
   
 14. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sir are you sure? can you bring the evidence down here?

  Kama huna ushahidi jamani si vyema kusema mambo ambayo ya aribu image yetu tena ya kiongozi mstaafu wa juu wa nchi.

  Lets talk with evidence and its good to realistic in our conversation as a sign of proffessionalism and maturity
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yeah sijui wasaidizi wake hawakumkumbusha kuwa yeye ndo pekee atae lishika.
  [​IMG]

  Mama alitaka kulishika mzungu akamuwahi
  [​IMG]

  Naona JK mzuka ulikuwa mwingi mpaka akajisahau na kutaka kumpa na mam'sap nae aliguse tu.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Coca cola wanatangaza bidhaa zao kwa kudhamini kombe hili. Rais alijipeleka BURE tu?
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Huoni anavaa cheni shingoni? waswahili tuna msemo ''aliyeshikwa na ngozi....??
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ilikuwa bonge la soo na noma kilo kumi!!!!!!

  mama alitaka kuligusa!
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ilikuwa ni bonge la soo na noma kilo kumi!!

  mama alitaka kuligusa!
   
 20. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli jana mh.rais wetu aliongea mambo ya maana sana katika maendeleo ya soka kwa nchi yetu.kuweka wazi uozo na uzembe na utendaji usioridhisha wa TFF alifanya jambo njema sana.

  TFF zingatie na myafanyie kazi maangizo ya kiongozi wa juu wa nchi yetu kwa maendeleo ya michezo hasa mchezo wa mpira wa miguu.
   
Loading...