Siasa na Utendaji Mbovu Usioeleweka wa CDA, Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa na Utendaji Mbovu Usioeleweka wa CDA, Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Worshiper, Oct 18, 2012.

 1. T

  The Worshiper JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni miaka mingi sasa imepita tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya ustawishaji makao makuu Dodoma – CDA (Capital Development Authority) huku ikipewa majukumu ya kupanga, kuratibu, kuustawisha na kuuendeleza mkoa kufikia na kubeba hadhi ya makao makuu.

  Kama ilivyo kawaida mambo mengi ya mustakbari wa nchi huamuliwa na siasa ndivyo vivyo hivyo inavyoendeshwa mamlaka hii (kisiasa) miaka nenda rudi. Ndiyo maana haishangazi kuona kwa miaka yote hiyo toka kuanzishwa kwake ikiwa hakuna lolote la maana likiwa limefanyika kufikia lengo na wala haieleweki uanzishwaji na utekelezaji wa mipango yake ilikuwa ni wa muda gani.

  Kazi nyingi inazozifanya kwa sasa ni zile ambazo zingekuwa zinafanywa na Manispaa ya Dodoma hivyo inashindwa kueleweka tofauti kati ya kazi za Mamlaka na Manispaa.

  Cha kujiuliza hapa ni kwamba; Je, kazi ya CDA ni moja tu kupima na kugawa viwanja? Kama ni hivyo uwepo wa Manispaa ya Dodoma ni nini? Kwasasa ukipita pale utakutana na magari ya kifahari kwa ajili ya maafisa wao lakini ukiingia ndani utakutana na mifumo duni na ya kizamani ya utendaji kazi huku urasimu ukiwa umeshika hatamu na ubadilishwaji wa wawakurugenzi usiyo na tija.

  Uwepo wa mamlaka hii hauonekani kuwa na tija sana kwa mji kwakuwa hata robo ya malengo yake hayajafikiwa na inaonekana kuwa ucheleweshwaji wa maamuzi ya serikali kuhamia Dodoma (unaofanywa makusudi na serikali ya CCM) una manufaa kwa watu na pengine kama hilo lingekuwa limefanyika ingekuwa inamaanisha kukata mirija ya viongozi hawa serikalini iliyochomekwa kwenye mamlaka hii. Hii inamaanisha kuzidi kuzama gizani kwa mkoa wa Dodoma kimaendeleo ndiyo kuneemeka kwa kwa baadhi ya viongozi.

  Siasa ndiyo inayoamua CDA ifanye nini, itende nini na iache kipi na ni ngumu kwa mkurugenzi kuja na kuendeleza mawazo mapya tofauti na yale aliyoyakuta ambayo inaonekana ni ngumu kutekelezeka kwakuwa yeye ni kama kivuli cha wakubwa serikalini.

  Naomba kuwasilisha
   
 2. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwani CDA ni jukumu lao kupima na kuallocate plots?functions zao ni zipi?
   
 3. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CDA Chafua Dodoma Always waliwekwa kwa nia njema ya Nyerere lakini imebaki kueneza ukimwi pale kwa kushirikiana na wabunge kama komba wasira et al
   
 4. M

  MUJARABU Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .....Nenda sehemu yeyote Tanzania hakuna mji uliopangiliwa kama Dodoma na hii ni kazi ya CDA, Kikubwa ninachokiona hapa ni ushabiki wa kijinga kabisa wakati wenzetu walioendelea wanatoa ushirikiano ili miji yao ijengeke sisi humu ndani tunaongelea kuvamia maeneo na tunafikiria kivivu-vivu............kisa mnataka wapewe Halmashauri ili Madiwani na Wabunge wakalete siasa kwenye mipango miji.......................
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mujarabu unajua mji uliopangiliwa kuliko yote Tanzani ni mji wa Tanga? Unaposema wananchi wanavamia maeneo unataka kutuambia nini? Kwamba sisi Watu wa Dodoma ni wampumbavu? Je tangu mwaka 2009 CDA walipouza viwanja 500 na kuwapiga watu mabomu kuna viwanja ambavyo vimeuzwa mpaka leo? Kwa miaka takriban minne sasa hakuna kiwanja ambacho CDA wameuza. Je tuendelee kuishi mitaani mpaka waje wapime? Hebu lete hoja. CDA ni janga la Dodoma. Kimsingi CDA haina tija.
  Unamkumbuka yule mkurugenzi aliyeitwa Mwanamtumwa ambaye alikutwa na viwanja zaidi ya mia mbili? Si hayo tu je bajeti ya punguzo la vifaa vya ujenzi kwa kila mwaka unaotolewa na serikali huishia wapi? Mfuko wa sementi hapa Dodoma unauzwa kwa bei ile ile ya sokoni, lakini unajua kwamba Dodoma ina bajeti ya kupunguza bei za vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kustawisha makao makuu? Amka sasa, cda wanachukua mashamba ya watu na kupima bila kuwafidia wenye mashamba. Je unajua kwamba kabla Dodoma haijawa manispaa kulikuwa na watu ambao walikuwa na makazi yao hapa Dodoma? Iweje leo CDA wanataka kuchukua mashamba ya watu bila ya kuwafidia? Mtu mwenye ekari kumi anapewa kiwanja kimoja tena kwa kulipia gharama za upimaji. Je huyu aende wapi sasa. CDA imewafanya watu wengi kuwa masikini. Inatumi mwanya wa ujamaa kupora rasilimali za watu.
  Je unajua kwamba cda inauza viwanja vya watu? Viwanja vingi sana hapa Dodoma vina migogoro. Wengine wamebadilishiwa viwanja na kupewa viwanje sehemu za mbali. Wengine wameporwa viwanja sehemu nzuri, na viwanje vingine vimeuzwa bila wao kujua.
  Angalia mfano barabara ya Chang' ombe imepita wapi? Pale sana sana itasababisha ajali. Pia barabara ni nyembamba no kwa sababu imepita kwenye vichochoro. Unajua kwa nini imepita sehemu za Chamwino? Ni kwa sababu Ngede diwani wa Chamwino ambaye pia ni msaidizi wa Maya anaishi pale. Yaani barabara imepitishwa sehemu ambayo haiikupangiliwa ipite lakini imepindishwa ili ipite nyumbani kwa Meya. Je kuna weledi cda?
  Mimi nafikiri inapaswa cda ifutwe kabisa. Haina tija hapa Dodoma.
   
 6. kiplagati26

  kiplagati26 JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  CDA imeshindwa kazi hakuna jipya walimwanguza mwalimu nyerere na mipango yake mizuri wezetu SA Walijipanga kwa zati kutoka johannesburg kwenda Pretoria na kuwacha miji ya kibiashara kama cape town,Daban. kwa ujumla tumeshindwa kuistawisha miji yetu,kama Tanga,dar es salaam,mwanza.tunaitaji kuwa na mifumo mama kwa kipindi hiki.
   
 7. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  C D A ni janga la Taifa.
   
Loading...