Siasa na Sera za kupambana na malaria

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Nilipokuwa mtoto tulikuwa tukihimizwa kwamba malaria yanayotokana na mazalia na mbu toka kwenye maji yaliyotuama. Wakati huo tulihimizwa kwamba tusafishe mazingira kuhakikisha hakuna maji yanayotuama ovyo.

na pale ambao maji yalikuwa ni lazima yaachwe yametuama basi tulikuwa tukihizwa kufunika ama kupulizia dawa.

Wakati huo kwa kiwango kikubwa tiba ya malaria ilikuwa Chloroquine.

Leo watoto wetu wanahimizwa kwamba kinga kuu ya malaria ni kujifunika kwa vyandarua. Na tiba ya malaria inabadilika badilika mara kwa mara, huku kukiwa pia na habari za kusambaa kwa dawa feki.

Wakati huu tuliwasikia wengine wakiimba 'marufuku DDT' lakini wakati huo huo nchi zingine wanazungumzia DDT.

Suala hili linaonekana kama ni mjadala kuhusu afya na utabibu, lakini asili ya mabadiliko haya ya mara kwa mara ni maamuzi ya wanasiasa kuhusu sera gani iwe kipaumbele katika kutafuta kinga na kutoa tiba ya ugonjwa husika.

Hiyo tujadili hapa; sera ipi ni muafaka zaidi katika kupambana na malaria? Je, mbinu zinazotumika hivi sasa zinakidhi haja? Zipi ziwe mbinu mbadala?

JJ
 
Yohana wa Mnyika,

Tatizo la Tanzania ni hili, ni heri waengelee kutibu kuliko kuleta kinga!

Ukileta kinga ya kudumu, ina maana watu wengine watakosa vitega uchumi!

Leo hii anayeagiza dawa za kunyunyizia kwenye vyandarua ndiye mwenye fedha nyingi, anayeagiza madawa ndiye mwenye fedha nyingi, anayeleta zile dawa za kuchoma na Xpel, ndiye tajiri na mbaya wote hawa watatu wamewakamata Wanasiasa vizuri mno KITAKRIMA kuwa ukitaka kuleta ufumbuzi wa kudumu kama hili la kutumia DDT, kila aina ya jarida la kitafiti la Kisayansi litatangazwa na kuonyeshwa ubaya wa DDT.

Lakini jiulizeni, gharama halisi ya sisi kutumia DDT in long run or long terms na gharama za kweli za kuendelea na vyandarua na Metacalfin ni kipi kina leta maana?
 
Mbaya zaidi hata Rais ameingia kwenye kampeni ya kupambana na Malaria kwa kusisitiza chandarua chenye dawa.
 
Hii ndio Tanzania nchi ya kufikirika nchi ya ajabu kwelikweli wazungu wanapoka dhahabu yetu watawala wanaenda kuomba msaada wa vyandarua dhahabu kwa chandarua AIBU leo Mtanzania amefikishwa mahali hawezi kununua chandarua cha shs.5000 wanapanga foleni kusubiri chandarua toka kwa mjomba Obama.Chandarua si suluhisho la malaria salama ni kuangamiza mazalio ya mbu lakin wakiangamiza malaria safari za ulaya zitapungua nani yupo tayari kukosa trip na kutangazia dunia watu wetu wanakufa na malaria simuoni labda kizazi kijacho
 
Mbaya zaidi hata Rais ameingia kwenye kampeni ya kupambana na Malaria kwa kusisitiza chandarua chenye dawa.
Hii kampeni ya malaria siyo project yetu. Kuna foreign agenda ndani yake. Mnakumbuka mamilioni ya dola alizoahidi George Bush alipotembelea hapa? Kitu kama $770m kwa ajili ya vyandaruwa. Mimi nilijiuliza, hivi vyandaruwa ndiyo first priority yetu au kuna la ziada ambalo hatuelezwi? Halafu kuna matangazo ya kupotosha kama lile linalosema malaria uenezwa na mbu wanaouma "usiku wa manane". Hili tangazo linajenga imani kuwa mbu akikuuma mchana au kabla ya usiku wa manane huwezi kupata malaria. Hivyo ukiwa na chandaruwa usiku basi uko salama. Ni uongo mtupu. Halafu nimeona mahala kuwa jeshi la marekani kwa kushirikiana na taasisi za utafiti za Marekani na za hapa hapa linashiriki katika utafiti wa ukimwi na malaria hapa kwetu. Je, haiwezekani kwamba sisi tunafanywa sampuli (guinea pigs) za utafiti wa biological warfare? Ni kawaida ya watafiti wetu kudandia miradi ya utafiti wa wengine ili mradi kuna pesa. Nadhani hao "wabia" wakishaondoka unakuwa ndiyo mwisho kwao. Kinachoendelea hawajui.
 
Na vyandarua vyenyewe hata haviwafikii walengwa inavyostahili! Wapo akina mama wajawazito ambao tangu waanze kwenda kliniki wanasikia kwamba watapata vyandarua viwili cha mama na cha mtoto. Mpaka wanajifungua hawaoni sura ya hivyo vyandarua. Utapeli na ufisadi mtupi!

Warudishe DDT tunyunyize kwenye mifereji na madimbwi yanayozalisha mbu kama ilivyokuwa huko nyuma. Tena wasi-dilute hiyo dawa maana kinachofanyika hivi sasa wale watu wanaobeba mitungi ya dawa za kunyunyiza wanakuwa hawana dawa yoyote ya maana nadhani wanaweka kiasi kidogo tu cha dawa ili harufu isikike lakini wanakuwa wamejaza maji!! Pia wanalipisha kila nyumba Sh. 2,000 kama sikosei.

Mnyika, pandeni majukwaani mrejeshe uzalendo miongoni mwa wananchi ndio njia pekee ya kuweza kukabiliana na haya yote. If at all you can do that!!! Kabla ya kutunga sera zenu angalieni kwanza namna ya kurekebisha status quo ya kukosekana kwa uadilifu miongoni mwa jamii nzima ya Kitanzania.
 
Umeanisha vyema mnyika,tabia ya mbu haijabadilika bado anazalia kwenye maji yaliyotuama,tukiweza kuthibiti mifereji na mashimo yetu ya vyoo yanayojaa basi tunaweza kupunguza kiasi cha asilimia 70% ya maambukizo na ni cost effective uhitaji $ za Bush! tatizo si sera ni commitment. wataalam wa kinga, viongozi wa siasa na wananchi wenyewe, kama tunaweza kula na kunywa karibu na maji machafu ya ****** na kuona hilo si tatizo tutamaliza vipi malaria?
Wazungu wamegundua siye ni wavivu na zaidi wavivu kufikiri kwa hiyo njia rahisi ni kutumia neti za dawa, kwa sababu kuishi na mashimo ya maji ya mavi ni jadi yetu, ni aibu na matusi,tuache uvivu tuwe wasafi, hakuitaji uwe na pesa za rada ili ufanye usafi.
 
Warudishe DDT tunyunyize kwenye mifereji na madimbwi yanayozalisha mbu kama ilivyokuwa huko nyuma. Tena wasi-dilute hiyo dawa maana kinachofanyika hivi sasa wale watu wanaobeba mitungi ya dawa za kunyunyiza wanakuwa hawana dawa yoyote ya maana nadhani wanaweka kiasi kidogo tu cha dawa ili harufu isikike lakini wanakuwa wamejaza maji!! Pia wanalipisha kila nyumba Sh. 2,000 kama sikosei

Mjadala mzuri huu

DDT haina madhara yeyote, nchi zote ambazo zimeeradicate malaria walitumia. Ingawa sasa hivi watu green revolution wanapinga kutumia DDT eti ina madhara kwa viumbe anuwai. Na sisi tulio nchi maskini ndo kabisa, nyuma kidogo Zimbabwe walitumia kwenye kumaliza tatizo la Mbu, matokeo yake Tumbaku ambayo ilikuwa inachangia uchumi wa taifa ilipigwa marufuku pamoja na mazao mengine ya Kilimo kutoka Zimbambwe eti yana vimelea vya DDT. Uchumi wa Zim ulishuka. SA wanatumia na hata India wamepunguza sana mazalia ya Mbu kwa DDT. Sisi Tanzania ni wakati sasa wa kuitumia kwenye Indoor Residue Spray na kuweka miundo mbinu vizuri. Ni aibu taifa lenye uhuru miaka 59 bado sewage system iko mbovu na sasa tunaota kuweka flyovers !

Matatizo ya kutumia DDT yalikuzwa na huyo mwanamazingira Rachel Carson na kitabu chake cha Silent Spring 1962. Marekani walikiadopt na kuzuia matumizi ya DDT kulinda ndege na accumulation ya DDT kwenye food chain. Lakini hakuna madhara yaliyothibitishwa kwenye matumizi ya DDT.

32eba2c008a0245df0489010.L._AA240_.jpg


National Malaria control Programme pale kwa Dr Mwita niwakati sasa tuanze kuitumia kuangamiza mazalia ya Mbu vyandarua ni suluhisho la muda mfupi
 
Mbu ni hatari.
Hatuwezi kumaliza shida ya malaria kwa vyandarua pekee. Maana pamoja na kuwa na vyandarua mbu wataendelea kuwapo. Na malaria itaendelea kuwapo.
Dawa ya kumaliza malaria ni kuharibu mazalia ya mbu na pia na matumizi ya vyandarua. kimoja tu yaani vyandarua pekee hakitamaliza tatizo.
Kampeni yetu lazima iwe kwa vyote viwili.
 
Back
Top Bottom