John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
Nilipokuwa mtoto tulikuwa tukihimizwa kwamba malaria yanayotokana na mazalia na mbu toka kwenye maji yaliyotuama. Wakati huo tulihimizwa kwamba tusafishe mazingira kuhakikisha hakuna maji yanayotuama ovyo.
na pale ambao maji yalikuwa ni lazima yaachwe yametuama basi tulikuwa tukihizwa kufunika ama kupulizia dawa.
Wakati huo kwa kiwango kikubwa tiba ya malaria ilikuwa Chloroquine.
Leo watoto wetu wanahimizwa kwamba kinga kuu ya malaria ni kujifunika kwa vyandarua. Na tiba ya malaria inabadilika badilika mara kwa mara, huku kukiwa pia na habari za kusambaa kwa dawa feki.
Wakati huu tuliwasikia wengine wakiimba 'marufuku DDT' lakini wakati huo huo nchi zingine wanazungumzia DDT.
Suala hili linaonekana kama ni mjadala kuhusu afya na utabibu, lakini asili ya mabadiliko haya ya mara kwa mara ni maamuzi ya wanasiasa kuhusu sera gani iwe kipaumbele katika kutafuta kinga na kutoa tiba ya ugonjwa husika.
Hiyo tujadili hapa; sera ipi ni muafaka zaidi katika kupambana na malaria? Je, mbinu zinazotumika hivi sasa zinakidhi haja? Zipi ziwe mbinu mbadala?
JJ