Siasa na nyongeza ya mishahara/maslahi bora kwa watumishi wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa na nyongeza ya mishahara/maslahi bora kwa watumishi wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Listener, Mar 20, 2012.

 1. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mafunzo mbalimbali yanaendeshwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma chini ya Programu ya KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA (PSRS) ya 2008 - 2012 na mwaka huu niyo inamalizika kabla ya kufanya tathmini. Programu hii inajumuisha mambo mengi likiwemo suala la maadili kwa watumishi wa umma. Kimsingi hapa yanajitokeza maadili katika ngazi mbili tofauti:

  1. Maadili ya utumishi wa umma ikimaanisha kanuni za msingi ambazo watumishi wa umma wanapaswa kuzizingatia katika utendaji wao wa kila siku. Kanuni hizi zimeainishwa katika kijitabu cha maadili ya utumishi wa umma (2005) ambazo ni pamoja na:
  (i) Kutoa huduma bora
  (ii) Utii kwa Sheria
  (iii) Bidii ya kazi
  (iv) Kutoa huduma bila ya upendeleo
  (v) Kufanya kazi kwa uadilifu
  (vi) Kuwajibika kwa umma
  (vii) Kuheshimu sheria
  (viii) Matumizi sahihi ya taarifa
  2. Kwa upande mwingine maadili ya viongozi wa umma yameanzishwa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi Na. 13 ya mwaka
  1995 likijumuisha viongozi wa kisiasa na viongozi wa kuteuliwa.

  HOJA:
  a. Imeonekana kuwa rahisi sana kwa watumishi wa kawaida wa umma kusimamishwa au kufukuzwa kazi kwa kukiuka taratibu za msingi za kiutendaji lakini hali imekuwa tofauti kwa viongozi. Suala la kujiuliza ni je kuna tofauti gani kati ya haya makundi mawili kwani yote yanaitumikia jamii.

  b. Kwa nini Serikali inaendelea kuwalipa watumishi wake mshahara mdogo huku ikitambua fika kuwa kipatao kidogo kwa watumishi ndiyo chanzo kikubwa cha ukiukaji wa maadili hasa upokeaji wa rushwa? Semina, warsha na makongamano mengi katika programu hii yanaonekana kama sehemu ya kuwaonya na kuwasisitiza zaidi watumishi waenende katika utendaji mwema kwa mujibu wa kanuni za maadili huku ikifahamu fika kuwa maslahi ni chanzo cha matatizo yao ya msingi katika kujikimu kimaisha.

  Nawakaribisha kuchangia kwani pamoja na tume kuundwa kuchunguza suala la nyongeza za mishahara bado kiasi kinachoongezwa ni kidogo mno kulinganisha na hali ya sasa ya maisha ya kitanzania

  MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE (VIONGOZI, WATUMISHI NA WANANCHI WAKE WOTE KWA UJUMLA) AMEN
   
 2. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio mshahara, tatizo ni kupanda kwa ghafla kwa hali ya maisha kusikoendana na kipato, ukipatikana mumo mzuri wa kudhibiti upandaji holela wa bei za bidhaa basi hata wenye mishahara midogo inaweza kusurvive. lakini kupandisha mishahara wakati vitu vinapanda kwa kasi haitasaidia.
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama mtumishi wa umma NAMBA ONE JK hafuati hata moja kati ya hayo, ni miujiza gani unategemea kwa walio chini yake kufuata hayo
  1). Kutoa huduma Bora. Serikali ya JK imeshindwa kutoa huduma bora za Afya kwa watanzania hadi kupelekea madaktari kugoma
  2). Utii kwa Sheria. JK amewasamehe wezi EPA baada ya kurudisha pesa walizoiba, badala ya kuwapeleka mahakamni
  3). Bidii ya kazi. Working rate ya JK < 30% ameshindwa kuchukua maamuzi mazito kwa masuala mazito ya Kitaifa, mfano kuwashughulikia mafisadi, kuwavua magamba mafisadi walio ndani ya CCM
  4). Kutoa huduma bila upendeleo. JK ameonesha Upendeleao kupindukia kwa kuwachangua wanamtandao walimuoweka madarakani katika nafasi nyeti za uongozi.
  5). Kufanya kazi kwa uadilifu. JK hana uadilifu wowote, amefisadi na kujilimbikizia rasilimali za nchi hii kwa mgongo wa mtoto wake Ridhwani Kikwete.
  6). Kuwajibika kwa Umma. Ameshindwa kuwajibika kwa umma, hata pale umma ulipokataa kuongozwa na wateule wake wabovu. Mfano DRS Mponda na Nkya.
  7). Kuheshimu Sheria. amewaachi huru WAUAJI wa KOMBE hata baada ya kuwa wamepatikana na hati ya kua mbele ya mahakama kuu, pia ameendelea kuwalinda wezi wa rada.
  8) Matumizi sahihi ya taarifa. Hata baada ya taarifa za HAZINA na BoT kuonesha kwamba serikali imefilisika haina pesa ameendelea kutalii nchi mbalimbali bila kuzingatia taarifa ya uchumi wa nchi.
   
Loading...