WanaJF,
Jana taifa limepata pigo kwa kukosa fedha za MCC takriban TZS 1.05Trillion ambazo zinatosheleza kujenga zahanati kata zote nchini, kuongeza kasi ya upatikanaji wa umeme hadi kufikia 57% ya kaya zote, kuweka maji kwenye vijiji vyote visivyo na maji nchini.
Kwanza kabisa masharti ya MCC hayakutolewa katikati ya mkataba bali yalikuwepo tangu awali wakati wa kupitishwa kwa MCC 1 kwamba serikali itapewa fedha hizo endapo itadumisha demokrasi, haki za binadamu, utawala bora, Utawala wa Kisheria, uwazi, nk. Hivyo MCC walivyoona baadhi ya vipengele (utawala wa sheria na Haki za binadamu) MCC waliwakumbusha serikali ya CCM kuhusu ukiukwaji huo unaoweza kuikosesha sifa ya kupewa msaada huo na wakapewa muda wa kufanya marekebisho.
swali nimejiuliza kwa nini tumekosa fedha hizo? majibu Yake????????
SUALA LA ZANZIBAR
Tume ya uchaguzi Znz ni huru kama inavyosemekana maamuzi yake hayaingiliwi na mamlaka yoyote (URT ama SMZ).
Lakini pili tume ni taasisi na maamuzi yake lazima yafuate utaratibu wa kitaasisi yaani Board/committee ikae na kufikia maamuzi yake kwa wajumbe wote kuafiki ama kutoafiki jambo hilo. Maajabu ni pale tume haikukaa kama taasisi badala yake familia moja ilifanya maamumuzi na kuyaita ya tume.
baada ya maamuzi hayo tulitegemea mamla za juu kumchukulia sheria mtendaji huyo. Hata hivyo tulitegemea mamlaka za juu zingechukua hatua kwa ukiukaji huo mkubwa wa kisheria aidha kwa kumwajibisha mhusika na kuendelea na mchakato ama kumuondoa kwenye nafasi hiyo na kuitisha uchaguzi mpya, badala yake yote hayakufanyika
Kwa mujibu wa Tume mtu yeyote atakayezuia mchakato wa uchaguzi kabla, wakati ama baada ya upigaji kura lazima sheria ichukue mkondo wake kama ilivyokua kwenye sheria ya Mita 100+. Tulitegemea Tume ya Zanzibar ingechukua hatua kwa wale wote aliyehujumu uchaguzi wa Zanzibar na kufanya uchaguzi huo ufutwe na tuambiwe jinsi walivyoharibu uchaguzi huo hadi leo hakuna wala mamlaka za juu hazijachukua hatua.
Leo MCC wamesema hawatupi hela tunasema wametupa masharti magumu, Kweli kuna ugumu wowote kwenye sheria tulizojitungia wenyewe? Hivyo basi:
Kwa nini Jecha Salum Jecha asiwaombe watanzania wote radhi kwa maamumuzi yake yaliyopelekea familia zaidi ya million 3 kuendelea kuteseka kwa maamuzi aliyoyafanya bila kushirikisha tume nzima?
Kwa nini Jecha Salum Jecha asijiuzulu sasa hata kama alishinikizwa iwe ni uwajibikaji kwa maamuzi yake (bila kujali yalikua sahihi ama la)?
Sheria ya Makosa ya Mtandao
Wakati wa upitishaji wa sheria hii mengi yalisemwa na wadau wengi hasa ule utaratibu wa kupelekea kwa dharura, maudhui ya mswaada na utaratibu uliotumika kuupitisha. sio tu ulilalamikiwa na wabunge wa upinzani bali vyombo vya habari, mashirika ya haki za binadamu, wanasheria n.k lakini bado wanaccm walipitisha kwa kauli moja Ndiooooooooo
Kama hiyo haitoshi mwenyekiti wa CCM ambaye wakati huo alikua Rais wa Jamhuri alisaini mswaada huo na kuwa sheria ambayo leo hii imeusababishia umma wa Tanzania kukosa fedha kiasi cha familia zaidi ya 3miilion zitateseka kwa maamuzi hayo. Hivyo basi
Je kwa nini Mwenyekiti wa CCM asijiuzulu kwa maamuzi yake hayo aliyoyafanya akiwa Rais bila kujalisha alikua na nia njema au la maana hizi kaya zaidi ya 3million ni pamoja na wanachama wa vyama mbalimbali na hata ccm na wasio na vyama. watu hao ndio waliopigia CCM kura leo hii wameambulia kunyimwa haki yao
Kwa nini wanaccm hasa wale wabunge waliopitisha mswaada huo wakiongozwa na aliyekuwa spika wa Bunge wasiombe radhi watanzania kwa maamuzi yao hayo?
Kwa nini uongozi mzima wa CCM Taifa wasiombe radhi watanzania kwa kuwa na serikali isiyo sikivu na ikiwezekana wajiuzulu nafasi zao kwa serikali yao kushindwa kutimizia matakwa ya wananchi
Kuwajibika kisiasa sio dhambi wala aibu ni ukomavu wa kisiasa, ni utu, ni heshima kwa wale uliokuwa unawatumikia na kuonyesha kuwajali. Lakini kubwa zaidi ni uwajibikaji kwa unaonesha kwa hali ya juu kabisa kuwajibika kwa maamuzi mtu aliyoyafanya wakati akiwa kiongozi