Siasa na dini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa na dini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Jun 21, 2010.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Rais Kikwete awaweka njia panda maaskofu, masheikh Send to a friend
  Monday, 21 June 2010 08:53


  Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa

  Phinias Bashaya, Bukoba

  RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba, wanasiasa waoga wanaoweza kutafuta madaraka kwa udini ni hatari na kuomba taasisi za dini nchini, kuwafundisha waumini wao kuwakataa wanasiasa hao kwenye uchaguzi wa Oktoba kwani wanawaeza kuingiza nchi katika maangamizi makubwa.

  Kauli ya Rais imekuja kipindi ambacho baadhi ya wanasiasa wameanza kutumia udini, kutafuta madaraka katika uchaguzi mkuu huo wa Oktoba mwaka huu, ambao mkuu huyo wa nchi anatarajiwa kugombea tena ngwe ya pili na leo anachukua fomu Dodoma.

  Onyo hilo alilitoa mjini Bukoba, alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Jubilee ya Injili katika Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambayo pia yalihudhuriwa na wawakilishi wa majimbo rafiki kutoka nchi mbalimbali duniani.

  Rais alionya, "mchezo wao ni mauti yetu sote, tusiwaendekeze…,siku ambayo tutaruhusu ubaguzi huo ndiyo mauti yetu, tujihadhari na viongozi hawa waoga na wasiojiamini ambao wanapenda madaraka kwa gharama yoyote.”

  Alifafanua kwamba, wapo wanasiasa waoga na wasiojiamini ambao wako tayari kutafuta madaraka kwa gharama yoyote kwa kutaka kueneza ubaguzi dhidi ya wapinzani wao, ili kujiimarisha kisiasa na kuwaomba viongozi hao, wasiwape nafasi kwani wanaweza kuipeleka nchi katika machafuko makubwa.

  Mkuu huyo wa nchi, aliwataka viongozi wa madhehebu ya dini kuwaelekeza waumini wao kuwachagua viongozi waadilifu na kuwasaidia kuwatambua viongozi safi na ubora wa sera za vyama mbalimbali vya kisiasa.

  Katika kuonyesha msisitizo, pia Rais alibainisha kwamba serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa kuabudu huku akionya kuwa siasa zina tabia ya kuchochea ubaguzi na kuwaomba viongozi hao kulisaidia taifa ili lisielekee kwenye misingi itakayowafanya watanzania kubaguana.

  Aliongeza kwamba, madhehebu ya dini yana wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuwaandaa viongozi watakao kuwa na maadili mema ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya rushwa na maasi yanayokwenda kinyume na utamaduni wa Watanzania.

  Awali, kabla ya Rais Kikwete kuelekea katika eneo la maadhimisho hayo, kundi kubwa la wananchi lilijikusanya nje ya Ikulu ndogo mjini hapa likidai linataka kumuona rais ili ashinikize kufanyika kwa zoezi la kuwatafuta ndugu zao wanaodaiwa kufa maji katika ajali ya mtumbwi iliyotokea juzi.

  Kundi hilo ambalo baadhi yao walidai wamewapoteza ndugu zao huku wakiwa hawaoni jitihada zinazofanywa na serikali kuwatafuta baadaye lilifuatwa na maafisa wa usalama na kuwataka waondoke eneo hilo kwani wasingeweza kumuona rais na badala yake kushauriwa kumfuata mkuu wa wilaya ya Bukoba Samwel Kamote.

  Wananchi hawakufanikiwa kumuona kiongozi huyo baada ya kudhibitiwa na wanausalama huku Alistides Gerase (43) akisimulia jinsi alivyookoka na kuwashuhudia abiria wenzake wakizama katika maji.

  Mwananchi mwingine Bayona Honorath (32)alidai ndugu yake aliyekuwa abiria katika mtumbwi huo uliozama siku mbili zilizopita mwili wake ulikuwa haujapatikana.

  Katika salamu zake Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Elisa Buberwa, alisema kanisa hilo litatumia fursa lilizonazo kuwaeliisha waumini wake jinsi ya kuwapata viongozi wenye uwezo na waadilifu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

  Askofu Buberwa aliweka bayana kwamba, kanisa hilo litawafundisha waumini kuzingatia sheria za uchaguzi kama zinavyoainishwa, ambapo pia sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Alex Malasusa pamoja na wawakilishi wa madhehebu mengine.
   
 2. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na mheshimiwa Raisi kwamba udini ni hatari sana katika usalama, amani na umoja wa taifa. Katika uchaguzi mkuu kumeanza kujitokea harufu ya udini tatizo ambalo likifumbiwa macho linaweza kutupeleka pabaya. Watanzania wengi bado ni waumini wa dini na hasa za kikiristo na kiislamu. Zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ni waumini wa dini hizi kuu mbili.

  Imani za kidini na heshima kwa viongozi wa dini vina athari kubwa katika mfumo wa maisha yetu. Hiyo pia inatokana na ukweli kwamba mafundisho na amri za kidini huwa hazina mjadala. Padri au Askofu akisema kupiga kura ni dhambi, asilimia kubwa ya waumini wake watamuamini bila kuhoji. Inakuaje sasa kama padri au sheikh anawaambia waumini wake tunataka kubadilisha utawala uliopo na kuleta utawala mwingine iwe ni kwa lugha ya moja kwa moja au kwa taashira ya kizushi.

  Kwa maoni yangu kuna haja serikali ikaangalia upya juu ya taratibu zake za kuratibu taasisi za dini. Utaratibu uliopo wa kuandikisha taasisi za kidini kama taasisi zingine za kawaida zisizo za kiserikali naona hautufai. Taasisi za kidini zinapaswa kuwa na usajili wake maalumu na masharti tofauti na ya NGO za kawaida. Taasisi za kidini hasipaswi kuruhusiwa kutoa elimu ya uraia au elimu ya kupiga kura. Wakitaka kufanya hivyo waanzishe taasisi ya kawaida yenye malengo kama hayo.
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135


  George Jinasa kama kungekuwa hakuna viongozi wa dini wanaotoa tahadhari na kukemea waumini wao kuhusu kutenda mabaya tungekuwa wapi leo? Kumbuka kuwa lengo la viongozi wa dini ni kuona amani na mshikamano wa kitaifa na ulimwengu kwa ujumla vinalindwa na waumini wake.

  Hata hao viongozi wanaotaka kuwa madarakani wanajua namna ya kuwafikia watu wengi zaidi ni kwenye nyumba za ibada, iwe kanisani ama msikitini. Viongozi wa dini wana ushawishi wa kuwatuliza waumini na hivyo kufanikisha kuwepo kwa amani kwa nchi husika.

  Kuhusu taratibu za kusajili taasisi za kidini kwa taratibu mpya ni kazi ya bunge letu kupitia upya katiba yetu na kubadilisha katiba hivyo kwa mapendekezo ya Watanzania likiwepo hili lako.

  Tuelewe kuwa Watanzania wa sasa wanaelewa haki yao iko wapi hivyo wanaitaka. Unapoona mtoto analia elewa ana sababu. Je ana njaa, ameumizwa/ameumia? Je wewe ukiwa mzazi utampuuza? Kwa nini viongozi wetu wafumbie macho kilio cha wananchi wake. Kwa nini wasiwape wananchi haki stahili?

  Au wewe unakubaliana na hali ya nchi hii. Kama wewe unashiba unaweza usikubaliane na mimi, lakini kama una njaa kama mimi basi lazima uhangaike ili upate mlo. Viongozi wa dini wanataka waumini wao wawe na maamuzi sahihi ya kufanya mabadiliko. Kufanya mabadiliko sio lazima kuwaondoa madarakani walioko madarakani! hata kwa kuwapa kura chache inatosha kuonyesha ni jinsi gani usivyokubalika! Na hii itampa dira kiongozi husika taswira ya watu awaongozao.

  Kama hukubaliki kwa nini usitafute ni kwa nini badala ya kukimbilia kulaumu viongozi wa Dini? Viongozi wa dini hawataacha kusema mpaka hapoviongozi watakapowatendea HAKI watu wake.

   
 4. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  MAJIBU YANGU KWA NDUGU YANGU MANGI
  *

  Ndugu yangu Mangi sina tofauti nawe juu ya nafasi na mchango mkubwa wa taasisi za dini katika kukemea maovu. Hamna shaka yoyote kwamba bila kazi kubwa ya taasisi za kidini katika eneo hilo tungekuwa pabaya. Kwa ufahamu wangu kukemea maovu, kuwafundisha na kuwaongoza waumini katika kumcha Mungu na kutoa huduma za kibinadamu na kijamii ndizo kazi kubwa za taasisi za kidini.

  Taasisi za kidini zinaporuhisiwa kijiingiza katika shughuli zenye harufu za kisiasa siasa kunahitajika umakini mkubwa sana vinginevyo amani inaweza kutoweka. Maandiko yanasema imani inaweza kuvunja hata milima. Fikiria ndugu zangu wa moja kati ya imani za dini hapa nchini walikuwa wanawafundisha waumini wao wasipige kura. Mafundisho hayo yalikuwa yanatolewa katika misingi ya kiimani. Nini itakuwa athari yake? Sasa kama viongozi wa kidini watawahubiri waumini wao wampigie mtu fulani au chama fulani tunategemea nini? Uzingatie kwama katika taasisi zao za kidini kuna watu wa vyama na itikadi mbalimbali za kisiasa. Chukulia hawa ni chama tawala na wale ni chama pinzani, huoni kwamba hawa wengine utawaweka kwenye nafasi ngumu na tata ya kuchagua mafundisho ya dini au mitizamo yao ya kisiasa? Nijuavyo mimi, viongozi wetu wa dini wamebobea zaidi katika fani ya dini. Katika waumini wao wapo waliobobea katika fani za siasa, utawala, uchumi na fani nyingine nyingi za kidunia. Ukiondoa kofia ya upadri au ushehe huyu muumini anaefundishwa awapigie wanamabadiliko anaweza kuwa na ueleo na upeo mkubwa wa kisiasa na uchumi kuliko baba askofu au sheikh. Lakini akimpinga japo yeye ni sahihi ataambiwa ameenda kinhyume na mafundisho ya Mungu.

  Mimi nilikuwa naona taasisi za dini ziwaachie wanasiasa na wataalamu wengine kufanya mambo ya siasa. Lau baadhi ya viongozi wa dini wakiona umhimu kufanya siasa wafanye kama mama Lwakatare. Wajiunge na vyama vya siasa wagombee. Wakiwa kanisani wafanye mambo ya dini na wakiwa katika vyama vyao wahubiri siasa. Au wafanye kama DR SLAA. Watoke katika uongozi wa dini wawaachie wengine waingie katika siasa.

  Vinginevyo chaguzi zijazo zitakuwa zinaamuliwa kwa misingi ya udini jambo ambalo sio dalili nzuri. Tukifika huko hata heshima za viongozi wa dini zitashuka. Kwa sasa viongozi wa dini wanaheshimika sana katika vyama vyote na vyombo vya serikali maana wanachukuliwa ni watu wasio na upande katika mivutano ya kisiasa. Ningekuwa kiongozi wa dini ningependa tubaki hivyo hivyo.

  Mimi ni binaadamu mwenye mapunguvu kama nitakuwa nimekosea natanguliza ungamo langu. Lakini nimetoa maneno haya kwa nia njema kabisa na nikiamini ni utaratibu muafaka kwa nchi kama Tanzania ambayo ina idadi karibu sawa ya waumini kati ya dini ya kikristo na kiislamu. Leo tunaanza kuwaonyesha waumini mtu wa kumchangua tukinogewa tutaka kuondoa serikali ya kisekula na kuweka serikali ya kikiristo au kiislamu.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hili swala la udini nadhani wamelipandikiza mafisadi wenyewe ili kuonesha kuwa upinzani uko katika masuala ya udini. Hivi mwenye data kamili atueleze kama Slaa aliwahi hata siku moja kuongelea kuwa anapinga baadhi ya dini au imani? Badala ya kutueleza ni kwanini wameshindwa kutekeleza ilani zao za uchaguzi tangu uhuru wao wanaongelea masuala ya udini!
   
 6. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani ni bora tukaupa ukweli nafasi yake kuliko tukasubiri mpaka ukweli tunaoficha ukazaa matatizo. Kwa hali tuliyonayo sasa lazima tukubali kwamba Tanzania tuelekea katika udini kwa mbio na sio kutembea. Sipendi tuyosheane vidole ya kwamba ni nani aneyepiga ngoma hii na wachezaji wake bali napenda kukubaliane kwa msingi kwamba udini kama tutauachia utatuchimia makaburi sisii na vizazi vyeti. Watoto na wajukuu zetu ambao wanaweza kuwa wahanga wakubwa wa mbegu hii tunayoipanda au tunayoichekelea watatulaani huko baadae na kukojoa juu ya makaburi yetu. Baba zetu na babu zetu bila kujali tofauti zao za kidini walitujengea Tanzania ya amani na upendo ambapo punda, wanakondoo, mbwa mwitu na chui waliishi pamoja bila ya kuzuliana.

  Kama tutaamua kulificha tatizo katika nafsi yetu na kuliita kama sio tatizo kwa midomo yetu tutakuwa tunajidanganya wenyewe. Aidha, tutakuwa hatuwasaidii viongozi wetu wa dini na siasa. Kama wananchi wa kawaida tutawakemea wanasiasa na viongozi wetu watakaoonesha dalili za udini na waumini tukawakemea viongozi wetu wa kidini wanaoelekeo huko mambo haya yataisha na nchi yetu itabaki ya amani na utulivu.

  Madhara ya udini, ukabila na umajimbo tunayashuhudia katika vyombo vya habari na tumekuwa tukiyashuhudia. Kwa wale waliokuwa wakiishi katika mipaka ya Tanzania na Rwanda wakati wa mauwaji ya kimbari walishuhudia maiti za mwanaadamu aliye na umbo bora na takatifu ikielea majini huku ikiwa imeharibika mamia kwa mamia. Tumeshuhudia yaliyotokea Nigeria, Sudani, Iraq na kwingineko. Tanzania limekuwa kimbilio la wakimbizi toka Rwanda, Burundi, Somalia nk tukiachia pengu kama hizo zimee tutakimbilia wapi? Watoto na wajukuu zetu watakimbilia wapi?

  Yawezekana kwamba tukawa na matatizo makubwa ya kiuchumi na kisiasa. Yasitukatishe tamaa na kuyafanya kuwa matatizo makubwa kama matatizo ya udini. Matatizo ya kiuchumi na kisiasa yanaweza kuisha kiurahisi tu lakini matatizo ya udini yakifikia kilele chake yanaisha kwa kudura za Mungu tu.
   
 7. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Naomba tulijadili hili kwa uzito wake
   
 8. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Hizi propaganda hazisaidii. Lete data na siyo mawazo ya kufikirika!
   
 9. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu yawezekana nikawa nimepotoka kama walivyopotoka wengine au nikawa nimepatia kama walivyopatia wengine. Msimamo wangu kama nilivyoubainisha toka mwanzo siko tayari kumnyooshea mkono yeyote katika hili na wala siko tayari kuanzisha malumbano yoyote katika suala nyeti kama hili. Kama tatizo hili halipo Tanzania wala halinukii tumshukuru Mungu na tumuombe atuepushe nalo. Kama lipo pengine ndugu yangu unayonipinga hujalibaini walioniskia na wanaohusika wazingatie ushauri wangu kama wakiuona ni sahihi. Hamna katika wanaadamu anayeweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba anajua kila kitu na anaona kila kitu.
   
 10. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  George, unapo'claim' kuna udini lazima uwe na uthibitisho kuwa upo - mfano, either wewe mwenyewe ulishabaguliwa kupata haki yako au ulishuhudia mtu akibaguliwa kwa misingi ya dini au wewe mwenyewe ni mmojawapo wa watu wanaobagua watu kwa misingi ya dini nk. Kwangu mimi mazingira kama haya - kubaguliwa hospitali, kupata elimu, kupata ajira - kwa misingi ya dini ndiyo ninayoyaita udini. Yaani, kwa kawaida udini unakuwa kwenye mfumo wa utawala - kutoa haki na huduma za jamii!

  Otherwise, kilichopo ni baadhi ya viongozi wa siasa kupiga propaganda za kidini kwa ajili ya maslahi yao au baadhi ya waendesha mihadhara ya kidini kutumia mahubiri yao kupandikiza mafundisho hasi katika vichwa vya waumini wao kwamba Wakatoliki au Wakristo walimchagua Dr Slaa kuwa rais na Waislamu walichagua kiongozi ambaye waliona anafaa! Maana hata huo udini unaosemwa unaelekezwa kwa Wakristo na unamhusisha Dr Slaa na Chadema. I can't buy this nosense! Tatizo kama hili mimi naliita 'projection' - yaani mtu anahamisha matatizo yake binafsi na kuyaweka kwa mtu mwingine na kisha anadhani kuwa yule mtu mwingine ndiye mwenye tatizo wakati tatizo ni lake mwenyewe.

  Propaganda hizi kwa mazingira ya Tanzania hazitafanikiwa ila zitafanikisha maslahi ya kisiasa (wakati wa kampeni) kwa vile zina'bank on' ignorance na poverty of people! Ukitaka kuthibitisha kuwa Tanzania hakuna udini ona mitaani tunakokaa - hakuna shida kati ya Wakristo na Waislamu au waumini wa dini nyingine na tunasaidiana kwa kila hali na mali. Mimi ni Mkristo na mtaa ninapokaa nimezungukwa na Waislamu lakini hatuna tatizo na wakati mwingine tukiulizana kuhusu udini huwa tunaishia kusema 'tunausikia kwa viongozi wetu wa juu na ndio wenye tatizo hilo na siyo kwetu mitaani'.
   
 11. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kikwete na ccm ndo mdini mkubwa na mnafiki. ndo amelata mambo ya mahakama ya kadhi, OIC, na teuzi zake nyingi anangalia dini yake ya uislam zaidi badala ya qualification na competences. ofizi nyingi za balozi za nje zimajaa waislam wasio na sifa na elimu.
   
 12. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu siwezithubu kusema kwamba tuna ubaguzi katika huduma za afya, elimu na nyingine kama hizo. Na pia mimi binafsi si muathirika wa ubaguzi wa kidini wala si muumini wa ubaguzi wa kidini wa aina yoyote. Kwa bahati nzuri katika familia yetu tumegawanyika katika dini na imani tofauti na tuna upendo wa karibu sana.Tunaweza kuwa na tofauti katika tafsiri ya udini. Mimi naweza kuona udini ni zaidi ya hapo. Kama kwa mfano mimi nitampigia kura X kwa kuwa ni mbudha mwenzangu au nitawahamasisha watu wasimpigie kura Y kwakuwa si mbahai mwenzangu huwo utakuwa udini hata kama simbagui Y katika huduma za afya, elimu na nyinginezo.

  Sitaki kutoa ushahidi wala kusema kuwa ninaushahidi wa moja ka moja wa udini. Lakini unaposema kuna watu wanahubiri katika majukwaa ya dini kwamba kuna udini hiyo sio dalili ya kupuuziwa. Ukiona kuna madai kwamba kuna watu wamempigia kura kiongozi fulani na kutompigia fulani kwa sababu ya dini sio dalili ya kupuuziwa. Ukisikia watu wanadai kwamba mtu fulani au watu fulani wamepewa vyeo fulani au wamenyimwa vyeo fulani kwa sababu ya udini pia sio dalili ya kupuuziwa. Mimi navyoona matatizo ya ubaguzi huanza kwa hisia. Yawezekana tukawa hatuna ubaguzi wa dini Tanzania laikini hisia za ubaguzi wa dini tunazo. Kama hatuna haja ya kupambana na udini kwakuwa halijawa tatizo Tanzania tupambane na hisia za udini ambazo zinaweza kutupelekea kwenye udini.

  Najua kwamba bado ni watanzania wachache wenye hisia za udini bila kijali imani zao. Hatuwezi kuwalaumu waumini wa dini au dhehebu fulani kwa kuwa kuna wachache kati yao wenye hisia za udini. Tutafute chanzo cha hisia hizi na namna ya kuziondoa kistaarabu. Tunahitaji kuelimishana zaidi na kuweka mahusiano ya karibu ili kuziona tofauti zetu za kiimani katika maisha yetu ni sawa na tofauti za urefu, ufupi, wembamba na unene.
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Tanzanians, learn from Sudan. It is coming.
   
 14. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kuna mchangiaji hapa yeye anasema udini upo lakini ndani ya CCM. Anasema Raisi Kikwete ameanzisha Mahakama ya Kadhi, OIC na anachagua watu kwa kuzingatia dini zao na sio qualification. Mimi sina uhakika sana uhuru na uadilifu wetu katika kuchangia hoja. Tunachangia hoja kwa kuzingatia hoja na ukweli wa mambo au tunaangalia maslahi yetu ya kidini na kisiasa? Tuko tayari kuukubali ukweli hata kama unatoka Chadema na sisi ni CCM na kinyume chake?Tuko tayari kuukubali ukweli hata kama unatoka kwa mkristo japo sisi ni waislamu na kinyume chake?

  Tunamlaumu Kikwete kuanzisha hoja ya Mahakama ya Kadhi na OIC. Tunamlaumu kwa haki? Nani asiejuwa kwamba hoja ya Mahakama ya Kadhi inachimbuko lake katika vyama vya upinzani kipindi cha utawala wa mh. Mkapa? Muasisi wa hoja hiyo hakuwa muislamu wala CCM bali alikuwa ni mkristo na wa chama cha upinzani kilichokuwa na nguvu kuliko vyote kwa wakati huo (NCCRE MAGEUZI) .Na hakuanzisha hoja hiyo kwa sababu ya maslahi yake ya kidini bali kwa maslahi ya kisiasa akizingatia waislamu ni sehemu kubwa ya wapiga kura. Hoja hiyo iliibiwa na CCM kipindi cha Mkapa, ikaingia Bungeni na kujadiliwa mara kadhaa, ikaundiwa na kamati na ikatumia fedha za wapiga kura kutafiti uzoefu wa nchi nyingine za Afrika zenye Mahakama ya Kadhi. Hoja hiyo iliingizwa na CCM wakati wa wenyekiti wa Mkapa katika Ilani ya Uchaguzi wa CCM ambayo chini ya Ilani hiyo hiyo iliibuka na ushindi wa zaidi ya asilimia sabini. Hamna mtu aliyemuuita Mrema wala Mkapa mdini wala hamna mtu aliekiita chama cha NCCR Mageuzi au CCM ni cha kidini. Iweje leo mmuite Mh. Kikwete mdini kwa suala aliyorithi kutoka kwa waliomtangulia ambao hawajapata kuitwa wadini?

  Suala la OIC lilianza toka wakati wa mh. Mwinyi. Na mmoja aliyelipigia debe sana alikuwa ni Waziri Mkuu Msataafu Mh John Malesea ambaye sio muislamu. Sababu alizozitoa kuunga mkono Tanzania kujiunga na OIC zilikuwa za kisiasa na kiuchumi. Kama alikososea au la, makosa yake hayana uhusiano na ushawishi woowte wa kidini.

  Kwamba mh. anachagua watu bila qualification ni hoja ambayo inadhihirisha hisia za udini tulizonazo. Watanzania (baadhi yetu) bado hatuaminiani kwa sababu za misingi ya udini. Raisi akiwa mkristo watanzania wenye maradhi ya hisia za udini watakuwa na hisia kwamba anapendelea wakristo wenzake. Akichaguliwa kiongozi mkristo kutakuwa na hisia kwamba amefanya hivyo kwa kuwa ni mkristo. Ni tatizo hilihili linalomkumba Mh. Kikwete. Ni tatizo hili hili linaloweza kuwafanya baadhi ya wapiga kura wasimpigie au washawishi wenzao wasimpigie kwa sababu za hisia zao za kidini. Watanzania tunapaswa kujitambua na kukubali utanzania wetu wenye tofauti za dini, kabila, siasa na rangi. Tuenzi misingi mizuri wliotuachia wazee wetu ambao wameendesha nchi kwa miongo kadhaa bila kuwa na hisia za maana za udini.

  Kwa hili pia nakubaliana na maoni ya ndugu yangu Magobe kwamba linachangiwa na umasikini wetu na uchache wa elimu. Watanzania tunapaswa kuelimishana juu ya hili na kuelekeza mapambano yetu kwa pamoja katika kuinua uchumi wa nchi ili kuondoa umasikini. Tupambane na ufisadi na ubadilifu wa mali ya umma kwa uadilifu na ukweli bila kuweka mbele ushabiki wa kisiasa na udini.
   
 15. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Kuhusu kumpigia kura mtu fulani kwa misingi ya dini ni 'speculations' tu. Hakuna kwenye data. Kwamba baadhi ya viongozi wa dini waliwahubiria waumini wao wapige kura kiaina inaweza kuwa kweli ingawa baadhi ya viongozi wa dini walisingiziwa pia. Mimi ninataka tukiongea vitu tuongee vile ambavyo tunaweza kuvithibitisha na kama hatuwezi na bado tunaviongelea tunakuwa tunajidhalilisha. Namna hii ya kufikiri mimi naiita 'intellectual masturbation'.
   
 16. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Kitu ambacho nimegundua pia ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vinafanya 'propaganda' (kutoa ushawishi kwa wasomaji na kwa umma wakati kitu kinachozungumziwa hakipo ila kinafanywa kama kipo). Vyombo hivi haziripoti matukio au habari bali vinatoa maoni kulingana na 'perception' yao. Wakifanya hivyo, wana'form an opinion' juu ya kitu fulani. Mind you an opinion is not a fact! Halafu sisi tunatoa maoni juu ya maoni ya mtu fulani juu ya kitu fulani. Hapa ndipo tunapokosea. Tungekuwa tunatoa maoni juu ya tukio fulani na siyo maoni ya mtu juu ya tukio fulani. Mwisho wa siku, unakuta kwamba maini yatu mara nyingi yamejenwa juu ya maoni ya watu wengine na siyo kile kilichotokea. Mfano, The SundayCitizen ya Aprili au Mei 2010 waliandika habari fulani juu ya Ilani ya Christian Professionals of Tanzania (CCT) kuhusu Uchaguzi Mkuu 2010. Kichwa cha habari kilikuwa kinasema (nitaandika kwa kiswahili maan text yake kwa Kiingereza sina kwa sasa na sitaki nikosee) Kanisa Katoliki linawaandaa waumini wake kumchagua kiongozi Mkristo. Lakini article nzima haikuwa na sehemu iliyosema vile. Baada ya watu kusoma hicho kichwa cha habari na hata bila ya kutafuta hiyo Ilani walianza kuchangia na kulaani vikali na hapo ndipo kauli za udini ziliianza kuibuka. Unaona kitu ninachojaribu kukionesha kuhusu kutoa maoni juu ya maoni ya mtu mwingine na siyo tukio au habari yenyewe?
   
 17. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kitendo cha ccm kuweka mahakama ya kadhi ktk ilani yake ni dhairi kwamba chama hicho ni cha kidini.ndiyo maana viongozi wa kislamu walihamasisha waislamu wampigie kikwete kura maana serikali yake ilihadi mahakama ya kadhi.kikwete ameshindwa kuongoza nchi kwa msingi ya katiba bali kwa matakwa na maslahi ya sehemu ndo ya waislamu.
   
 18. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  lazima ccm na viongozi wa serikali na jk waonyeshe kwa vitendo na wala sii kwa maneno kuwa hakuna upendeleo wa kidini.na wafanye siasa bila kutafuta upendeleo kwa misingi ya kidini.magazeti ya serikali, ya RA, al-huda, al-nuur yanachochea udini.maana habari zake nyingi ni za kutunga
   
 19. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  lazima ccm itambue kuwa wananchi wahitaji demokrasia ya kweli na maendeleo ya haraka na thabiti.chama ni njia tuu ya kupata viongozi kwa mujibu wa sheria ya sasa.hitaji la wananchi sii chama.kwa hiyo mtu yeyote hata kama ni mwanachama wa ccm kama RA lazima afute sheria na taratibu za nchi.
   
 20. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  serikali gani yenye double standard?badala ya kufunga magazeti ya uhuru, daily news, ya RA, alhuda,alnuur yanayochochea udini, wanakemea gazeti lenye quality kama mwananchi?!ccm hovyo kabsa.imejaa watu wenye kujali matumbo yao tuu, hawapo kwa maslahi ya taifa
   
Loading...