Siasa mfu: Zipi tofauti za kazi ya Meya na Mkuu wa mkoa?

gwijimimi

JF-Expert Member
Sep 24, 2011
7,344
3,608
Mimi kuna jambo silielewi. Hivi kila jambo la maendeleo, matamko mkuu wa mkoa ndio anahusika. Sasa kaza ya Meya ni nini?

Jana CRDB wamemkabidhi 100m Makonda kwa ajili ya madawati, sasa hiki cheo cha umeya ni ceremonial ama? Cha kushangaza ndio kinatokana na kura za wananchi.
 
Aliyeomba hizo pesa nani? Makonda aliomba msaada kwa wadau
 
Mimi kuna jambo silielewi. Hivi kila jambo la maendeleo, matamko mkuu wa mkoa ndio anahusika. Sasa kaza ya Meya ni nini?

Jana CRDB wamemkabidhi 100m Makonda kwa ajili ya madawati, sasa hiki cheo cha umeya ni ceremonial ama? Cha kushangaza ndio kinatokana na kura za wananchi.
Mkuu hiyo waachie ccm waendelee na usanii wao, sisi wana ukawa tunapiga mzigo maana crdb haichagui mbunge wala diwani
 
Mimi kuna jambo silielewi. Hivi kila jambo la maendeleo, matamko mkuu wa mkoa ndio anahusika. Sasa kaza ya Meya ni nini?

Jana CRDB wamemkabidhi 100m Makonda kwa ajili ya madawati, sasa hiki cheo cha umeya ni ceremonial ama? Cha kushangaza ndio kinatokana na kura za wananchi.

Mkuu hapa ndio utaona haja ya katiba mpya. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Makatibu Tarafa ni wateule wa Rais, kufanya majukumu ambayo Madiwani na Mayor wangeweza kufanya. Watu pekee ambao mimi binafsi naona wana tija ni Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa.

Hawa wengine ni post za wakuu wa nchi kutolea shukrani kwa waliowafanikisha kuingia madarakani. We don't need them as we don't choose them
 
Simply ni wafanyakazi hewa
 
Tunaishi bila kujua nani afanye nini na wapi.

Hii yote ni kwa sababu ya kujipendekeza kwa watawala.

Ukimpa Meya. Utaonekana ni Mpinzani.

Bado siasa zetu hazijakaa kimaendeleo. Bado tunasiasa mfu. Siasa za Ubinafsi, siasa za kuangalia uchaguzi, siasa za Credit. Siasa za Kuhisiana, Siasa za Kutishana.
 
We hujui kama siku hizi Makonda anafanya ligi ya kutokea kwenye media na Diamond
 
Naamini anaetakiwa kuwa na mamlaka kwenye eneo fulani iwe wilaya au mkoa ni yule aliechaguliwa na wananchi wa eneo hilo.. Lakini kwa hapa Tz wateule wa raisi ndo wenye mamlaka ya hata kuwaweka ndani wawakilishi wa wananchi.. Rasimu ya Warioba iliondoa hii.. Lakini chama dola wakairudisha..
 
Back
Top Bottom