Siasa, Media vs Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,465
2,857
Najua kuna mengi anazungumza anajiita mwanaharakati wa kumtetea JPM aendelee kukalia kiti cha Urais 2020. Mtu wa kwanza kuibua hoja ya kutaka JPM aungwe mkono alikuwa Rostam Aziz (Mbunge wa zamani wa Igunga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha)
Musiba anawatuhumu akina Makamba na Kinana kwa kupanga njama, nadhani kwa mujibu wa Musiba, anaowatuhumu ni kama vile wangependa kubadili gia angani ili CCM iache utamaduni wake wa kumuunga mkono JPM kama mgombea anaetakiwa kupita peke yake 2020 kwenye kinyang’anyiro cha Urais. Kama wazee hawa wana njama za kutaka kusimamisha mgombea wao ni nani? Ana uwezo gani mbadala na maono ambayo yanaweza kutupeleka kwa haraka kuona Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inatimia ili effect yake ipelekee Watanzania kuwa middle class income earners.

Kwa upande mwingine Bashe kasimama ku-allign na alichosema Musiba hali kadhalika Rostam.
Anyway, chokochoko hizi nadhani wanaozileta wanajaribu tu, ila wanajua watafeli.
Wengi tunakumbuka “Komandoo” Salimin Amour mwaka alijaribu kutaka kubadili katiba ya Z’bar ili ongeze muhula wa III. Mpango wake ukafeli. Akajitutumua kutengeneza mgombea ambae atakuwa na uungwaji mkono wake.

Mgombea wa Salim Amour alikuwa Waziri Kiongozi wakati huo Dr. Bilal. Miaka 5 baadae Dr. Bilal akataka kum-challenge tena Amani Karume akiwa anatakiwa kumalizia kipindi cha pili. Bado Bilal aliangukia pua.

Nadhani mafigisu yote hayo hayana tija ukilinganisha na kasi ya JPM kukuza uchumi kwa kutumia viwanda kama tool ya kukuza uchumi. Hawa wengine wanapiga kelele, wamekuwa wabunge na mawaziri na hata hatujui wana strategy ipi kupigana na maadui wa Taifa hili ambao ni UMASIKINI, UJINGA na MARADHI.

Kwa upande mwingine, JPM anafanya kazi kubwa ila wasaidizi wake sijui nini kinafanya wasiendane na kasi yake. It was and it is unthinkable mpaka anafika MZA anashangaa kwanini approval toka wizara ya Fedha haijafanyika ili containers za ujenzi wa MELI unaofanywa na wakandarasi toka Korea uende kwa haraka.

Siasa na propaganda za baadhi ya wastaafu na walioko kwnye nafasi zina makelele ambayo ukipima hayo makelele na mwangwi wake unatutua vip suala la kukuza uchumi wetu tufikie kipato cha kati ambapo spending power ya Watanzania itaongezeka na by default tax base itapanuka.

JPM mara kwa mara anakiri nchi hii ina utajiri, ni wakati umefika tuwe na focus na namna gani tutumie Competitive Intelligence kama tool ya kutusaidia Watanzania ku-maximize kukuza uchumi wetu na wallet zetu kutuna kwa kuzalisha na kuongeza thamani mazao ya kilimo unlike utamaduni wa kuuza mazao ghafi. Ni aibu tunauza pamba kama raw halafu sisi hawa hawa tuna-import nguo. Ni aibu tunauza ufuta nje ya Tanzania kama raw, yet hatuna mafuta ya kula ya kutosha. JPM kana na right strategy ambayo itaongeza thamani na kutengeneza ajira na kuuza final products kwa soko la ndani, EAC, SADC & duniani kote.

Kwa kuwa baadhi ya waastaafu hawakuenda vyema wakiwa madarakani kwa kujituma kufanya kila wawezalo kukabiliana na UMASIKINI, UJINGA & MARADHI;tuna option moja tu, kuendelea na JPM kama mgombea wa Urais ili kukabili maadui zetu wakubwa. Baadhi ya kelele na propaganda zina kusudi tu la kututoa kwenye angenda na maadui wakubwa na kuanza kulumbana kwa hoja ambazo hazina mchago wowote kukuza uchumi wa Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom