Milango ya bwawa la umeme, tani 26 kukodi wichi toka nje, ni kutupiga Watanzania na kitu kizito

Kwa hatua ulipofikia ujenzi wa tuta kuu tunaruhusiwa kuanza kuhifadhi maji (water emponding) isipokuwa hatujaanza kuhifadhi kwakuwa njia ya kuchepusha maji haijafungwa.

Ufungaji wa geti la njia ya kuchepusha maji lina hatua mbili.

1. Kujenga tuta kuu hadi kimo cha mita 95 kutoka usawa wa bahari. Kazi hii imeshakamilika

2. Kufunga mfumo ya kushushia mageti kwenye njia ya mchepusho wa maji. Mageti yalishafika ila mfumo wa kuyashushia unafika mwanzo mwa Januari 2022.
Mfumo ukikamilika kufungwa mageti yatashushwa, na tutaanza kuhifadhi maji.

Ni mfumo ambao ndani una crane na miundombinu wezeshi ya kutumia na kuendesha crane hizo. Crane hizo zinaitwa wire rope hoist crane zimaendeshwa kwa umeme sio hydraulic
Majibu mzuri Tanesco

Swali:
Kwanini vifaa vinavyo hitajika site vichelewe kufika/kuagizwa?

Kuna hujuma kuelekea kufanikisha mradi
 
Kwa hatua ulipofikia ujenzi wa tuta kuu tunaruhusiwa kuanza kuhifadhi maji (water emponding) isipokuwa hatujaanza kuhifadhi kwakuwa njia ya kuchepusha maji haijafungwa.

Ufungaji wa geti la njia ya kuchepusha maji lina hatua mbili.

1. Kujenga tuta kuu hadi kimo cha mita 95 kutoka usawa wa bahari. Kazi hii imeshakamilika

2. Kufunga mfumo ya kushushia mageti kwenye njia ya mchepusho wa maji. Mageti yalishafika ila mfumo wa kuyashushia unafika mwanzo mwa Januari 2022.
Mfumo ukikamilika kufungwa mageti yatashushwa, na tutaanza kuhifadhi maji.

Ni mfumo ambao ndani una crane na miundombinu wezeshi ya kutumia na kuendesha crane hizo. Crane hizo zinaitwa wire rope hoist crane zimaendeshwa kwa umeme sio hydraulic
Hongera sana TANESCO
 
Vibaraka wao tayari wamefika na majibu yao mepesi kwa maswali magumu!

Hili ndilo tatizo letu lingine la kitaifa; yaani wako watu ambao kazi yao ni kuzitetea mamlaka na viongozi wa hizo mamlaka hata kama wanafanya makosa.

Miaka 60 ya UHURU; Ujinga, Umasikini, na Maradhi, havitaondoka kamwe kwa watanzania kwa sababu wasomi ambao ndio waliotakiwa kusaidia taifa hawa maadui waondoke wamekuwa wapumbavu.
Wasomi hawa watoto wa wakubwa huwa wanasoma kweli? Halafu Leo ndio mawaziri mbona kichekesho wapo kimkakati SS tunaotaka maendeleo tuna subiri awamu ijayo.
 
Kwa hatua ulipofikia ujenzi wa tuta kuu tunaruhusiwa kuanza kuhifadhi maji (water emponding) isipokuwa hatujaanza kuhifadhi kwakuwa njia ya kuchepusha maji haijafungwa.

Ufungaji wa geti la njia ya kuchepusha maji lina hatua mbili.

1. Kujenga tuta kuu hadi kimo cha mita 95 kutoka usawa wa bahari. Kazi hii imeshakamilika

2. Kufunga mfumo ya kushushia mageti kwenye njia ya mchepusho wa maji. Mageti yalishafika ila mfumo wa kuyashushia unafika mwanzo mwa Januari 2022.
Mfumo ukikamilika kufungwa mageti yatashushwa, na tutaanza kuhifadhi maji.

Ni mfumo ambao ndani una crane na miundombinu wezeshi ya kutumia na kuendesha crane hizo. Crane hizo zinaitwa wire rope hoist crane zimaendeshwa kwa umeme sio hydraulic
Leo ni tarehe ngapi? Na unaposema mfumo unamaanisha nini, na boss wenu Makamba aliposema winchi la tani 26 alimaanisha nini? Na mnaukodi huo mfumo kwa muda gani? Na kwa kila siku wanatuchaji kiasi gani?
 
MILANGO YA BWAWA LA UMEME, TANI 26, KUKODI WICHI TOKA NJE, NIKUTUPIGA WATZ NA KITU KIZITO

Watu wengi wameonekana kushangazwa na maelezo ya Waziri wa sekta husika baada ya kujibu hoja mbungeni kuhusu maendeleo ya mradi wa bwawa la umeme Lililopo kati ya Rufiki na Morogoro.

Ambapo Waziri alisema, Hatua ya kwanza ya kujenga ukuta imeishafanyika isipokuwa hatua ya pili ambayo nikuweka MILANGO YA CHUMBA YENYE TANI 26 ndiyo bado haijakamilika kwa sababu INASUBIRIWA CRANE (WICHI) YA KUKODI TOKA NJE YA NCHI KWA AJILI YA KUJA KUSETI HIYO MILANGO.

WAZIRI kama umeambiwa basi maelezo uliyoambiwa na unayotakiwa kuyatoa kwa umma wa Watanzania yalitaliwa kuwa na ufafanuzi mzuri na wenye kueleweka.

Haiwezekani Crane zilizoko ndani ya mradi wa umeme zishindwe kubeba mzigo wa tani 26. Wakati Crane ZILIZOKO KWENYE MRADI ZIKO ZENYE KUBEBA TANI 25, 50, 60, 90, 120 NA HATA 200

Waziri CRANE ILIYOPO KWENYE MRADI WA UMEME AINA YA XCMG (Total Mass: 36000 Kg Ukichomoa Boom Angle ya Lenght 10.3 na boom ikawa kwenye mlalo wa Mita 4 INAWEZA KUBEBA TANI 43.5, 53 na TANI 55 ILA ITAWAKA ALAMA YA NJANO KUONESHA NI HATARI

Crane XCMG 36000 Kg ikiwa na Counter weight 7.6 boom ikawa Mlalo wa 20.6 na radius ya Mita 3, Crane hii INAWEZA KUBEBA MZIGI TANI 26.0 HADI 27.6.

Hii CRANE ya kusubiriwa kutoka nje ya nchi ina uwezo gani wa ziada kuzidi crane zilizoko ndani ya mradi au ina maajabu yapi kuliko crane zilizopo.

Hii CRANE inayosubiriwa toka nje ni ya nani na inakodiwa dola ngapi kwa saa na itatumia siku ngapi?

Hii CRANE toka nje, itakuwa inaweza kubeba tani 26 na inaizidi vipi CRANE XCMG 56000 KG yenye kuweza kubeba tani 90.

Hii CRANE YA KUKODIWA ina maana inaizidi LIBBER CRANE ambayo inaweza kubeba TANI KATI YA 50, 90 na 120.

CRANE HII TOKA NJE INAIZIDI CRANE AMBAYO IKO KWENYE MRADI NA INAWEZA KUBEBA TANI 200 mbona kama nikuwapiga Watanzania na kitu kizito.

CRANE Toka nje inazizidi uwezo Crane Tower zote zilizoko kwa Mchina, Mwarabu, AFFCO na zinginezo, Hapana Mh, Waziri maelezo hayawaridhisha Watanzania.

Watanzania wa sasa wameishaelimika na wanahitaji ufafanuzi yakinifu ili kuwaridhisha.

#Usisahau like na share page yetu

#lakini pia Inawezekana pamoja na kuwa ni mdua wa page hii ungependa pia kunisapoti kupitia kampuni yangu kwa kuagiza Mchele toka Mbeya. Kama ni hivyo jiunge kwenye gruop la WhatsApp kwa kubofya link hii na utaagiza popote

Nimeikuta mahali:
Ujinga wako na wanaokuunga mkono unasikitisha.
 
Tuachane na hayo, crane hilo la tani 26 tunalokodi toka nje ya nchi, lipo wapi?
Ndio maana nasema ujinga wa kutoelewa kinachoongelewa hapa, watu wanatiana michecheto bure.

Mimi nimefika hapo na hakuna crane inayohitajika.

Ni kama mtu kuanzisha uzi amemuona sheikh akila kitimoto, akiambiwa amuonyeshe huyo sheikh ndiyo anagundua kuwa hana kitu.

Sasa nami niwaulize wanao shabikia crane watueleze , ni la wapi na la kufanya kazi gani na linawekwa wapi haswa.
Tuanzie hapo.
 
Ndio maana nasema ujinga wa kutoelewa kinachoongelewa hapa, watu wanatiana michecheto bure.

Mimi nimefika hapo na hakuna crane inyohitajika.
Ni kama mtu kuanzisha uzi amemuona sheikh akila kitimoto, akiambiwa amuonyeshe huyo sheikh ndiyo anagundua kuwa hana kitu.

Sasa nami niwaulize wanao shabikia crane watueleze , ni la wapi na la kufanya kazi gani na linawekwa wapi haswa.
Tuanzie hapo.
Maji yameshaanzwa kujazwa? Kama ni hapana, kwanini?
 
MILANGO YA BWAWA LA UMEME, TANI 26, KUKODI WICHI TOKA NJE, NIKUTUPIGA WATZ NA KITU KIZITO

Watu wengi wameonekana kushangazwa na maelezo ya Waziri wa sekta husika baada ya kujibu hoja mbungeni kuhusu maendeleo ya mradi wa bwawa la umeme Lililopo kati ya Rufiki na Morogoro.

Ambapo Waziri alisema, Hatua ya kwanza ya kujenga ukuta imeishafanyika isipokuwa hatua ya pili ambayo nikuweka MILANGO YA CHUMBA YENYE TANI 26 ndiyo bado haijakamilika kwa sababu INASUBIRIWA CRANE (WICHI) YA KUKODI TOKA NJE YA NCHI KWA AJILI YA KUJA KUSETI HIYO MILANGO.

WAZIRI kama umeambiwa basi maelezo uliyoambiwa na unayotakiwa kuyatoa kwa umma wa Watanzania yalitaliwa kuwa na ufafanuzi mzuri na wenye kueleweka.

Haiwezekani Crane zilizoko ndani ya mradi wa umeme zishindwe kubeba mzigo wa tani 26. Wakati Crane ZILIZOKO KWENYE MRADI ZIKO ZENYE KUBEBA TANI 25, 50, 60, 90, 120 NA HATA 200

Waziri CRANE ILIYOPO KWENYE MRADI WA UMEME AINA YA XCMG (Total Mass: 36000 Kg Ukichomoa Boom Angle ya Lenght 10.3 na boom ikawa kwenye mlalo wa Mita 4 INAWEZA KUBEBA TANI 43.5, 53 na TANI 55 ILA ITAWAKA ALAMA YA NJANO KUONESHA NI HATARI

Crane XCMG 36000 Kg ikiwa na Counter weight 7.6 boom ikawa Mlalo wa 20.6 na radius ya Mita 3, Crane hii INAWEZA KUBEBA MZIGI TANI 26.0 HADI 27.6.

Hii CRANE ya kusubiriwa kutoka nje ya nchi ina uwezo gani wa ziada kuzidi crane zilizoko ndani ya mradi au ina maajabu yapi kuliko crane zilizopo.

Hii CRANE inayosubiriwa toka nje ni ya nani na inakodiwa dola ngapi kwa saa na itatumia siku ngapi?

Hii CRANE toka nje, itakuwa inaweza kubeba tani 26 na inaizidi vipi CRANE XCMG 56000 KG yenye kuweza kubeba tani 90.

Hii CRANE YA KUKODIWA ina maana inaizidi LIBBER CRANE ambayo inaweza kubeba TANI KATI YA 50, 90 na 120.

CRANE HII TOKA NJE INAIZIDI CRANE AMBAYO IKO KWENYE MRADI NA INAWEZA KUBEBA TANI 200 mbona kama nikuwapiga Watanzania na kitu kizito.

CRANE Toka nje inazizidi uwezo Crane Tower zote zilizoko kwa Mchina, Mwarabu, AFFCO na zinginezo, Hapana Mh, Waziri maelezo hayawaridhisha Watanzania.

Watanzania wa sasa wameishaelimika na wanahitaji ufafanuzi yakinifu ili kuwaridhisha.

#Usisahau like na share page yetu

#lakini pia Inawezekana pamoja na kuwa ni mdua wa page hii ungependa pia kunisapoti kupitia kampuni yangu kwa kuagiza Mchele toka Mbeya. Kama ni hivyo jiunge kwenye gruop la WhatsApp kwa kubofya link hii na utaagiza popote

Nimeikuta mahali:
Mtajuana wenyewe.
 
Tuwaache wataalam wafanye kazi yao...sio kila winch lenye kapacity ya ton 30 linaweza fanya kazi kayika mazingira yote. Ndo maana winches zipo za muundo tofauti tofauti kulingana na nature ya matumizi.

Ilo libber crane unayozingumzia, kwanini haitumiki ku off load containers toka kwenye meli! Ni kwa vile haliko designed for that purpose. Same pia bwawa lililo na structure iliyo very complex kwa crane ya kawaida kufanya kazi.

Tuachie wataalamu wafanye kazi yao.
Hebu tujaribu tu kukubaliana na wewe, lakini swali la msingi ni kwamba mkandarasi alikuwa hafahamu muda woote tangu ameanza mradi kuwa atahitaji hiyo crane? Kwanini mradi usimame eti kungojea crane iwasili? Na Bunge zima limesimama wima kusikiliza huo upuuzi?
 
Ni sawa na kuulizia kachumbari ya pilau kama iko tayari wakati mchele wenyewe bado haujanunuliwa.
Unafahamu kwamba maji yanachukua mwaka au miaka kujaza? Kiasi by the time bwawa linakuwa limekamilika kwa 100%, linaweza kukaa mwaka mzima au zaidi likisubiri maji yajae? Kiasi ni muhimu ujazaji uanze angalau mwaka kabla ya kukamilika ujenzi. Nakuuliza tena, maji yameshaanza kujazwa? Na kama bado kwanini?
 
Turudi kwenye mantiki ya mada yenyewe.

Mtoa mada anataja crane ambayo sijui ni nani kamwambia inahitajika kule, na kwa sehemu gani.

Pili, bwawa halijaanza kujazwa kwa sababu za kitaalaam, kwamba dam lenyewe halijakamilika sasa unajaza maji kwa vipi na ili iweje.
Jengo lemyewe la kuweka turbines 9 za kufua umeme halijakamilika.
Kwa mlinganisho tu, turbine moja kati ya tisa inafua umeme wa 235MW, wakati Kidatu nzima ni 200MW!

Tatu, pale wanaofanya kazi za
kitaalaam si watoto wa sekondari, ni wahandisi waliobobea wa kiTanzania,Misri na hata China wenye uzoefu.

Mkuu mshauri mtoa mada asianzishe mada asizo na utaalam nazo.
 
Sasa hapa mbona unaanza kujifanya taahira wakati mimi najua for a fact wewe sio taahira?

1.)Unasema hujui nani kasema crane inahitajika, Kalemani na Makamba umeshawahi kuwasikia wakizungumza juu ya hilo bwawa na wakataja kuhusu kujaza maji, na Makamba akasema nini kuhusu kushindwa kujaza maji?

2.) Hapo kusema ujenzi bado mbona nimekujibu kwenye hiyo post uliyo-quote, kwamba bwawa linahitaji mwaka au zaidi ili kujazwa vya kutosha kabla kuweza kuzalisha umeme, hivyo hata ujenzi ukikamilika kwa 100%, tunaweza kujikuta tunakaa bila kuzalisha umeme kwa hata mwaka au zaidi kisa tu hakuna maji bado, ndio maana ujazaji wa bwawa unapaswa kuanza angalau mwaka kabla ya kukamilika ujenzi, ili ujenzi ukikamilika na maji ya kuzalisha umeme yawe yameshajazwa tayari.

Sasa mimi sielewi unajifanya taahira kwa faida ya nani zaidi ya kujidhalilisha tu.

Tuachane na hayo, crane la tani 26 tukikoambiwa na Makamba kwamba wanakodi nje ya nchi, liko wapi?
 
Back
Top Bottom