SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,888
Mh Rais anasema "waache kuwekeza kwenye majengo na badala yake wawekeze kwenye viwanda". Anasema pia angetamani mifukoi ya kijamii ianze kuagiza sukari! Haya ameyasema akiwa Arusha lakini hilo la viwanda alilisema pia Dar alipokuwa akifungua Daraja la Nyerere. Lakini ni vema tukahoji mapema haya maagizo ya Mh Rais.
Mifuko hii inakusanya pesa wafanyakazi na wananchi wengine ili ziwasaidie uzeeni kwa hivyo kwa kweli tungependa kuwa na uhakika wa usalama wa hizo pesa katika miradi/uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo. Kulilipotiwa matatizo kadhaa juu ya uwekezaji wa mmojawapo ya mifuko hii katika ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Haya "maagizo" ya Mh Rais juu ya aina ya uwekezaji ambao mifuko ya kijamii inapaswa kufanya yana hatari gani kwa mustakabali wa hii mifuko (risk and returns) na wanachama wao? Maagizo yanaweza kuwa na nia njema lakini tunajua hatari zake? Hili sakata la sukari pia lilianza kwa maagizo.
- hivi hii mifuko ya kijamii haina miongozo/kanuni juu ya uwekezaji?
- Najua baadhi ya hii mifuko tayari ina hisa kwenye baadhi ya makampuni ambayo yame list share zao DSE. Je aina hii ya uwekezaji ni tofauti na uwekezaji ambao Mh Rais anaukusudia? Au angetaka kuona mifuko hii inajenga viwanda moja kwa moja? Na je aina hiyo ya uwekezaji inakidhi matakwa ya kikanuni/sheria?
Tuelimishane