Siasa kwa wenye uelewa

Carl Marx

Member
Oct 2, 2011
20
3
Twataka maendeleo yanayosababishwa. Utasikia mtu asema wakati wa uhuru 1961 tulikuwa na chuo kimoja sasa tuna 50! Hata nchi iliyokuwa chini ya ukoloni iliweza kuwa na vyuo 50 kwa miaka 20 kama Zimbabwe (1961-1980). Mtu aonyeshe kama tungalikuwa si huru, hali ingekuwaje na sasa tu huru maendeleo yaliyosababishwa ni yepi! We do not like chama just sitting on their behinds waiting for a natural course of action, eating and squandering then waibuka kusema wao wamesababisha maendeleo. Hata maji ya mto hufuata a natural force of gravity. Je tuseme sisi ndo tumechimba mito?

Avoid agreeing to everything hata kama umeambiwa na babayo. Tujifunze kujiuliza. We all know that "When contradiction ends, development ceases!"Ukiona nchini "ndiyo baba" nyingi, anza kuogopa.
 
Thread yako hii ni zaidi ya hata ulivyoielezea, kama ni mfatiliaji ama msomaji mzuri wa sayansi ya siasa/political science hasa siasa zile za kale utakumbana na kitu kinaitwa RATIONAL VOTERS, hapa wataalam wanataka Uwakilishi hasa katika chaguzi na mambo yahusiyo maamuzi magumu yafanywe na watu wenye akili timamu. Ndio maana ukifatilia political situation of Athens (Athenian democracy) ambapo wanasema ndio hasa kulikuwa na Direct democracy utakuja gundua kuwa indirectly kulikuwa na representative democracy. Enzi zile watu design ya watumwa, wanawake na watoto hawakuruhusiwa kushiriki ktk maamuzi ama politik kama wenyewe walivyo ita. Nadhani kuna haja ya kuwa na Siasa kwa wenye uelewa. Mfano mzuri swala la Igunga, wananchi wa vijijini wanatuangusha. Uelewa wao juu ya mambo na mahitaji ya dunia ya sasa kwao ni mdogo! Hiyo ndio tafsiri yangu juu ya Siasa za Uelewa!
 
Nafikiri elimu ya haki itolewe sehemu za mashambani. Watu wameshindwa kutofautisha haki na upendeleo. Hajui mkataba wake na serikali ni upi! Unamkuta mtu hana nyumba, hana barabara, hana soko/gulio, kiwanja hakijapimwa, hana maji, hana umeme, hana simu au aina yoyote ya mawasiliano, hajasoma kwa ukosefu wa shule, etc. Maisha yamebana hajui akaombe wapi msaada. Huyu ataipigia kura CCM. Anadanganywa imeleta amani na hajui amani ni kitu gani. Hajui amani inaletwa na wananchi wenyewe, if at all!

On the other side, mtu amesomeshwa bure, ni PHD holder, anaishi sehemu yenye umeme, maji, barabara, viwanja vimepimwa, mawasiliano anayo, etc lakini atakuambia bado kuna mapungufu mengi na haipi kura CCM.

THIS IS A POLITICAL PARADOX!
 
Tuwe na mtihani wa kupima uelewa wa siasa darasa la saba na tuweke alama za ufaulu A,B,C na F.
Atakayepata A aruhusiwe kuchagua rais,mbunge na diwani.
Atakayepata B aruhusiwe kuchagua mbunge na diwani tu.
Atakayepata C aruhusiwe kuchagua diwani peke yake.
Atakayepata F asiruhusiwe kushiriki uchaguzi.
Haiwezekani mtu haelewi viongozi anaowachagua wanaenda kufanya nini,haelewi kwanini kuna uchaguzi,haelewi lolote kuhusu siasa ETI bado anaruhusiwa kushiriki jambo asilolijua ETI ndio demokrasia inavyotaka.
Mtu wa namna hiyo anaweza kufikiri uchaguzi ni kupewa vyakula vya msaada,anaweza kudanganywa chama kikiongozwa na mchagga ni cha wachagga anaweza kuaminishwa kufuata maoni ya viongozi wa dini kwenye chaguzi na sio sera za vyama.
Chama kinachotegemea mtaji wa wajinga hakiwezi kuniunga mkono.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom