Siasa: Kumbuka hii ndio CHADEMA

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Unakumbushwa tu ukipenda kuwa CHADEMA jitahidi uijue KATIBA, falsafa ya chama sambamba na itikadi yake ili uweze kujipima na kufanya maamuzi rafiki.

1. CHADEMA kila mwanachama ana haki na wajibu sawa linapokuja swala la kulinda maslai ya chama popote pale iwe ndani au nje ya eneo la uvunjwaji huo wa maslai ya chama unapotokea.

2. CHADEMA inatoa fursa sawa kwa kila mwanachama ambaye anahisi au mwenye uwezo wa kukisaidia chama kukipeleka ngazi ya juu kimaendeleo iwe ndani ama nje kiuongozi na kichama.

3. CHADEMA mwanachama mpya ana haki sawa na mwanachama mkongwe. Ndio, yaani ukikidhi vigezo wewe unafaa kuwa miongoni mwa wanachama na unaruhusiwa kufanya chochote chenye baraka ya CHAMA.

4. CHADEMA ni chama kinachotoa mafunzo kwa wanachama wake kupitia njia mbalimbali za kizamani na kisasa kwa mfumo wa hali ya juu sana.

ANGALIZO

Ukiwa CHADEMA ukumbuke tu unaweza kupoteza maisha, mali, kazi, kudharirishwa, kupata ulemavu, kupakaziwa mambo yasiofaa nk. Unakumbushwa tu uyaonapo hayo yanatokea au kukutokea jua kabisa wewe sio wa kwanza, wapo waliowengi sana wamefikwa na changamoto mbalimbali katika CHAMA.

CHADEMA hakuna fedha. Hapa kuanzia CHADEMA MSINGI ( Uongozi wa kibarozi mtaani/ kijijini ) mpaka ngazi ya juu katika kukijenga CHAMA huwa kunafanyika harambee kukuza mfuko ili kazi za CHAMA ziende kwa usahihi.

Kuchangia CHAMA ni jambo la hiari kwa mwananchi, wanachama na kwa viongozi kuna utaratibu wa kuchangia kwa kiwango kilichopangwa.

"Freedom is coming tomorrow"
 
Matumizi mwachie Mbowe Mugabe!
Umesoma kitu kinachoitwa bajeti?

Bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi. Katika mapato unapaswa uainishe vyanzo vya mapato yako mfano ruzuku ya chama, makato kwa viongozi na michango ya wananchi au wahisani. Upande wa matumizi ndio napo unaandaa taarifa zako utafanya nini na nini kwa kuzingatia mtiririko wa mapato utakavyokuwa ndani ya chama kwa kuzingatia Uhasibu.

Mwisho, bajeti huwa inapitishwa na jopo la watu husika kichama na huwa mapato na matumizi yanakaguliwa kwa kuzingatia sheria za nchi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom