Siasa katika nishati yetu ni hatari kuliko UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa katika nishati yetu ni hatari kuliko UKIMWI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Jan 3, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Leo ndiyo siku ambayo watanzania tunaanza kuonja joto la jiwe la bei mpya ya Tanesco. Mambo makubwa ya kujiuliza ni juu ya utashi wa serikali yetu kulinda na kutunza mazingira yetu, wakati waziri wa fedha akisoma bajeti yake ya mwaka 2009 kati ya mambo ambayo aliyataja kama kipaumbele cha serikali ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaacha kutumia nishati ya kuni na mkaa, leo miezi 18 baadaye bei zote za nishati mbadala zimepanda kwa wastani wa asilimia 30%. Mojawapo wa vitu vinavyochangia kupanda kwa vitu hivi ni pamoja na wanasiasa wanaoshiriki katika maamuzi kuwa ndio wanufaika wakubwa wa biashara ya nishati.
  Nilinunua mtungi wa gesi ya kupikia wa kilo 15 kwa shiling elfu 30 tarehe 30 Nov 2009, leo hii mtungi huo huo unauzwa kati ya elfu 40 na 45, mpaka leo (takribani miaka 15 tangu tupate gesi) bado tunanunua gesi ya kupikia kutoka nje ya nchi. Tukiwa tumejaliwa utajiri huu wa gesi ya asili katika taifa letu tungetegemea kuwa serikali ingewekeza katika kuhakikisha kuwa angalau asilimia 75 ya Watanzania wanapikia gesi na kwamba serikali inahakikisha kuwa bei ya nishati yoyote ile haipandi bei na badala yake ipungue (ukizingatia kuwa Tanzania ndiyo nchi yenye bei ya umeme kubwa kuliko zote kwenye kanda hii ya Afrika) lakini badala yake inapandishwa.
  Umefika wakati tuwakatae wanasiasa ambao wanajali masilahi yao ya leo na kutelekeza mahitaji yetu na vizazi vijavyo, imefika wakati tuwawajibishe wale wote walioliingiza taifa hili kwenye mikataba tata ya aina ya Richmond/Dowans, IPTL, Aggreko, n.k hawa wanathamini matumbo yao kwa gharama kubwa ya vizazi vijavyo kwani badala ya watu kutumia nishati mbadala inabidi waendelee kutumia kuni na mkaa huku wakiacha majangwa ambayo yana gharama kubwa kwa jamii zetu
   
 2. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2015
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  Uliyoyasema yamejirudia katika bajeti hii mwaka 2015/16
   
Loading...