MC Chere
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 586
- 400
Ni kitambo sana nimekuwa nikizama kwenye tafakuri nzito inayoumiza moyo wangu juu ya elimu yetu kuendeshwa kisiasa.
Ni kuwa elimu hii kwa ukubwa wake watu wengi haiwakomboi kutokana na nadharia zake.
Hoja yangu ni kuwa shule za msingi kuna somo moja linaitwa STADI ZA KAZI.
Sote tunajua namna somo hili lilivyobeba uhalisia wa kumkomboa mtu pindi aipatapo elimu yake.
Fikiri kuna masuala ya kujifunza STADI ZA:-
-KILIMO na UFUGAJI
-MUZIKI
-USEREMALA
-USHONAJI VIATU & NGUO
-UCHORAJI
-USUSI
-UPISHI
n.k
Hizo zote mtu akifundishwa kwa vitendo ni rahisi mno kujiajiri na hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini.
Shida iliyopo,hakuna vifaa wezeshi na walimu karibia wote hawana uelewa na somo hilo hivyo linaendelea kuwa la kinadharia tu.
NINI KIFANYIKE BASI?
Somo hili liwe hai shule za msingi,lianzishwe sekondari na vyuo na liwe la lazima kwa wote.