Siasa inavyochangia Uchafu ndani ya Jiji la Dar es Salaam

namraroh

Senior Member
Sep 9, 2010
112
122
Habari za leo wanabodi, Ni matumaini yangu tupo salama na tunaendeleza mapambano dhidi ya Uviko 19, ni vyema tukachanje ndugu zanguni!!!

Niende moja kwa moja kwenye mada yangu, Swala la usafi katika jiji letu la dar isalaam linaendelea kuwa kitendawili kigumu kwa wakazi wa jiji hili na mamalaka za serikali zinazosiamamia mambo haya ya usatawi wa miji yetu! Sijajua tatizo liko wapi? kwani tangu kuhamishiwa kwa shughuli nyingi za kiserikali jijini Dodoma, mambo mengi ya Dar es Salaam yanaenda mrama, kwa mfano swala la mpangilio wa jiji, hususani ufanyaji biashara holela, usafiri wa umma (DART) na kadhalika!

Kwa kweli napata taabu sana kuelewa nn kinaendelea kuhusuiana na uboreshaji wa miundombinu ya jiji hili wakati huo huo uharibifu wa miundombinu hiyo ukifanyika kwa kasi ya kutisha! Kuanzia Kariakoo kwenye kituo kikuu cha Mwendokasi, Mbezi kwenye maboresho makubwa ya miundombinu (barabara na Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani) Sehemu hizi kwa kweli zimevamiwa kwa kiasi kikubwa sana na hata kuhatarisha maisha ya wananchi wanaotumia au wanaopata huduma katika sehemu hizo.

Mfano mzuri ni pale Kariakoo kwenye kituo cha Mwendokasi, eneo hili limekuwa eneo hatari sana kwa watembea kwa miguu kwani wafanyabiashara wa mwendazake wameziba njia zote za kuingia kituoni kiasi kwamba ni vigumu kwa mwenda kwa miguu kupita bila kusukumana na magari na bidhaa zilipopangwa chini, juu, na hata pembeni ya barabara. Bado hujafika Mbezi ambako njia zote za waenda kwa miguu zimezibwa kiasi kwamba hata mifereji ya maji machafu nayo imekuwa ni sehemu za kufanyia biashara!

Sasa najiuliza kweli tunaboresha miundombinu yetu kwa aina hii ya maisha? Tunahitaji watu wajiari wapate kipato, lakini tunahitaji sana ubora wa miundombinu kwa ajili ya kurahisisha na kuboresha maisha ya wananchi, tunapoziba mifereji, tunaziba njia za waenda kwa miguu, je siku za mbeleni hii miundombinu ikifa hizo biashara zitafikiwa? nawaza tuu
 
Uongozi wa uchumia tumbo ndo upo tanzania hakuna Cha Samia wote chumia Tumbo nikitembea nchi za watu huwa naona aibu mimi
 
Yote haya nikumlaumu Mwenda zake, Mama anawakati mgumu kuliondoa hili
Ni kweli ana wakati mgumu lakini kwa nn asisimamie maamuzi yake? Kwa nn mambo mengine amefanikiwa kubadilisha? Kwa nn hili linakuwa gumu kwake?
 
Back
Top Bottom