Siasa imetufikisha hapa- angalia ukweli huu ktk hudum za afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa imetufikisha hapa- angalia ukweli huu ktk hudum za afya

Discussion in 'JF Doctor' started by Mrekebishaji, Mar 8, 2011.

 1. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu watanzania,
  Leo naandika huku nikiangalia hali ya afya zetu, watoto wetu na ndugu zetu wengine ambavyo hazina uhakika wa usalama.

  Leo hii, mtoto akiugua kwa Dar, daktari mwenye uwezo mzuri wa kumtibu mtoto ni mmoja tu, Dr. Masawe ambaye yupo Morocco. Hata hivyo, huyu doctor kwa wanayemfahamu, kila siku kwa siku anazotibu huchukua watu kumi tu na lili umpate unahitaji ufike pale saa kumi usiku, mimi leo nimefika saa kumi na moja nimepata namba tano baada ya kumkosa kama mara nne hivi na nimekwenda kwa wengine bado sijapata huduma nzuri. Utasikia ma-doctor wa watoto ni wengi lakini, utaenda hapa na mtoto, utaambiwa hili, utakwenda pengine utaambiwa lingine. Huku watasema malaria, huku watasema si kweli, hizi dawa ulizopewa tupa.

  Tutafakari yafuatayo;
  1. Hivi wizara ya afya na ustawi wa jamii,hawawezi kufanya uchunguzi wa kubaini madaktari wasiofaa maana ni wagonjwa wengi wanapewa dawa zisizofaa.
  2. Kutokaka na siasa zetu, watu wengi wenye uwezo wamekimbia kusoma u-dokta kutokana na maslahi duni ya fani hiyo na pia mfumo mbaya wa kuwapata ma-doctor. Angalia jinsi wanafunzi wa chuo cha tiba muhimbili wanavyolalamika namna shule yao inavyoendeshwa.

  Siasa, inaua kila kitu.

  Kweli maisha yetu yapo hatarini.

  Yote haya yanatupelekea kuona kwamba kwa sasa ni kweli tunahitaji chama makini ambacho kitaiangalia nchi kwa jicho la tofauti. Chadema wanaonyesha nia hiyo.
   
 2. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Daktari ambae ndugu zangu na wenzao wanamtumia wakiwa dar likizo as wanaishi ulaya ni Dr. Amir kama sijakosea jina na wote wanasema ni mzuri na ni anakwambi bila kukupotezea muda

  Muhimu ni kuwahi namba asubuhi maana anapata wagonjwa wengi

  Yupo pale fire ukitoka traffic lights kuelekea kariakoo ni kushoto kwa corner either 2nd or 3rd left.

  Akiwepo dar yeye ndio anaangalia watoto na anajua haswa as sasa kila wakija toka ulaya ni hapo wanapeleka watoto wao kama wanahitaji kuwapeleka.

  Tanzania ni ya asili nyingi ya watu hivyo kote tuangalie na sio wabantu tu

  Nasikia kuna mwingine near muhimbili.
   
 3. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Madaktari wa watoto wapo wengi tu sema wewe unamjua massawe tu, umeenda tumaini, aga kahn au rijens? Ninavyojua mimi hawa madokta bingwa wa muhmbl wengi wanatibu huko. Pia hata mumbil kuna ippm ambayo unaweza kumuona specialist unaemtaka.
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu Mrekebishaji hayo uliyosema hapo juu ni matusi kwa chama cha madaktari wa watoto (Paediatric Association of Tanzania), na pia ni matusi kwa madaktari bingwa lukuki wa watoto waliopo Dar es salaam hii! Paeditrics ni moja ya specialization ambazo madaktari wengi sana wanakimbilia, na hivyo kufanya moja ya fani zenye madaktari bingwa wengi sana. Dr Massawe kuwa 'Legend' kwenye fani ya kutibu magonjwa ya watoto hakufanyi wengine kuwa 'si kitu'! Kuna madaktari bingwa wa watoto weengi tu hapa Dar es salaam wanaosifika sana (pengine zaidi ya Dr Massawe).

  Nakubaliana na wewe juu ya umuhimu wa MoHSW kuchunguza kuhusu ubora wa huduma watu wanazopata kwa hospitali za serikali na private pia, na nakupa hongera kwa kuguswa na hali duni ya kikazi na kimaisha ya madaktari wetu wanaohangaika kutwa-kuchwa kuokoa maisha ya watoto wetu, lakini tusiwakatishe tamaa wale ambao wako 'kiuzalendo' zaidi kiasi cha kusota kwenye hospitali za serikali na hivyo kutokuwa maarufu kwa watu wenye status za kupeleka watoto kwa 'Massawe' kuwa hao si madaktari wazuri wa watoto.
   
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Limekuwa tatizo.Ndg nakushauri we hukifika moroco hapo hospital muone Dr yeyote,Pale atakusaidia.Madakitari wengi wamekuwa kama waganga wa kienyeji.Siki moja nilifika hapo hospital kumuona Dr masawe nikafuata utaratibu wa kupata namba,Mtoto alipewa huduma na Dr masawe.hali ya mtoto aikubadilika baada ya siku tatu nikarudi pale,sikuweza kumwona Dr masawe hila kinaona na Dr mwingine akanipa dawa zingine tofauti na za mwanzo na mtoto akapona,Ni kamuuliza mke wangu nini sababu ya kuniamusha usiku kuwai namba ya kumwona Dr masawe wakati wapo wengine pale wanatibu.?Mkuuu tatizo ni watu kufata mkumbo wa kusikia tu Dr wa watoto ni masawe.Nakushauri kuwa na tabia ya kuonana na dr mmoja pale hospita ya moroco mtoto wako atakuwa na tatizo
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Tatizo la madaktari tanzania ni kubwa sana....Pengine inawezekana si la kitaalamu yaani hawajafundwa nadhani tatizo kubwa ni MFUMO mzima wa hii sector ya afya. Utakuta DMO ni administrative na yuko kisiasa zaidi kuliko kimatibabu. Sasa hiyo ni sehemu moja tu, na huyu mtu ni a very well trained guy na inawezekana ni specialist lakini hafanyi kazi zake kutokana na mfumo. Mara yuko kwenye vikao huko almashauri, sijui uzinduzi na makamu wa raisi, sijui ajibu hoja za wakaguzi wa mahesabu (kazi za DT) etc etc....miaka nenda rudi fani yake kesha isahau kabisa. Sasa utawakuta wapi....matokeo yake utakutana na wenzangu na mie humo hospitali wengine ni aibu kabisa kama juzi nimeenda hospitali nikamwambia huyo aliyekuwepo (sie twamwita dokta) ni mzushi kwani vitu alivyokuwa anasema havimake sence. So hali ndo hiyo...
   
 7. M

  Matarese JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  wamekata tamaa kama walimu tu, kwa hiyo wanasukuma tu bora liende!
   
 8. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yupo Dr. Hassanal MTENDENI CLINIC foleni ya watoto hapo nayo siyo mchezo ni Dr. mzuri sana
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Siyo siasa, ni sisi wenyewe ambao tunachagua hovyo!
   
 10. i

  iwensato Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujaelekeza vizuri kwani wengi tunashida na Dr. Amir, kuwa specific kwa mtaa au jengo ieleweke vema
   
 11. i

  iwensato Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  elekeza vizuri Dr. Amir alipo, wengi tunashida
   
 12. V

  Vancomycin Senior Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Kaka nimeisoma habari hii kwa masikitiko makubwa kwa sababu naona kama haujatutendea haki sisi madaktari wachache ambao tumejitoa kwa moyo mmoja kulitumikia taifa hili tukijua tukiondoka nchi hii dada zetu kaka zetu ndugu zetu watakosa hata wachache wakuwatibu mbali ya changamoto nyingi tunazokumbana nazo.Naomba kukanusha kuwa Daktari wa watoto ni mmoja na ndie mwenye uwezo wa kutibu watoto Dar na kukubaliana na wewe kuwa siasa zimetufikisha kwenye huduma zisizo na kiwango ila hii ni tofauti na mtazamo wako.Pia napenda uyafahamu yafuatayo machache ambayo nitayaandika huku nikilinda maadili ya udaktari

  1.Madaktari(MD-medical doctors) hapa Tanzania ni wachache sana kiasi ambacho uwiano wa daktari kwa wagonjwa ni mkubwa mno ambao haulingani na unaotakiwa na WHO hivyo hii inapelekea watu wanaotibu wengi kuwa ni waganga wasaidizi(CO-clinical officers au AMO-assistant medical officers) ambao kimsingi elimu yao ni ndogo kwa utabibu.Uchache huu unatokana na mishahara midogo na mazingira yasiyo rafiki ambayo yamepelekea madaktari wengi kuondoka na kwenda kufanya kazi nje ya nchi.Pia ni rahisi kukuta hospitari ya wilaya haina MD achana na specialist ambao wengi utawakuta refferal hospitals.Pia tukubali hawa waganga wasidizi wamekuwa msaada mkubwa.

  2.Kwa kawaida daktari anahitajika kukaa na mgonjwa kwa takribani dakika 45 au chini ya hapo kutegemeana na uzoefu hii ni kwa ajili ya kupata maelezo na vipimo(siyo maabara) ambapo hutakiwa kupima zaidi ya malalamiko ya mgonjwa kwani anaweza kuwa na tatizo tofauti na lililomleta ambalo hajalitambua.Lakini nikiri hali haiko hivyo kutokana na wingi wa wagonjwa ambao anastahili kuwaona ambayo hii imepelekea madaktari kuwa na wakati mgumu.

  3.Kutokana na maslahi madogo madaktari wengi hasa madaktari bingwa wamekuwa wakifanya kazi kwa mda wa ziada katika hospitali binafsi kujiongezea kipatoau kufungua hospitali zao binafsi ambapo hutoa huduma kama biashara ambayo hutolewa kwa ufanisi ili kuvutia wateja na wengine hutumia fursa ya kujulikana kutokana na kuwa wa mda mrefu hivyo kujenga imani kwamba wako peke yao.Kaka amini watu wanagombania wagonjwa hata kuchafuana.

  Naomba niishie hapa ingawa na mengi ya kuandika ila pia na majukumu mengine
   
Loading...