Siasa imenifikisha hapa: Je Mwanza Airport ni International au Sio?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Napenda wajuzi wa mambo wanifahamishe kama uwanja wa ndege wa Mwanza ni International au la? Swali hili linatokana na ukweli kwamba sometimes ninaona ndege kutoka nje ya nchi zinatua hapo, hivi karibuni pia Rwandair itaanza kutua mwanza.

Kwa upande wa pili, ninafika uwanjani hapo siamini ninachokiona, hata stendi ya mabasi ya zamani ya kampuni binafsi inakuwa nzuri kuliko uwanja wa ndege wa Mwanza, waiting room paa linavuja, chumba ni kama cha kusubiri kwenda kumuona daktari kituo cha afya au zahanati. Nashindwa kujua wala kuamini ninahisi kuna international flights hapo.

Je uwanja wa ndege wa Mwanza umeshindwa kutengenezwa kuwa international ya ukweli? Je hukuna fedha kwa kazi hiyo, tutasafiri hadi lini kwenye kijiuwanja cha namna hiyo? Uwanja utadhani sokoni kwenye vijigenge vidogo vidogo kibao??

Nani ameshindwa kuwa na maono ya mbali??? serikali kuu, ya Mkoa au ya Wilaya? Jiji au Wananchi wa Mwanza???
Nawasilisha.
 
Mkuu, changamoto hiyo serikali sikivu ya chama cha mapinduzi inaifahamu sana na iko ktk mchakato na upembuzi yakinifu kwa kushirikiana na wafadhili wetu ili tuweze kurudi kwenye drawing board na kurekebisha changamoto hii.
 
ule uwanja mvua kubwa ikidondoka na ya maana ,ndege haziruki wala kutua.....kwa maana maji yanajaa asikwambie mtu....mweshimiwa wa LIWALO NA LIWE(alipoenda mwanza kwenye sherehe za hospitali ya bugando).....ilishawai kumkuta hii akahairisha safari mpaka maji yalipopungua na uwanja kuwa salama kwa kuruka na kutua ndege......

ila wahusika wa pale wanasema ni international airport kwa sababu wanafanya kazi 24/7 iwe kuna ndege inatua usiku ama hakuna.
 
liko tatizo kubwa, kuna viti 100 tu lakini abiria kibao husmama kwa kukosa viti.
upuuuuz tu.
 
Mkuu pale tunapopokea mizigo mbona aibu...yaani miaka nenda miaka rudi ni story tu. Huku Mbeya sasa miaka karibu kumi airport haikamiliki. Tunajenga nyumba za magholofa tu kuepuka kulala kwenye nyumba za tembele...nchi hii nayooooo!
 
serikali dhaifu haioni aibu kukurupuka na kubadili sifa ya majina ya mahali kwa sababu ya kisiasa. lakini ukweli unabaki palepale uwanja wa ndege wa mwanza kuitwa international ni aibu maana sioni nini hasa wana kiita hivyo, jana tumesikia hosp ya lugalo kupandishwa kuwa ya rufaa kwa majengo yapi na ofisi zipi na wodi zipi za kutosha kupokea wagonjwa wa rufaa? Hata miji yetu inayoitwa majiji ni aibu tupu haifanani kabisa lakini kwa kuwa serikali yetu inapenda kujipa matumizi yasiyo ya lazima ndo maana kila kukicha utasikia wamefanya hiki na kile kuboresha huduma kwa jamii lakini kiuhalisia hakuna cha maana .Kesho utasikia zahanati ya chanika imepandishwa kuwa na hadhi ya wilaya, kesho mji wa bgmoyo kuwa jiji la viwanda, n.k
 
Ni kweli uwanja wa ndege Mwanza ni aibu zile ofisi za pale zinasikitisha jengo limechoka sana mvua ikinyesha wote mnanyeshewa na mvua.
 
huo upembuzi yakinifu huwa haukamiliki2? huu ni mzaha mwingine wa serikali ya ccm, mwanza inachangia kiasi gani katika pato la taifa? kwa umuhimu wa kanda ya ziwa ni muhimu kuwa na uwanja wa kimataifa,serikali ione aibu basi.
 
Ni kweli uwanja wa ndege Mwanza ni aibu zile ofisi za pale zinasikitisha jengo limechoka sana mvua ikinyesha wote mnanyeshewa na mvua.
kama hata wewe umeliona hilo na kulisemea basi hali ni mbaya. Maana ungeweza kuja na hoja ya ajabu hapa mpaka tungesikia kizunguzungu.
Ila nadhani mwishoni utasema Halmashauri ya jiji sii inaongozwa na Chadema? Ritz una mahaba ya kweli na CCM (kama wale wasemao chongo ni kengeza)
 
Mkuu pale tunapopokea mizigo mbona aibu...yaani miaka nenda miaka rudi ni story tu. Huku Mbeya sasa miaka karibu kumi airport haikamiliki. Tunajenga nyumba za magholofa tu kuepuka kulala kwenye nyumba za tembele...nchi hii nayooooo!
Nilifika Mwanza kwa ndege kwa mara ya kwanza kutokea Dar. Niliposhuka nilitoka moja kwa moja mpaka nje! Ilibidi niliyekuwa nimesafiri naye aniite na kuniambia mbona huchukui mizigo? Mwenzenu mimi ndiyo nilikuwa naelekea hivyo kuchukua mizigo...mpaka nikatoka nje!
 
hauna return nzuri on investment kama wa mbeya, na arusha ndio maana upo hivyo.
 
Mkuu pale tunapopokea mizigo mbona aibu...yaani miaka nenda miaka rudi ni story tu. Huku Mbeya sasa miaka karibu kumi airport haikamiliki. Tunajenga nyumba za magholofa tu kuepuka kulala kwenye nyumba za tembele...nchi hii nayooooo!

Kweli hapo ni aibu kubwa sana,ukizingatia migodi mingi iko huko!!!Mabegi yanarushwa kwenye ile sehemu kama ya kulishia ng'ombe msosi!!!
Tumechoka na hizi Master Plan zao za kila siku!!!
 
endapo hicho kiwanja kina ofisi hizi

1.ofisi za forodha
2.ofisi za afya/chanjo
3.ofisi za uhamiaji

ni lazima utakuwa ni uwanja wenye hadhi ya kimataifa/international
 
nafikiri 2015 haya malalamiko tukiyapeleka kwenye masanduku hata waibe vp..haziishi
 
Jamani, naona tunaongea bila kujua hasa ninini kinachoendelea. Uwanja wa Mwanza ni Uwanja wa Kimataifa, ndiyo maana hata zile ndege Antonov za Warusi ziliweza kushuka pale na kubeba MAPANKI hadi ulaya bila kupitia Dar kwaaajili ya ishu za clearance.
Kiwanja cha Mwanza kipo kwenye hatua za mwisho za kupata Jengo zuri sana la Terminal ambalo litakidhi projection ya abiria wa Mwanza.
Kwa kawaida viwanja vyote vya ndege viko chini ya Mamlaka iitwayo TAA inayovisimamia.
Tulieni wakuu mtakula mema ya nchi hii.
 
Kweli muhimu kutulia tule mema ya nchi yetu,lol!
 
Back
Top Bottom