Siasa imekuwa uadui, siku kama leo Alphonce Mawazo aliuawa

strategist22

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
495
500
Siasa Tanzania imekuwa zaidi ya uadui ni vita vya maangamizi kabisa. Mwaka 2015/11/14 Kamanda Alphonce Mawazo aliuawa kikatili hatua chache kutoka kituo cha polisi katoro saa nne asubuhi. Alikatwa mapanga na watu makatili sana. Wanaofikiri siasa ni uadui na wapinzani malipo yao ni kifo , kupotezwa kutekwa kubambikiwa kesi kubwa kubwa na ukatili wa aina hiyo.

Kifo cha mawazo kilifungua ukurasa mpya wa siasa za Tanzania na sasa hali ni mbaya zaidi. Usithubutu kuwa mpinzani, utaenda na maji.

Wajue ya kuwa upinzani sio mtu upinzani ni fikra na huletwa na wakati

Rest in peace Kamanda Mawazo

Mwenyekiti wa CHADEMA Geita

Mbunge wa Busanda

Fikra zako bado zinaishi.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,752
2,000
Mkuu usidanganyike popote,siasa lazima iwe na uadui kwa sababu kuna maslahi makubwa yanapatikana.

Mtu anachukua 12M kila mwezi akitoka miaka mi5 ana zaidi ya 200M halafu pasiwe na uadui ?

Mbona ukuu wa mkoa hailuna uadui,ukuu wa wilaya hauna uadui.

Sjida ni hivi vyeo vya kugombania ndio shida yenyewe,haitokuja kuwa siasa isiwe uadui,trump huko anahaha haamini kilichotokea ije kuwa huku kwetu bwana ?
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Mkuu usidanganyike popote,siasa lazima iwe na uadui kwa sababu kuna maslahi makubwa yanapatikana.

Mtu anachukua 12M kila mwezi akitoka miaka mi5 ana zaidi ya 200M alafu pasiwe na uadui ?

Mbona ukuu wa mkoa hailuna uadui,ukuu wa wilaya hauna uadui.

Sjida ni hivi vyeo vya kugombania ndio shida yenyewe,haitokuja kuwa siasa isiwe uadui,trump huko anahaha haamini kilichotokea ije kuwa huku kwetu bwana ?

Kwa hiyo una halalisha Watu wauane kisa ni Madaraka sio !?

Kama Siasa ni Uadui una shauri tuwe na mfumo gani mbadala Mkuu!?
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,752
2,000
Kwa hiyo una halalisha Watu wauane kisa ni Madaraka sio !?
Nimesema uadui lazima uwepo,sijasema kuwa ni halali uwepo.

Kama ambavyo nikisema kuwa zinaa lazima iwepo kwa sababu ya technolojia na wanawake kujirahisisha na kuvaa uchi na wanaume kukosa maadili,hapa nagusia mazingira ambayo lazima jambo hilo lisiepukike na sio kwamba nahalalisha kama ambavyo wewe umenielewa mkuu.
Kama Siasa ni Uadui una shauri tuwe na mfumo gani mbadala Mkuu!?
Mfumo mbadala ni kuwe na utaratibu kama wa wakuu wa mikoa.

Wabunge wasiwepo kabisa.

Kusiwe na nafasi yeyote ya kugombea kwa wananchi na mtu kujisifia pale kwamba anaweza jambo fulani na fulani huko ni kuruhusu uongo hadharani.
 
Mwami Ntale

JF-Expert Member
May 26, 2018
221
500
Moja wapo ya matukio yaliyonipa mwanga juu ya utawala wa jiwe in hili tukio.Wakati mauaji yalipofanyika alikuwa na Siku chache tu tangu aapishwe na hakuwahi kusema chochote juu ya tukio lile ,kimyaaa kana kwamba hakuna kilichotokea.Kwa rais ambaye watu walikuwa na matumaini makubwa juu yake hili lilinishangaza mno.Baadaye matukio mengine kama kuzama kile kivuko na tetemeko la bukoba ndiyo yakanifanya nimuelewe vivuri!
 
Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Kweli hajasema chochote Pamoja na kuwa Mawazo ni ndugu yake wa karibu Busanda na Chato
 
Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,095
2,000
Nimesema uadui lazima uwepo,sijasema kuwa ni halali uwepo.

Kama ambavyo nikisema kuwa zinaa lazima iwepo kwa sababu ya technolojia na wanawake kujirahisisha na kuvaa uchi na wanaume kukosa maadili,hapa nagusia mazingira ambayo lazima jambo hilo lisiepukike na sio kwamba nahalalisha kama ambavyo wewe umenielewa mkuu.

Mfumo mbadala ni kuwe na utaratibu kama wa wakuu wa mikoa.

Wabunge wasiwepo kabisa.

Kusiwe na nafasi yeyote ya kugombea kwa wananchi na mtu kujisifia pale kwamba anaweza jambo fulani na fulani huko ni kuruhusu uongo hadharani.
Hata Rais asiwe anagombea maana pia kuna uadui mkubwa zaidi ya uliopo kwa wabunge maana hata maslahi ni makubwa zaidi!
Turudi kwenye utawala wa kifalme,Magu akitoka amrithishe mwanaye Nk!
 
kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
14,935
2,000
R.I.P ALPHONCE CHEMU MAWAZO
hqdefault.jpeg
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,752
2,000
Hata Rais asiwe anagombea maana pia kuna uadui mkubwa zaidi ya uliopo kwa wabunge maana hata maslahi ni makubwa zaidi!
Turudi kwenye utawala wa kifalme,Magu akitoka amrithishe mwanaye Nk!
Ndio hata raisi asigombee pia kama inavyofanywa hivi sasa.

Iwe ufalme tu.
 
Tindikali Kali

JF-Expert Member
Jan 9, 2018
529
500
Wanaofikiri siasa ni uadui
Siasa inaweza kuwa urafiki au uadui kutegemeana na aina ya upinzani! Kwa kujua Kikwete alivyowabeba hawa na akaambulia dharau na matusi, hata ningekuwa mimi joto ya jiwe wangeipata hakyanani.
Eti leo Kenya ndiyo wakutuambia kuhusu demokrasia, hovyo kabisa...
 
The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,055
2,000
Namkumbuka sana Alphonce Mawazo maana niliwahi kuhudhuria mkutano wake mmoja uliojikita katika ku-raise awareness ya watu kuhusiana na haki zao na jinsi Siasa za nchi zinavyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja kila siku.Mkutano huo ulifanyikia pale Igoma,Mwanza.

Kwa ufupi jamaa alikuwa inspirational, charismatic na revolutionary wa ukweli.

Sauti yake ilikuwa kama ya Zitto Kabwe,hawa jamaa walikuwa wana-share vitu vingi(ila kwenye suala la ujasiri sidhani kama ZZK alikuwa anamfikia AM). Yaani kama ungemsikia akihutubia kabla hujaiona sura yake, basi usingekuwa na shaka kuwa huyo anayehutubia ni Zitto Kabwe, kumbe wapi bwana!

Rest in Eternal Peace brother. Miungu-watu ambao wanadhani wao hawatakufa na kwamba hakuna siku watasimama mbele za Mungu kujitetea wenyewe, waliyaondoa maisha yako. They think they live in heaven but they live in hell (according to Bob Marley's Redemption Song). Mungu wetu,YEHOVA anazo details zote za namna ulivyodhulumiwa na SIKU INAKUJA ATAKAPOMLIPA KILA MMOJA WA WATESI WAKO.

Nimekukumbuka sana, Natamani nikuone, Ipo siku Mungu atatukutanisha 😨 😭 .Mwenyezi Mungu awajaalie faraja Mkeo na Wanao, najua Baba wa Yatima (Mwenyezi Mungu) anashughulikia furaha yao hadi sasa na hataruhusu wapungukiwe.

Nakuombea tuonane Paradiso kwa furaha.
 
The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,055
2,000
Mleta uzi umeniliza. Na hili si kosa lako,bali la wale washenzi. 😭

Hii nchi yetu ingekuwa ni Congo, Sierra Leone au sijui wapi kule na mimi ningekamata 'manati ya mzungu' nilipize hiki alichotendewa Alphonce.

Haya bwana, 'hongera' zao hao miungu-watu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom