Siasa imekua ajira sasa kimbilio la watanzania wengi

FredKavishe

Verified Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Bado siku 34 tumalize mwaka tuingie 2013 kama tunavyojua 2014 kutakua na uchaguzi wa serikali za mitaa na 2015 vikumbo vyote vitakua kwenye udiwani,ubunge,uraisi.

Sasa hizi siasa imekua midomoni kwa wengi vijana wengi hata wazee wana uchu wa kugombea ubunge au udiwani naweza kuita imekua kama ajira sasa maana watu wengi wanakimbia professional zao kama Madr,Eng,walimu kuingia kwenye siasa kwa kasi ya ajabu.

Labda ieleweki haikatazwi madr,Eng kuingia kwenye siasa lakini je waingia kwa lengo gani kujinufaisha wao pamoja na familia zao au waingia kupitisha mikataba mibovu ya chama tawala ili kisionekane kinashindwa au wanaingia kama wazalendo.

Watu wengi sana watagombea mwaka 2014 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,pia uchaguzi mkuu 2015 ndo vizuri kuwa na muamko wa kisiasa ili tupate wagombea wazuri lakini je watatumikia wananchi.

Kumekua na post nyingi naona nataka nikamtoe fulani jimboni je nini kimekusukua kugombea mtu anajibu simple tu aliyepo ni gamba,elimu ya kuunga unga,hafanyi chochote jimboni mimi nitaenda wakomboa wananchi je utawakomboa kivipi nini matatizo yao hajui jibu???

Tumeona matatizo ya sioi sumari aliye simama kwenye uchaguzi wa arumeru mashariki alikua hajui hata hospital ya meru iko wapi.je tunahitaji viongozi ambao watasukumwa na ombe la pesa nyingi kwenye mishahara ya ubunge kuutaka ubunge wakitudanganya watatutumika.

Tunahitaji madiwani,wabunge,raisi watakajua rasilimali zetu na kuzitumia ipasavyo wasisikumwe na pesa kuingia ubunge wasisukumwe na tamaa za kufanikiwa haraka wasukumwe na nia moja ya ukombozi.

Hatuhitaji vijana watakao simama na chadema huku wakijifanya wapambanaji lakini wataenda kutuangusha bungeni tunahitaji vijana wenye nia ya dhati na tanzania yetu vijana watakao buni mirani kuanzia kwenye kata,jimbo,mpaka serikali kuu.

Labda niwe muwazi mimi ni mtu ninayeogopa vijana sana hawa hawa vijana waliokimbilia masomo fulani wawe matajiri wa haraka eti course fulani inalipa ndo nitasoma hawa hawa vijana walioacha masomo ya sayansi eti mtakufa masikini.

Leo wanakuja kwa kasi kuukimbilia udiwani,ubunge kisa unalipa kisa watapata posho na maisha yao yatakua vizuri.tunahitaji viongozi bora haijalishi atatoka nccr,ccm,cuf,chadema lakini mwenye uchungu na nchi wenye nia kweli ya kuinua uchumi anachukia rushwa,ufisadi kwa dhati.

Mimi nina mashaka sana na kizazi hiki cha vijana japo na mimi mmoja wao kinaweza kuwa kibaya kuliko cha wazee wetu kinaweza kuwa cha kifisadi kuliko hiki kinachokwenda kuisha vijana wengi hawana uchungu na nchi yao.

Nilikua natoa maoni kuhusu plan zangu za baada hata watu wakanishaanga wakaniambia utakua mjinga wewe lazima ule kwanza wewe niliwaambia neno moja tu najaribu kubadilisha hiki kizazi cha vijana nakiita cha nyoka.

Hatuhitaji kura za chuki kama zilivyopigwa baadhi ya maeneo tunahitaji viongozi bora,wenye maono ya miaka 30 ijayo wenye kuililia tanzania na tuanze kuambiana mapema ubunge sio ajira ubunge ni utumishi wa umma.

Tusijenge kama siasa ni ajira siasa ibaki utumishi kwamba unakera na kitu fulani na una uchungu nacho kweli utakifanya kuhakikisha kinafanikiwa.

Ubunge,udiwani,urasi sio ajira ni utumishi je ni kijana gani atakuwa tayari kuukata nusu ya mshahara wake akawapeleka maendeleo jimboni,kata, kama yupo aseme sasa.

Je ni kijana gani atakuwa tayari kutopitisha sheria kandamazi kwa wananchi kisa kukiugopa chama.

Niseme tu siamini vijana wa kizazi cha sasa wengi ni wababaishaji wengi hawana nia ya dhati pimaneni kuanzia vyuoni,alevel,olevel nani anatufaa.

Ubunge,udiwani sio ajira

Fred kavishe
 

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,087
2,000
Kama wanasiasa hawatujali tufe njaa? Hata Mimi 2014 naacha chaki naenda tafuta maisha mazuri! Mtu anakaa analipwa na seating allowance mi napiga Kelele toka asubuhi madarasani MWEZI mzima afu mshahara kiduchu acha tukabanane huko huko!
 

FredKavishe

Verified Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Kama wanasiasa hawatujali tufe njaa? Hata Mimi 2014 naacha chaki naenda tafuta maisha mazuri! Mtu anakaa analipwa na seating allowance mi napiga Kelele toka asubuhi madarasani MWEZI mzima afu mshahara kiduchu acha tukabanane huko huko!
Mkuu kwahiyo seating allowance inakuuma hii inabidi iondolewe
 
Top Bottom