Siasa hizi za Kihuni zitaiangamiza Tanzania!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa hizi za Kihuni zitaiangamiza Tanzania!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Sep 29, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siasa zote zinazofuata misingi hii katika uendeshaji wake ni siasa za kihuni na endapo sisi Watanzania tutaendelea kuzishabikia zitaiangamiza nchi yetu!!

  1. Udini
  2. Ukabila
  3. Ubaguzi wa Jinsia na Umri
  4. Ubaguzi wa Rangi
  5. Ubaguzi wa mahali mtu atokako
  6. Ubaguzi wa hali ya mtu kiuchumi

  Mtindo wa kuendesha siasa kwa kufuata misingi hii mufulisi imekuwa inashika kasi siku hata siku na inaonekana ina wafuasi wengi sana na inashabikiwa na wanasiasa uchwara ambao idadi yao kwa sasa si haba! Siku hizi si ajabu kukuta mtu anaomba nafasi ya uongozi kwa kigezo cha "mtoto wa nyumbani" huku akimnanga mpinzani wake kwa kigezo cha "wakuja"

  Udini ni kitu kilichopandikizwa kwenye jamii yetu kwa maslahi ya CCM lakini nasi kama jamii tumeanza kuona kwamba ni jambo la kushabikia na kulipigia upatu. Wakristo wengi ndani ya CCM ya sasa hawajioni wako salama na waislam nao wanawatilia shaka wakristo waliomo CCM.

  Kuna mvumo mkubwa sana ndani ya CHADEMA na uungwaji mkono na wakristo wanaoamini kwamba CHADEMA ni njia pekee iliyotayarishwa na Mungu "kuiokoa" Tanzania na ndiyo maana hata humu JF maneno kama "mungu wa Israel ametenda" au "Bwana atatuvusha salama" hayakosekani kutoka kwa wachangiaji wanaoamini kwamba wao ni CHADEMA damudamu!!

  Ukipita kwenye baadhi ya Misikiti na kusikia shutuma zinazoelekezwa kwa CHADEMA utagundua kwamba ni kazi kwa muislamu asiye mpembuzi wa mambo kuweza kuwa mwanachama wa CHADEMA. Hata zile kauli kwamba CHADEMA ilipata kura zaidi ya CUF kwenye ule uchaguzi wa Marudio kule Zanzibar eti kwa sababu eneo la Uzini lina Wakristo wengi ni kielelezo tosha cha kuonesha ni nini kinaendelea kwenye duru za siasa hapa nchini mwetu!!

  Lakini siasa hizi zinakuzwa na Rais wetu ambaye ndiye yeye kwa kinywa chake alisema kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 kulikuwa na udini bila ya kusema udini huo ulikuwa ni dhidi ya nani na yeye kama Rais wa Nchi atachukua hatua gani!!?

  Kuna watu kwenye siasa zetu ni Waoga waogopao waoga walio na woga wa UKWELI. Ukweli ni kwamba haitatokea hata siku moja nchi hii ikaongozwa na dini fulani dhidi ya dini nyingine au kabila fulani dhidi ya makabila mengine. kwa pamoja kama taifa ndiyo tutaijenga nchi yetu!!
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tatizo la wanansiasa wa tanzania wanaongea sana kuhusu udini ndio matokeo yake haya. nionavyo mimi hata machafuko yatatokana na dini maana uchanguzi wa 2010 uligubikwa na maneno ya kashifa za kidini na kuna baadhi ya wananchi waliaminishwa kuwa kuna chama kina uhusiano na zehebu fulani lakini huu ni ujinga wa kukosa sera na kutokujua nini kitatokea kutokana na matamshi kama hayo.
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kutaja Mungu wa Israel nao ni udini?

  Wanasiasa wengi wanamini ushirikina ndio maana mambo ya Mungu kwao ni kama mbingu na ardhi so acha watu wataje Mungu wao ktk kuliombea taifa kwani hata 2005 tulisemea hivi hivi CCM kwa kutaja majina ya Mungu kwa kila mtu na imani yake.

  Pia all in all umetoa maada nzuri na ninaiunga mkono.
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unafikiri muislamu anaweza kusema "mungu wa Israel" au "bwana ametenda"!!?
   
 5. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatujui Siasa ama tunachanganya siasa na ubaguzi ni vitu viwili haviendani huwa vinaleta madhara makubwa.Kila mtu ana dini yake na akae nae mwenyewe na kila mtu aheshimu kabila la mwenzake ni huu ubinafsi ndio unasababisha watu kubaguana na kupendeleana kikabila au kidini
   
 6. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata post yako ni ya Kikiristo ikilenga kuiosha Chadema!
  Chadema ni chama cha Kikatoliki,kukanusha jambo hili lazima uwe mwenda wazimu!
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,737
  Likes Received: 12,807
  Trophy Points: 280
  Sito uliza umri!

   
 8. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mbaya zaidi hata kiongozi mwenye madaraka na nafasi nzuri ya kulikemea hili nae anaishia kujichekelesha chekelesha tuu. Hayo mengine tuyasubirini tuu, maana banafsi simuoni mwingine wa kulikemea hili isipokuwa mimi mwenyewe kwenye nafsi yangu. Kama na wewe unaweza, niunge mkono. Hakika kuwagawa watnzania kwa njia yoyote ile ni mbaya mno, watu. Sanasana tutambuane na tuheshimiane maana kila mmoja kachagua namna fulani ya kuendesha maisha yake isipokuwa havunji tuu sheria.
   
 9. W

  Wimana JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Kama CUF kilivyokuwa chama cha Kiislamu na CCM chama cha Wapagani wa Kiislamu?
   
 10. Secretary General

  Secretary General Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mungu ibariki Tanzania na watu wake.
   
Loading...