Siasa halisi na thabiti za upinzani kuanzia mwaka 2021

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,564
46,109
Baada ya uchaguzi wa mwaka huu ndipo utachipuka upinzani halisi na thabiti zaidi japo utachukua muda mrefu kuwa imara. Hoja yangu imejengwa juu ya mtazamo huu

1) Kuanzia mwaka 2021 hakutakuwa tena na sababu za watu kuhama vyama vyao.Hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wanasiasa wote maarufu katika vyama vya upinzani watakuwa wamehamia chama tawala au vyama vingine vya upinzani,pia nafasi za uteuzi kwa wahamaji vyama zitapungua kama sio kwisha kabisa.Hivyo kuanzia mwaka kesho na kuendelea kuhama vyama ni jambo litakalokosa mashiko na hamasa stahiki.

2) Kuanzia mwaka huu haitakuwa tena rahisi kwa mtu kutoka chama tawala na kupewa nafasi za juu katika vyama vya upinzani vyenye ushawishi mkubwa.Hali hii itaendelea kuimarika zaidi kuanzia mwaka 2021.

3) Wapinzani wengi waliohamia chama tawala hawatapata nafasi za kugombea ubunge au udiwani na wengi wao watapoteza kabisa umaarufu wao kisiasa na wengine wengi wataachana na siasa.

4) Minyukano ya kisiasa itakuwa ndani zaidi ya chama tawala badala ya ilivyo sasa ambapo nguvu kubwa imeelekezwa kwa upinzani unaozidi kufifia.Hali hii itaupa nguvu upinzani kupumua, kujikongoja na kujipanga upya lakini ukiwa na uzoefu wa hali ya juu na mikakati makini zaidi dhidi ya chama dola.

5) Wananchi wengi wataacha kushangilia siasa za kuhama vyama iwe ni kutoka chama tawala kwenda upinzani au kinyume chake.Kuhama vyama zitakua ni siasa zilizopitwa na wakati kwa watu wengi.

6) Upinzani utakuwa umemulikwa kiasi cha kutosha na dola na ule utakaoweza kusalia umesimama utajisahihisha na makandokando yake,utapunguza pia kutoa sababu hata ndogo za kusakamwa na kuufanya uwe imara zaidi.
 
Bila kuharibu mtiririko wa mawazo yako katika hiyo hoja, naongeza moja kwamba siasa majitaka (kupinga kila kitu kwa sababu ya upinzani) zitakufa baada ya Uchaguzi Mkuu 2020.

Mwaka 2021 (mwanzo wa karne mpya) wanasiasa watashindana kwa jinsi wanavyosaidia wapiga kura katika shughuli za maendeleo. Kwa msingi huo kuhamahama vyama kwa wanasiasa na kujipendekeza kwa mwenye mamlaka ya uteuzi itabaki historia
 
Tunahitajj upinzani wa hoja, huu ufe uje upinzani utakaokuwa unajibu kwa hoja tu sio matusi na dhihaka

Kwa bahati mbaya sana kizazi cha kupangiwa namna ya kufanya siasa na ccm kilishaondoka na Nyerere. Kuna uwezekano wa kushurutisha kwa muda fulani watakacho ccm, lakini ccm haina uwezo wa kulazimisha watu kufuata watakacho. Mfano mrahisi, kama ww ni mzazi, unaweza kumnunulia mtoto wako nguo unazoita za heshima, lakini huwezi kumshurutisha azikubali nguo hizo. Na anaweza na atafurahia zaidi nguo za kizazi chake, kuliko hizo zako unazoita za heshima.

Hivyo ccm hizi siasa za shuruti na kutaka siasa zifanyike kwa utashi wenu lazima mtachemsha. Hao CUF, NCCR nk mnaweza kulazimsha wawe wapinzani na kufanya siasa mzitakazo, lakini hamuwezi kuwalazimisha wananchi kuwakubali, sana sana mtawapotezea mvuto na kisha mtawawatupa kama mpira wa kiume baada ya matumizi. Kama ccm yenyewe haina mvuto, iatawezaje kuwapa mvuto vyama vingine? Hao CUF na NCCR wameshajua hii na awamu ya mtaka sifa, na kwa vile hawana ushawishi tena kwa umma, inabidi wamtumikie shetani ili mradi wapate chochote.
 
Nani alikudanganya kuwa kuna siku ccm itaacha kununua wapinzani? Kimsingi ccm haina hoja wala Sera zenye ushawishi na matokeo yake wataishia kutumia sehemu kubwa ya kodi za wananchi wanyonge kununua upinzani! Hivyo hoja yako kuwa 2021 hamahama itaisha inakosa mashiko
 
Ni mtazamo wangu tu,na nimetoa sababu kwa nini siasa za kuhama hama zitapungua.
Nani alikudanganya kuwa kuna siku ccm itaacha kununua wapinzani? Kimsingi ccm haina hoja wala Sera zenye ushawishi na matokeo yake wataishia kutumia sehemu kubwa ya kodi za wananchi wanyonge kununua upinzani! Hivyo hoja yako kuwa 2021 hamahama itaisha inakosa mashiko
 
Naam Nccr mageuzi wataichalanji Ccm tofauti na Chadema wanaobwata matusi tu
Na hiyo ndiyo siku mtakapolia na kusaga meno. Heshima na thamani yenu hapa jamii forums ni kwasababu ya upinzani wa CHADEMA. Siku NCCR watakapoanza kuimba wimbo mmoja na CCM hamtakuwa tena na wakumtukana so kazi yenu itaisha. Naomba uige mwelekeo wa johnthebaptist ambaye kwa moyo wa dhati, anajua kuwa heshima yake CCM ni kwaajili ya CHADEMA. Hata Ndugai atakuwa kama takataka tu maana hatakuwa tena na wakumnyonga.
 
Tunahitajj upinzani wa hoja, huu ufe uje upinzani utakaokuwa unajibu kwa hoja tu sio matusi na dhihaka
Mnawachagua wapinzani wenu wenyewe,bado mnatuaminisha kuwa nccr,tlp,UDP,cuf siyo matawi yaccm?Mmejichagulia hadi KUB toka nccr?Kweli CCM imechokwa.
Kubalini Tume Huru ya Uchaguzi na heshimuni kila kura ya Wananchi tuwaone.
 
Utabiri namba 3 waanza kutimia

Back
Top Bottom