Siasa haiwezi kutusaidia

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Wana JF,
Nimejifunza kwamba mchezo unao fanyika kwenye siasa hauta tusaidia katika maisha yetu, lazima tupate suluhisho la kudumu kuhusu maisha yetu nje ya siasa na tuamue hatma ya maisha yetu nje ya siasa si vinginevyo, tumeyaona mengi na mengi yanakuja kwanini nasema hivi mfano:

1. Nasikia machinga wamepigwa sana Mwanza, kumbukeni kabla ya uchaguzi mdogo walibembelezwa wakae wanakotaka leo hii wanapigwa, tusubiri kabla ya uchaguzi unaokuja watabembelezwa zaidi sasa niulize kwanini wasipatiwe sehem ya kudumu na pasiwepo na suluhisho la kudumu bila ya kusubiri msimu flani?

Mwenyezi Mungu atusaidie kwa hili maana wengine tumechoka kupendwa kwa msimu. Hakuna kipindi kibaya kama kipindi ambacho mtu unauhitaji mkubwa na huwezi kupata mahitaji yako halafu mtu anakuja ili apate kitu flan anakuletea mahitaji yako unampa ukijua fika huyu sio tabia yake kuamua kunisaidia bali ni kwakuwa anahitaji kitu kutoka kwangu (nipe nikupe) kwa kipindi hiki,

Hebu fikiria mmemchagua mtu au umempa kura zako ukitegemea mengi kwa ajili ya maisha yako pamoja na kurekebisha makosa yaliyofanyika na wengine walio tangulia na waliotakiwa kukusaidia ila hadi sasa harekebishi makosa ya wenziye na anataka akusaidie kivingine ili apate anachokitaka,

Sasa muda wake ni wa mwisho kuwepo kukuongoza anasubiri msimu ufike ili akubembeleze kwa kukupa kidogo tu na akuahidi mengi yanakuja anatumiangharama kubwa akishachukua kiti mtaionja joto la jiwe.

2. Itakapo karibia uchaguzi utasikia ajira kibao zimetoka wakati kipindi hiki haiwezekani, kila unacho kihitaji kwa kipindi hiki kwa ajili ya maisha yako ni ngumu sana haiwezekani kupata ila msimu ukifika kitawezekana kwa kiasi flani na utaambiwa ndio zinaanza inamaana mwaka unaofuata zitakuwa mara tano, kote huku ni kuaminishwa tu kiti kikichukuliwa tu kosa joto la jiwe sasa kwanini swala hili lisiwe la msimu kwetu liwe la wakati wowote maana ni haki ya kila mtu.

3. Unadai fedha zako unaambiwa ni madai hewa kweli? Ikifika msimu utaambiwa tunaanza kupunguza madeni na huku tunapoteza kumbukumbu kuwa tuliambiwa ni madai hewa, sidhani kama tutaweza kuendelea na kuziendeleza familia zetu endapo tutakuwa watu wakukubaliana na misimu, ina maana ukali wa maisha utapingua kwa msimu baada ya hapo basi.

Katika maisha yetu sote hata majumbani kwetu tusiwe watu wa msimu na familia zetu kwa wale tulio oa na kuolewa tusifanyie familia zetu vitu vya msimu, eti mtu una mke usipomletea zawadi hakupi unyumba kweli? Ndoa ni ya nini?

Akianzisha masharti piga chini, aende kwao akapumzike maana ni wajibu wake na sio lazima ila ni sehem yake ya kuwajibika si vinginevyo tunayalea haya ndio maana tuna magonjwa mengi yatokanayo na ukosefu wa haki, acha vitu vya mtego ili upate kitu flan tufanye na tuwape watoto wetu na familia zetu kwakuwa ni haki yao na tuwape kwa wakati ambao tumepata na tumefanikiwa si vinginevyo,

Mwenyezi Mungu atatupa baraka nyingi kama mnvua kwakuwa hatutoi vitu kwa mtego ila ni kwakuwa familia zinahitaji na ni wajibu wetu kama wazazi kuwapa kile wanachohitaji kwa muda muafaka, nimeshuhudia wengi waki aibishwa pamoja na kutoa kwa msimu, tuache kabisa, atakayeona ni vema kutoa vya msimu aendelee ila... Shauri yake.
 
Yeyote anayemuamini mwanasiasa basi anajidanganya, mimi mwanasiasa hua simuamini zaidi ya 50%
 
Back
Top Bottom