VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Siasa ni neno pana. Siasa ni uwanja mpana. Siasa hutawala maisha yetu kila siku. Siasa huanzia kwenye ngazi ya kifamilia hadi ngazi ya kitaifa. Baba na mama hufanya siasa kwa kila mmoja wao na kwa watoto wao. Na watoto ni vivyohivyo.
Kwa dunia tuliyonayo sasa,kukwepa siasa ni kukwepa maisha. Kuacha siasa ni kuacha kuishi. Kuna siasa za kiuchumi,kijamii na kiutamaduni. Watanzania wote sasa ni wanasiasa kwakuwa ni washiriki. Siasa haiepukiki wala haipigiki marufuku.
Siasa ni watu. Siasa ni mchezo unaowahusu watu. Ni nguzo ya amani,mshikamano na utulivu. Watu lazima waambiane majukwaani;waoneshe hisia zao kwenye maandamano na waseme hoja zao Bungeni. Watu waseme,watu wasikilize na kufuatilia.
Serikali isitumike kufanya siasa peke yake. WanaSerikali watafanya ziara na kufanya mikutano. Watafanya uzinduzi na matembezi. Hiyo yote ni siasa. Itakuwa ya upande mmoja. Siasa inapaswa kuwa shirikishi na shindani. Wananchi hufurahia na kujifunza kupitia siasa. Kupiga marufuku siasa za mikutanoni na majukwaani nayo ni siasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)