Siasa bwana, eti watumishi wa umma kukopeshwa hadi 45 milioni na serikali

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Katika mwaka huu wa fedha 2011/12 kuna waraka toka utumishi umetoka ambao unaelekeza kuwa serikali itakopesha fedha kwa watumishi kutokana na ngazi zao za mishahara na kulingana na mahitaji ambayo wao wameainisha.
kuna mkopo kwa ajili ya matengenezo ya magari, pikipiki, samani na kununua magari na muda wa kulipa ni kuanzia miezi 36 hadi 72

wasiwasi wangu;
kuna mambo mengi hayaendi vizuri kama umeme, na miradi ya maji kwa sababu serikali haina hela; je, kuna uwezekana wa kukopesha kiasi hicho cha fedha kwa watumishi wote wa serikali ambao watakidhi vigezo?

Mtazamo wangu
  1. kuna mikopo kama hii mingi ambayo imeshawahi kutangazwa na haikufanikiwa kwa mfano mwishoni mwa mwaka 2009 kulikuwa na mkopo wa fanicha 500,000 watumishi waliomba lakini wengi wetu hatujapata na sijui kama kuna watumishi waliopata
  2. nahisi ni sababu kwa vigogo kujigawia fedha kwa kigezo cha mkopo kwa sababu ipo wazi watumishi wa ngazi za chini hatutapata
  3. nahisi wanataka umaarufu wa kisiasa kwa kusema wanawajali watumishi na kutolea mfano wa waraka huu
maoni yangu
ninauhakika watumishi wengi hawatafaidika na mikopo hii; kwa nini serikali isiamua kukopesha angalau sh. 2 m kwa watumishi wote ambao watakuwa na vigezo?

Karibuni kwa michango.


 
Back
Top Bottom