Siasa: Bunge la 2010 lilikuwa tamu sana

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Bunge la 2010 - 2015

Kupitia hili bunge wananchi Tanzania kwa ujumla ndio mara yao ya kwanza kuweka muda wao na kulisikiliza bunge na ikachochea kila Mtanzania kujiona anafaa kuwa mbunge kwa vijana wa wakati huo.

Kulikuwa na hoja nzuri sana na bunge lilikuwa limechangamka maana hata ndani ya bunge kila kiti cha mbunge kilijaa bakuli la peremende za kutosha za kuchachusha hoja zitoke za moto moto.

Ndio bunge lililochangia kupunguza na kuondoa tatizo la kusinzia kabisa kwa waliowawakilishi wa nchi maana ilikuwa ni aibu na fedhea kulala bungeni huku ukichukuliwa picha. Vijana waliohitimu vyuo wakati huo walipania pasipo mashaka kuwa bunge lijalo lazima wawemo maana waliona mapungufu mengi na namna mtu nzuri kwa mbunge kuweza kutengeneza na kuweka hoja yake ili ipewe umuhimu wake.

Lilikuwa bunge la watu wazoefu wakongwe dhidi ya watu wasomi wapya. Ndio lilikuwa bunge ambalo linakupa elimu ya sheria na kanuni za bunge maana vurugu za hapa na pale za kuhoji na kuuliza maswali zilikuwa hazikauki.

NB

Natamani kuliona tena bunge lijalo likiwa na picha hiyo au zaidi ya hiyo.
 
Back
Top Bottom