Siamini nilichokishuhudia: daladala level seat, hakuna foleni, hakuna kelele, abiria hawasukumani, makonda hawatukani, unafika haraka unakoenda

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
807
964
Hata kama corona ikiisha halafu mtu akatangaza kuwa sasa daladala zinaruhusiwa kujaza watu kama magunia kama ilivyokuwa mwanzo nitamshangaa sana. Kila mtu kukaa kwenye seat yake ni tija kwa afya ya msafiri, kiakili, kimwili na kisaikolojia. Kwa mara ya kwanza leo nimepanda daladala na kwenda ninakoenda na kurudi bila kichwa kuvurugika kwa sababu ya kelele, matusi, foleni na bughdha mbalimbali za daladala na makonda wao.

Kwa maoni yangu, huu ni utaratibu ambao waziri au mamlaka zinazohusika zilitakiwa kuchukua hatua tangu siku nyingi na kuusimamia. Ndio leo nagundua kuwa foleni na misongamano vituoni na barabarani kisababishi kikubwa kilikuwa ni daladala kujaza watu kama zitakavyo -- makonda wana msemo wao gari haijai. Ukiacha COVID-19, ndani ya daladala iliyobeba watu waliojaa kama magunia ni chanzo kingine cha kuambukizana magonjwa kwa njia ya hewa na kugusana/kubanana. Adha ya kubanana huku kukiwa na joto kama tanuru kwa daladala hasa za Dar ni chanjo cha stress na frustrations kwa watu wengi.

Daladala ikishapakia watu wakajaa kwenye seats tu haisimami popote isipokuwa kama inashusha. Daladala zilikuwa zinasimama vituoni au barabarani hata kama zimejaa kwa lengo la kuendelea kubeba abiria, hili ndilo tatizo lililokuwa linasababisha barabara zipitike kwa shida. Maoni yangu ni kuwa huu utaratibu uendelee, na watu vituoni waanze kupanda kwa foleni, yaani aliyefika wa kwanza mpaka wa mwisho.

Nimeweza kufika nilikokuwa naenda haraka sana kuliko kawaida, na kutambua kumbe nilipokuwa naenda ni pafupi mno.

Pamoja na haya "matrafiki" waache tabia zao za kuongoza magari badala ya taa, hawa ndio tatizo jingine kubwa. Hivi inakuwaje trafiki anajigeuza roboti na kuanza kuongoza magari kwa mikono? Taa za kazi gani? Nilishaambiwa mapolisi hawa wa barabarani huvuta magari ya upande fulani ili kumuwahisha mtu fulani ambaye ana uhusiano naye kwa namna moja au nyingine - kiongozi, hawara, mke/mme/rafiki/etc., ni mambo ya ajabu sana! Taa zipo na zinatosha kuongoza magari, labda kama zimezima.

Abiria kukaa level seat lisiwe tu zoezi la muda kwa sababu ya COVID-19, bali liwe ni zoezi endelevu kwa sababu ni zoezi la kistaarabu, linalojali afya na utu wa abiria.
 
Niko barabarani naseleleka kama barabara yangu huku NIKISHANGAA.
 
Hakuna foleni kwasababu ofisi nyingi wamefunga ofisi zao wanafanyia kazi majumbani ... Vodacom makao makuu wamefunga.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimekuwa barabarani kabla ya leo, ofisi zikiwa zimefungwa ilikuwa ni vurugu sana. Hata kama ofisi zikifunguliwa, ikipita sheria ya daladala kutokubeba watu kama magunia, itapunguza msongamano na vurugu za ajabu kwa kiasi kikubwa sana.
 
Kweli aisee. Tunafika haraka tunapoelekea na hakuna bugudha za msongamano. Ila Makondakta ndio wanaoathirika maana kwa kujaza abiria wengi wao walikuwa wanapata posho za ziada.
 
Kiukweli leo nimefanya route zangu za maana ndani ya muda mfupi tuu.....
na nikaongeza route nyingine baada ya kuona hali inaruhusu

Finally nikaja kujiuliza leo si jumanne!! najiuliza hivo nishafika nyumbani chini ya dk 15 wakati nilikua natumia zaidi ya dk 50

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli aisee. Tunafika haraka tunapoelekea na hakuna bugudha za msongamano. Ila Makondakta ndio wanaoathirika maana kwa kujaza abiria wengi wao walikuwa wanapata posho za ziada.

Hata hivyo watapata tu hela tena bila shida. Assume daladala itaenda mjini safari tano kwa siku. Kwa hiyo kwenda na kurudi ni trip 10. Kila daladala inabeba abiria 31. Kama kila abiria atatoa TZS 400, maana yake kwa siku konda atakusanya 10 x 31 x 400 = TZS 124,000. Hapo hatuhesabii anayepanda na kushuka njiani na mwingine kupanda.

Pia magari yatakuwa kwenye hali nzuri kwa sababu hawatayaoverload, hivyo kupungua kwa gharama ya service.
 
Yes level sit imetick leo..But vipi msongamano katika kuzipata hivyo viti katika vituo? Maana isijekuwa tunasongamana kupigania kuwahi siti

Tupangiwe utaratibu wa Kupanga foleni ili kuingia katika hizo daladala..na mita 100 zizingatie sio tunagombania goli mlangoni kisha daladala ikijaa tunazuiwa …….tutaambukizana wakati wa kugombania mlango wa daladala.
 
Hiyo nimeisema mkuu -- kupanda kwa foleni, ahsante kwa kukazia.
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom