Siamini katika serikali Tatu: Ni moja au utengano - Matokeo ya hoja ya Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siamini katika serikali Tatu: Ni moja au utengano - Matokeo ya hoja ya Katiba Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 8, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Bara na Visiwani zinaweza kuwa nchi mbili majirani na zenye uhusiano wa karibu wa kihistoria. Zote zimewahi kuwa nchi mbili tofauti huko nyuma. Kweli zinahistoria ambayo imeiingilia kiasi kwamba haiwezekani kuandika historia ya upande mmoja bila kugusia historia ya upande mwingine.

  Siamini katika serikali tatu kwa sababu tulizikataa mwanzo na sababu ya kuzikataa toka mwanzo hazijabadilika hadi hivi sasa. Ninaamini njia nzuri ni aidha twende kwenye serikali moja ya mifumo mbalimbali ya kiutawala kama ilivyo Uchina (ambapo Hong Kong inautawala na mfumo wake tofauti na Bara) au Canada ambako Quebec kama Jimbo wana uhuru wa aina fulani fulani. Ipo mifano mingine ya aina mbalimbali ya mahusiano ya kiutawala katika pande mbalimbali; Afrika ya Kusini kwa mfano mahusiano kati ya serikali kuu na majimbo yake na makabila yake.

  Kwa upande mwingine hata hivyo ninaamini katika mazingira ambapo Muungano wa sasa hauna watetezi na wengi wanaanza kushabikia "serikali tatu" bila kujibu maswali ambayo Mwalimu aliyauliza kwenye "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" kuhusu uendeshaji na gharama ya serikali tatu na mambo mengine ya msingi sana.

  NI katika kufikiria hayo nimejikuta ninaamini uchaguzi uliopo huko tunakokwenda kuelekea katiba mpya jambo kubwa kabisa ambalo ni lazima tuliamue ni uhusiano katika ya Zanzibar na Tanzania Bara. Siamini kabisa kuwa uhusiano wa serikali tatu ni muafaka ni aidha serikali moja yenye mifumo mbalimbali ya utawala au kutengana kwa Zanzibar kupiga kura ya maoni 2014 kama walivyofanya kwenye kura ya Katiba yao.

  Kura hiyo ya maoni iwe huru kabisa ikiwa na uchaguzi wa aina mbili tu; Muungano wa serikali moja na mifumo mbalimbali ya utawala au Zanzibar kutoka kwenye Muungano na kuwa taifa kamili kama walivyofanya Sudan.


  One Nation, One Country or Separation - Taifa Moja, Nchi Moja au Utengano!

  Hili lipigiwe kura kabla hatujaamua juu ya Katiba Mpya kwani hatuwezi kuwa na Katiba Mpya bila kuamua suala la Muungano. Suala la Muungano ni zito na kubwa sana sawasawa kabisa na suala la Katiba Mpya. Muungano lazima ujadiliwe in light ya kuandikwa kwa Katiba Mpya.
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  "Serikali ya Tanganyika ni Gobarchev wa Tanzania," Nyerere, Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  consensus ad idem .... (meeting of minds) between mzee Nyerere and Mzee Karume haikushirikisha uma wa nchi zote mbili.....this was a defected contract which lacked the minds of the citizens meeting together... ingawa by that time kulikua na sababu nyeti za muungano ambao ni complete kwa maono ya wazee hawa wawili..... ninakubali kabisa kwamba kama wananchi ndiyo wanaofanya nchi kuwa taifa basi ni jukumu la wanachi wao wenyewe kuamua kwamba wanahitaji ushirikiano wa aina gani baina ya bara na visiwani......tutakapoanza kuandika kaitiba mpya basi tuwe tayari tunayo maamuzi yanayohusu aina ya taifa....mimi nadhani tubakie na muungano wa kishirikisho katika nchi mbili yaani zanzibar na tanzania bara kwani tayari zanzibar ni nchi .....kwa hisia zangu... it is close to impossible to deform zanzibar and dilute it with tanganyika
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  flag of zanzibar.png
  map of zanzibar
   
 5. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  Katika hili gharama sio ishu sana, maana hata ukiwa na serikali moja yenye mifumo tofauti ya utawala, bado gharama zipo. South kuna majimbo ambayo yana utawala na mamlaka kubwa zaidi kuliko halmashauri zetu. Gharama ya kuendesha jimbo si sawa na gharama za kuendesha halmashauri hata 5. Ishu ni kuwa na kitu ambacho watu wengi (bara na Visiwani) watakiafiki na hivyo kukilinda. Na ktk hili, tusiache watu wa bara wakaamua kwakuwa ni wengi. Uwiano utumike.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Je, tukiwa na Serikali tatu tutaondokana na ufisadi, mikataba mibovu kusainiwa, shule za kata kufeli kwa kishindo, nk? Hatuoni kwamba tunashughulikia mambo yasiyo na tija na tutabaki kupiga mark time muda wote?
   
 8. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli uliyo wazi kuwa kabla ya kuwa na KATIBA mpya lazima .....tujue ni mfumo gani wa muungano tuwe nawo kwa sababu jambo hilo ni moja ya misingi ya itakayokuwa katiba mpya.

  Lakini naona kama hoja ya KATIBA mpya imeshatekwa na watu wa CCM na hatari yake ni kuwa wanaweza kuamua kupeleka peleka mambo huku masuala ya msingi yakiwekwa uvunguni.
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Binafis napenda Tanganyika na Zanzibar zitengane, then mstakabali wa muungano wake uunganishwe na mchakato wa Shirikisho la A. Mashariki.
   
 10. r

  rmb JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu zetu wazanzibari inaonekana hawako radhi kabisa na huu Muungano tuliokuwa nao kwa sasa, na wala sidhani hata hizo serikali tatu wanazitaka pia! Hawa jamaa wanaona bara ni kama mkoloni vile, wanatafuta uhuru wa nchi yao hawa. Miye naona tupige hizo kura ya kuwa na nchi moja (zanzibar ukiwa mkoa) au nchi huru na wajitegemee.
   
 11. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Muungano inabidi ungaliwe na maamuzi yapatikane ili yaingizwe katika katiba mpya... kwa hali ilivyo sasa muungano umekaa kimaslahi sana...

  watu wengi akimo mimi sielewi na hainingii akilini kuona Wazenji wengi wanatuongaza au kufanya maamuzi ya Wa watu wa bara WATANGANYIKA ambayo yanatuathiri kama utumiaji wa nguvu wa jeshi la polisi huko Arusha... LABDA kila taifa liwe na viongozi wao na sio one traffic kwa wazenj kuzana Bara ili hali wa bara hawana ajira huko zenji hata kumiliki ardhi ni issue kubwa...

  Muungano ni ule wenye maslahi 50-50 na sio kuegemea sana upande mmoja kama ilivyo sasa... Wazo la serikali moja ni na devoved adminstration safi ingaje ni wachache wenye upeo wa kuliona hilo.. Viongozi wengi BARA pia VISIWANI ni Viongozi maslahi na hawajiulizi hivi nchi kama nchi inataka nini.. wanachojiuliza mara nyingi ni hivi nitanufaikaje kwanza....
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Tukitengana theni suala la Shirikisho la Afrika ya Mashariki litaweza kujadilika kwani Zanzibar wanaweza wakaamua kujiunga kule wakati wa Bara inaonekana wanasisa sita..
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  mi naona tungetengana tu, hakuna masilahi makubwa kwetu katika huo muungano zaidi ya kuneemesha tu vigogo na usanii mtupu.
  Tukiweka shirikisho maana yake ni kuwa sisi Tanganyika tutakaoigharamia hiyo serikali ya shirikisho, kwani ukweli uko wazi kabisa kuwa mapato ya kuongoza hata hao wanaojifanya wajanja (wazanzibari) yanatoka Tanganyika.Hivyo mzigo bado utaendelea kuwa kwetu sisi.
  Tukitengana na kuendelea kuwa na ushirikiano wa karibu nadhani ndiyo itakayokuwa suluhisho zaidi.
   
 14. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Unalaumu bila kutoa ufumbuzi

  Hakuna haja ya serkali tatu mbili ima moja muungano huu wa kisanii uzikwe na kaburi wazenj wamesha lichimba wenye macho wanaona.
  mjumbe wa nyumba kumi tg zenj mbunge
  kuna watendaji kibao toka zenj huku tg wakati watg hawana haki hiyo huko zenj
  huoni huo ni ubaguzi dhahiri?
  wamegeuza tg kuwa koloni lao.
  tutengane kama tutarudiana
  baadaye
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180

  Sure!
   
Loading...