Siamini kama kweli benki ndio wameuza nyumba ya milioni 25 kwa milioni 3 kisa wanamdai mteja wao milioni 1 na laki 6. Au kuna utapeli ndani yake?

Kuna vitu fulani katika maisha vikikukuta utajiuliza hivi hi ni ndoto au live. Jamaa alikopa million 3 na laki 5 Access Bank akaweka dhamana mjengo wake wenye thamani ya million 25. Akalipa lipa ilipobaki kama nusu ya mkopo mkewe akamuibia pesa zote za biashara hivyo akashindwa kufanya marejesho yaliyobaki.

Jamaa wa bank wakamuita wakamwambia tunacancel mkopo tunakupa miezi 3 utuletee pesa yetu million 1 na laki 6.
Miezi 3 ikapita jamaa akashindwa kulipa kuna siku akatoka kidogo mida ya jioni aliporudi akakuta nyumba yake ipo tupu.

Akaenda kwa Mjumbe kuripoti Mjumbe akamwambia alipewa amri na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kusimamia watu watoe vyombo ndani na kuvipeleka kwa Mwenyekiti wa Mtaa kwa madai kwamba nyumba imeshauzwa. Jamaa aliposema mimi hayo siyajui na kuingia ndani kwake alikuja mwenyekiti wa mtaa na watu wake wakamtia pingu na kumuita mvamizi

Jamaa akaenda mahakamani, bank na hao madalali hawakutokea mahakamani mara zote 3. Sasa mimi ndio najiuliza hivi ni kweli Access Bank wameuza au kuna matapeli wametake advantage?
Nyumba haiuzwi kama nyanya sokoni. hapo kaibiwa mahakama ndo itamsaidia. kama wameitwa mara 3 hawajaja mahakamank basi yeye asubuhi maamuzi ya mahakama pia in the meantime ajitahidi amuone Lukuvi atamsaidia . Vijana wa bank anatoka shule ndani ya miezi kadhaa anataka avae moka nzuri aendeshe prado lazima awe tapeli wa kudalalia nyumba za watu
 
Kuna vitu fulani katika maisha vikikukuta utajiuliza hivi hi ni ndoto au live. Jamaa alikopa million 3 na laki 5 Access Bank akaweka dhamana mjengo wake wenye thamani ya million 25. Akalipa lipa ilipobaki kama nusu ya mkopo mkewe akamuibia pesa zote za biashara hivyo akashindwa kufanya marejesho yaliyobaki.

Jamaa wa bank wakamuita wakamwambia tunacancel mkopo tunakupa miezi 3 utuletee pesa yetu million 1 na laki 6.
Miezi 3 ikapita jamaa akashindwa kulipa kuna siku akatoka kidogo mida ya jioni aliporudi akakuta nyumba yake ipo tupu.

Akaenda kwa Mjumbe kuripoti Mjumbe akamwambia alipewa amri na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kusimamia watu watoe vyombo ndani na kuvipeleka kwa Mwenyekiti wa Mtaa kwa madai kwamba nyumba imeshauzwa. Jamaa aliposema mimi hayo siyajui na kuingia ndani kwake alikuja mwenyekiti wa mtaa na watu wake wakamtia pingu na kumuita mvamizi

Jamaa akaenda mahakamani, bank na hao madalali hawakutokea mahakamani mara zote 3. Sasa mimi ndio najiuliza hivi ni kweli Access Bank wameuza au kuna matapeli wametake advantage?
Kuna watu wanachulia mkopo kama zawadi. Hayo ndo madhara yake
 
Siku 60 bank walimpa kuwa awapele pesa yao hiyo 1.6 nahisi hiyo ndio notisi
Lakini hayo mengine hayakufanyika zaidi ya kuja watu kuvunja mlango na kusomba vitu vyake vya dukani pamoja na vya ndani na kuvipeleka kwa mwenyekiti na kutia kofuli zao
Jama alipovunja ili apate kulala akaja mwenyekiti akamtia pingu na akamwambia wewe ni mvamizi umevamia nyumba ya mtu aliye inunua kwa shs million 3
Kwanini hukumsaidia ndugu yako kwenye hzo siku 60
 
Acha kutetea uongo broo, Hakuna kitu Kama hicho, huyo Rafiki yako kuna mambo kakudanganya kakuficha muulize vizuri Hakuna bank yenye utaratibu huo, Hakuna bank inayoweza kufanya mchezo huo, huo ni wizi muulize vizur atafunguka kilichotokea ni hatua zipi zilifuatwa had ikafikia huko, na Kama kweli ndio mwenye nyumba katokaje kwenye Nyumba yake aliyojenga atoke tu kisa imeuzwa pasipo yeye kuwa na taaarifa? Acheni uongo wenu, usikurupuke kuleta taarifa za uongo huku huyo anajua kila kitu kila hatua anaijua iliyofuatwa ila anakuficha kwa kutaka msaada wa kimaisha, hata ungekuwa wewe ungeondoka kwenye Nyumba? Hiyo Nyumba haina majirani? Wa kuweza kuingilia Kati? Na je anadaiwa milioni mbili sasa unataka kusema kuwa Nyumba ya 30m imeuzwa 2m? Acha zako za kukurupuka
Mkuu hebu funguka aisee, inaonekana habari hii unaifahamu vyema. Wewe ndio Mwenyekiti wa jamaa aliyeshindwa kulipa hilo deni au Mwakilishi wa ACCESS BANK?
Funguka Mkuu, tupate picha halisi.
 
Kumbuka unaongea na watu wazima humu mkuu,sawa ila kwa haraka haraka jamaa yako hana mausiano mazuri kwa hawa wafuatao.

I) Benki iliyomkopesha.
ii) Mke wake
iii) Serikali ya mtaa
iv) Majirani
v) Ndugu zake
vi) Rafiki zake (ukiwemo wewe).

Kwa Siku hizo alizopewa kwenye notisi kama angelikuwa na mahisiano mazuri na angalau makundi manne kati ya hayo sita kwa Hakika hayo majanga yasingemkuta.
Yawezekana ni kweli anayo hayo unayo yasema lakini je ! Ndio afanyiwe utapeli wa nyumba yake na kuharibiwa vitu vyake na taasisi kibwa kama Access Bank

Kipindi wanampa mkopo walithaminisha nyumba yake kwa million 25

Ameshindwa kumalizia deni la 1.6m wanamfanyia utapeli kwa kuithamisha na kuiuza nyumba yake kwa million 3

Sio sawa hata kidogo
 
Kuna vitu fulani katika maisha vikikukuta utajiuliza hivi hi ni ndoto au live. Jamaa alikopa million 3 na laki 5 Access Bank akaweka dhamana mjengo wake wenye thamani ya million 25. Akalipa lipa ilipobaki kama nusu ya mkopo mkewe akamuibia pesa zote za biashara hivyo akashindwa kufanya marejesho yaliyobaki.

Jamaa wa bank wakamuita wakamwambia tunacancel mkopo tunakupa miezi 3 utuletee pesa yetu million 1 na laki 6.
Miezi 3 ikapita jamaa akashindwa kulipa kuna siku akatoka kidogo mida ya jioni aliporudi akakuta nyumba yake ipo tupu.

Akaenda kwa Mjumbe kuripoti Mjumbe akamwambia alipewa amri na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kusimamia watu watoe vyombo ndani na kuvipeleka kwa Mwenyekiti wa Mtaa kwa madai kwamba nyumba imeshauzwa. Jamaa aliposema mimi hayo siyajui na kuingia ndani kwake alikuja mwenyekiti wa mtaa na watu wake wakamtia pingu na kumuita mvamizi

Jamaa akaenda mahakamani, bank na hao madalali hawakutokea mahakamani mara zote 3. Sasa mimi ndio najiuliza hivi ni kweli Access Bank wameuza au kuna matapeli wametake advantage?

Nilichojifinza hadi sasa bank sio mahali pazuri pa kukopa,asilimia 91 ya nnaowafaham na wamewah kukopa bank walishindwa kurejesha japo sio madeni makubwa saaana
 
Siku 60 bank walimpa kuwa awapele pesa yao hiyo 1.6 nahisi hiyo ndio notisi
Lakini hayo mengine hayakufanyika zaidi ya kuja watu kuvunja mlango na kusomba vitu vyake vya dukani pamoja na vya ndani na kuvipeleka kwa mwenyekiti na kutia kofuli zao
Jama alipovunja ili apate kulala akaja mwenyekiti akamtia pingu na akamwambia wewe ni mvamizi umevamia nyumba ya mtu aliye inunua kwa shs million 3
Hizo Pingu mkiti katoa wapi? Au mkiti ni afande?
 
Inavyoonekana hiyo bank ni majambazi akikosa sheria aanze na huyo mwenyekiti ampeleke kaburin ili liwe fundisho kwa wenyeviti wengine,PANGA LA KICHWA MWAMBIE ASIKOSEE AKAPIKA KWENGINE KWANZA AKALINOE MAENEO YA MBALI.
 
Kuna vitu fulani katika maisha vikikukuta utajiuliza hivi hi ni ndoto au live. Jamaa alikopa million 3 na laki 5 Access Bank akaweka dhamana mjengo wake wenye thamani ya million 25. Akalipa lipa ilipobaki kama nusu ya mkopo mkewe akamuibia pesa zote za biashara hivyo akashindwa kufanya marejesho yaliyobaki.

Jamaa wa bank wakamuita wakamwambia tunacancel mkopo tunakupa miezi 3 utuletee pesa yetu million 1 na laki 6.
Miezi 3 ikapita jamaa akashindwa kulipa kuna siku akatoka kidogo mida ya jioni aliporudi akakuta nyumba yake ipo tupu.

Akaenda kwa Mjumbe kuripoti Mjumbe akamwambia alipewa amri na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kusimamia watu watoe vyombo ndani na kuvipeleka kwa Mwenyekiti wa Mtaa kwa madai kwamba nyumba imeshauzwa. Jamaa aliposema mimi hayo siyajui na kuingia ndani kwake alikuja mwenyekiti wa mtaa na watu wake wakamtia pingu na kumuita mvamizi

Jamaa akaenda mahakamani, bank na hao madalali hawakutokea mahakamani mara zote 3. Sasa mimi ndio najiuliza hivi ni kweli Access Bank wameuza au kuna matapeli wametake advantage?

Kama kuna mteja wa bei ya juu wewe ungemtafuta anunue na cha juu unarudishiwa.
Elewa sekta ya nyumba[real estate ] imeshuka sana, hakuna wanunuzi, si kwamba hela hakuna , hapana ila wanunuzi wanaogopa toka awamu ya tano kuingia madarakani ukisema unanunua kitu ama unafanya muamala wa milioni 10 kuendelea jua kwamba, TRA wanakuja kukagua mahesabu yako, TISS usalama wa taifa wanakufuatilia na PCCB wanafuatilia biashara zako zote, ndio maan sasa hivi hata wenye nyumba kodi zinashushwa isipokuwa tu madalali ndio wamefanya kuzipandisha, ila wapangaji hawapo
 
Inavyoonekana hiyo bank ni majambazi akikosa sheria aanze na huyo mwenyekiti ampeleke kaburin ili liwe fundisho kwa wenyeviti wengine,PANGA LA KICHWA MWAMBIE ASIKOSEE AKAPIKA KWENGINE KWANZA AKALINOE MAENEO YA MBALI.
bank is a legel person, utaiuaje?
 
Hizi taarifa ni za upande mmoja, ukipata kusikia za upande wa pili za banki,utashangaa.
 
Niwafahamishe kitu hapo.
Kiutaratibu benki ana tolerance ya kisheria ya miezi 3 kutoka kwa mteja kutokulipa mkopo...baada ya kuona miezi 3 imepita tena consecutively izo miezi,badae wanaandika demand note kwenda kwa mteja ya mwezi mmoja kwamba kama kashindwa basi dhamana itafidia mkopo wake, mteja akisaini hyo demand note, wanapeleka tangazo kwenye gazeti kwa mwez mmoja tena! Baada ya hapo wanaweka mnada ulio wazi baada ya kutangaza. Na hapo kama nyumba itanunuliwa hata milion 50 na benk wanadai mil 1 na laki 5 basi zingne mteja anatakiwa arudishiwe kiasi kitakachosalia.
Lakin kwa upande mwingine ili umbakize mteja wako lazima ukae nae ili afanye ku re-schedule huo mkopo kama ulikuwa OD basi upelekwe kwenye TERM,lakin pia Management huwa ina uwezo wa kuangalia je mteja karejesha asilimia ngapi ya Principal + Interest ili mteja aweze kupunguziwa zaidi na aweze kulipa na sio kufutiwa kabsaa. Hakuna Benki inayofuta deni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MREJESHO

Nilichogundua hi nchi bado kuna watu wananyanyasika na kudhurumiwa kwa ajili ya kipato chao duni na kutojua sheria na kutopata msaada wa haraka wa kisheria

Jama alienda mahakamani akiwashitaki waungwana action mart na access bank kwa kumtoa kwa nguvu katika nyumba yake bila ya kufuata utaratibu unao takiwa

Mara zote nne wadaiwa hawakufika mahakama ya mwanzo mbagala lakini bado jama alishindwa kesi baada ya hakimu kumuambia kesi yake inahusiana na nyumba hivyo aende mahakama ya aridhi

Jama ikabidi akate rufaa kwa kusema kwamba hakimu wa mahakama ya mwanzo hakuyafanyia kazi madai yake ya msingi aliye yapeleka pale mahakamani

Madai yake ya msingi aliyoyapeleka pale ni kwamba access bank wamemekiuka mkaba wao wenyewe kuwa nini kitafuata kama mteja atashindwa kulipa deni la mkopo ulio salia kwamba ilitakiwa wauze nyumba wakate pesa yao shs 1,600,000 kiasi kilichobaki wampe lakini badala yake walituma mabaunsa kwenda kumtoa katika nyumba yake kwa nguvu

Kwa hiyo akaenda mahakama ya wilaya pale akambiwa aweke wakili yeye akasema hana uwezo huo hivyo atasimama mwenyewe

Kesi ikasikilizwa kwa siku moja wakili wa access bank akasema hakimu wa mahakama ya mwanzo alikuwa sahihi kwa maamuzi yake

Jama akasema benk hawakuuza nyumba yangu kwa mnada ila tu walinitoa nyumbani kwangu kwa kutumia nguvu
Na kama waliuza kwa mnada naiomba mahakama yako iamuru wakili wa bank aithibitishie mahakama yako kuwa

1) mnada ulifanyika lini
2) Nyumba iliuzwa kwa shillingi ngapi
3)Pesa yangu iliyobaki baada ya benk kuchukua pesa yao ipo wapi

Baada kama ya wiki 1 hakimu wa mahakama ya wilaya akatoa hukumu akasema

Ni kweli hukumu ya mahakama ya mwanzo ina mapungufu hi sio kesi ya mahakama ya aridhi ila ni kesi ya kimkataba kati ya access bank na mdai

Pia akasema bank walikuwa sahihi kuuza hiyo amana uliyoiweka ili wapate pesa yao

Kuhusu bank kukiuka mkataba hakimu akasema hana majibu kwa hilo kwa sababu aliyefungua madai hakuleta huo mkataba ili uangaliwe kama ulikiukwa au la

Jama akasema sikubaliani na maamuzi yako nakata tena rufaa kwa sababu

1) umeshindwa kumwambia wakili wa bank athibitishe kama kuna mnada wowote wa halali ulifanyika katika nyumba yangu na hilo ndio dai langu la msingi

2)mkataba nilikuonyesha na una hatua 4 za kufuata endapo ningeshindwa kulipa lakini hakuna hata hatua moja iliyofuatwa na bank

3) kama ulikuwa unataka fail langu la mkopo wa bank lilisombwa na hao waliotoa vitu vyangu ndani na RB ya polisi kuhusu hilo tukio ni nayo vipi wewe hakimu huseme hukuona hivyo vitu katika faili la kesi wakati maelezo ya kukosekana kwa hilo faili la mkopo yapo katika faili la kesi

Jama sasa yupo katika mchakato wa kuenda mahakama kuu

Ila Mimi naamini katika hili jambo la hi nyumba access bank hawahusiki officially ila ni mchezo unaochezwa na baadhi ya wafanyakazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vitu fulani katika maisha vikikukuta utajiuliza hivi hi ni ndoto au live. Jamaa alikopa million 3 na laki 5 Access Bank akaweka dhamana mjengo wake wenye thamani ya million 25. Akalipa lipa ilipobaki kama nusu ya mkopo mkewe akamuibia pesa zote za biashara hivyo akashindwa kufanya marejesho yaliyobaki.

Jamaa wa bank wakamuita wakamwambia tunacancel mkopo tunakupa miezi 3 utuletee pesa yetu million 1 na laki 6.
Miezi 3 ikapita jamaa akashindwa kulipa kuna siku akatoka kidogo mida ya jioni aliporudi akakuta nyumba yake ipo tupu.

Akaenda kwa Mjumbe kuripoti Mjumbe akamwambia alipewa amri na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kusimamia watu watoe vyombo ndani na kuvipeleka kwa Mwenyekiti wa Mtaa kwa madai kwamba nyumba imeshauzwa. Jamaa aliposema mimi hayo siyajui na kuingia ndani kwake alikuja mwenyekiti wa mtaa na watu wake wakamtia pingu na kumuita mvamizi

Jamaa akaenda mahakamani, bank na hao madalali hawakutokea mahakamani mara zote 3. Sasa mimi ndio najiuliza hivi ni kweli Access Bank wameuza au kuna matapeli wametake advantage?
Mi nafikiri ishu hapo ni tahadhari aliepewa na bank hakuifatilia.
Kiukweli bank huwa wanakuandikia demand letter na kukwambia ulipe fedha yao ndani ya siku kadhaa, let's say 7,14 au hata 30.
Bank kwa sasa huwa hawapitiagi mahakamani iwapo watataka kuuza nyumba hvyo huwa wanachagua madalali wao.
Madalali nao huwa wanatoa barua kupitia serikali za mtaa, na kwenye gazeti, na mhusika hupewa.
Siku ya siku huwa wanakuwa na gari na hutoa matangazo sehemu hyo na watu hujazana na mnunuzi yule atakaeweza kutamka dau kubwa ndo mnunuzi.

Swali hapo ni jee, process hizo zimefuatwa? Na yeye alikuwa wapi kwenda kuongea nao hata kma ataiuza yeye atafute mteja na aiuze mbele ya bank maana wao ndo wana hyo hati?
Sasa kama kashindwa kulipa tshs 1.5 milion, ataweza kumlipa wakili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom