Siafu wamekazana,joka lazima litoke pangoni

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,389
285
Nipo kijijini kwangu,Ibangamoyo-kalenga,najionea namna makamanda wenzangu kwa pamoja tunavyo shambulia pango la nchi,kiasi kwamba joka limeanza kufoka ndani ya pango,tunapita nyumba hadi nyumba,mtu kwa mtu huku tukivua magamba kedekede.Siafu sasa wamekazana,wanataka joka litoke huku wakiwa wamelizonga mdomoni,machoni na puani.Hakika likishatoka pangoni litauwawa kwa fimbo laini tu wala si kisonzo au bunduki ama mkuki.SIAFU WAMEKAZANA,TANZANIA KUIKOMBOA.
 
bila CCM (Joka) kutoka madarakani (Pangoni) ni ndoto kufikia maendeleo. safi makamanda, kila mmoja kwa nafasi yake kulishambulia joka.
 
Ila likitoka nanyi mkazingua mjue machafuko ndio kitachofuata!!!!!!

Be care and strategic
 
BIG UP SANA MAKAMANDA.Huku kwetu hatulali,kila fursa inapotokea tunalishambulia joka na sasa linatapatapa.ni kijiwe kwa kijiwe,mtu kwa mtu na hata msiba kwa msiba ili mradi tu joka tunaliteketeza.
 
Ila likitoka nanyi mkazingua mjue machafuko ndio kitachofuata!!!!!!

Be care and strategic

Strategically makamanda tupo gado kwani MABADILIKO NI LAZIMA.JOKA LIKITOKA PANGO LITAKUWA SAFI KWA SIAFU KUISHI KWA HAKI NA AMANI YA KWELI KWA WENGI
 
Strategically makamanda tupo gado kwani MABADILIKO NI LAZIMA.JOKA LIKITOKA PANGO LITAKUWA SAFI KWA SIAFU KUISHI KWA HAKI NA AMANI YA KWELI KWA WENGI

Just for records wengi hawana vyama ila wanataka maisha mazuri sasa wakiwaamini halafu mkawa vigeu geu(kama itakuwa) hawa huwa hawana mapenzi wala ushabiki wa kusubiri vikao halali,atatokea mtu wa kuwaunganisha na hakuna litalozuia na sababu watakuwa nazo,ujasiri wao mtaushangaa!!!!!!!

God forbid!!!!!
 
Jokaa lileee joka lileee:-x2
lina vichwa sabaa
viwili tumeshavifanya supu
 
Just for records wengi hawana vyama ila wanataka maisha mazuri sasa wakiwaamini halafu mkawa vigeu geu(kama itakuwa) hawa huwa hawana mapenzi wala ushabiki wa kusubiri vikao halali,atatokea mtu wa kuwaunganisha na hakuna litalozuia na sababu watakuwa nazo,ujasiri wao mtaushangaa!!!!!!!

God forbid!!!!!

Point taken mzalendo
 
asanteni sana makamanda , kuweni makini na huyo jamaa anayetumia vyombo vya dola huku akisaidiwa na RUSHWA YA ULANZI , kinyume na hapo ni MWEPESI KAMA PAMBA !
 
joka ni rahisi kuliua ila kwa usaliti na unafiki joka litavizia na kumla mmoja mmoja. mshikamano wa kweli na nguvu ya pamoja joka litakufa tu. na ikigundulika kuna msaliti kati yenu anayetaka joka lisife basi ni kumsukumizia pangoni ili kumuuua yeye na joka asiogopwe na kuhurumiwa hata kama alikuwa mpiganaji hodari kiasi gani.JOKA lazima life na mijusi na kenge na vijoka vilivyomo pangoni.
kwani inasadikika kuwa mijusi wengine hugeuka kuwa nyoka.
joka lazima life.
 
to dare is to do!

halitutishii gamba, hata liwe nene vipi,
hata lijipake kimba, tafuata hata wapi,
taliburuta kwa kamba, tusherehekee kwa pipi,
Siafu wamekazana, litoa joka pangoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom