Si wabunge wote wa upinzani wana sifa za uwakilishi! kiu ya mabadiliko imewasaidia!!!

Rich Dad

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
748
133
Wana JF nimekuwa nikifuatilia speech mbalimbali za wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kabla na baada ya uchaguzi.
Wenye upeo mkubwa wa kufikiri na kuchambua mambo mtagundua ya kwamba si wabunge wote wa upinzani waliochaguliwa walikuwa na sifa za kuwakilisha majimbo. Wabunge wengi wa upinzani wamechaguliwa kutokana na hasira za wananchi walizokuwa nazo dhidi ya wabunge wa CCM kutokana na ahadi hewa walizokuwa wanapewa kwa kipindi kirefu. Hivyo basi baadhi ya wananchi wa majimbo fulani fulani walifanya maamuzi ya kuchagua chama kingine cha upinzani pasi na kupima uwezo wa mgombea kama malipizi kwa kile walichofanyiwa na wagombea wa CC kwa miaka nenda rudi.
Baadhi ya viashiria vimeshaanza kujitokeza bungeni na mfano mzuri ni mbunge wa chadema, Bwana John Shibuda. Jamaa hawezi kuunda hoja zaidi ya kutoa mipasho kama walivyo wabunge wengi wa CCM.
 
Back
Top Bottom