Si vibaya tukiiga hili la jirani zetu jamani..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si vibaya tukiiga hili la jirani zetu jamani.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, May 10, 2011.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jana wakati naangalia news kunako runinga TBC nilivutiwa na habari mmoja kutoka nchini Kenya kuwa serikali ilikuwa imeandaa jopo la watalaamu wa sheria ili kufanya usahili wa kumpata Jaji mkuu wa nchi hiyo.

  Hii ina maana kuwa nafasi hiyo ya jaji mkuu watu wanaiomba na kuna ambao wanakuwa short listed na baadae kuingia kwenye interview nzito kabisa. Nadhani hata hapa kwetu tunahitaji kuwa na utaratibu wa kuwafanyia usahili watu katika nafasi kadhaa kama vile Wakuu wa mikoa na wilaya, Watendaji wakuu wa taasisi za umma kuliko haya mambo ya mtu mmoja kututeuliwa watu anaojisikia kuwaweka yeye mwisho wake wanafanya madudu kwa kukosa uwezo...
   
 2. L

  Losemo Senior Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena ilikuwa live kwenye citizen TV. Niliipenda kwa sababu hakuna nafasi ya kufanya usanii hata kidogo. Hapo kitatoka kichwa
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hawa waliliona tatizo hilo tangu zamani na walipoandika katiba mpya, wakaweza vipengele hivyo kwenye katiba yao. Na sie tunapaswa kuliona na kuhakikisha kuwa si kwa jaji mkuu tu, bali nafasi nyingine kwenye taasisi nyeti aachiwi rais peke yake kufanya uteuzi
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  tuna mengi ya kujifunza toka kwa wakenya. kikubwa ni kwamba wenzetu wameona hizi partisan politics zinawavuruga. wameamua kuwa objective kwa nchi. nasi tutakapoona umuhimu wa kuwa above partisan politics na kufanya mambo kwa nia njema ya nchi badala ya makundi tutafika mbali tena kwa kasi ya ajabu (sio kwa kasi zaidi!)
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  siyo hilo tu mkuu, juzijuzi bunge la kenya lilisitisha kazi zake na kuamua kujadili juu ya mfumuko wa bei na maisha magumu kwa wakenya, huko kwenu hata sijui kama viongozi washawahi kuongelea haya!
   
 6. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  tukifikia hapo hata kihelehele cha kuchakachua kura ilikuingia ikuru hakitakuwepo!!
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ashukuriwe raila odinga aliyeupinga ule uteuzi wa awali ambao kibaki aliuchakachua!!

  tukiwa na viongozi jasiri na wawazi kama hao, maendeleo itakuwa "kanyaga twende"
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kama ni kweli basi hilo ni bunge la wananchi haswa!
   
 9. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Da, bac jamaa wako mbele sana...hongera kwao nasi tusiwe vipofu kujifanya hatuoni mazuri ya majirani.
   
Loading...