Si vema kuilaumu serikali juu ya yule "mchora nembo" ya Taifa letu

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,141
20,787
Inasemekana kwamba Enzi hizo baada ya kuchora hii nembo ya taifa tuifahamiyo, huyu marehemu mzee wetu alipewa eneo/kiwanja na Hayati Baba wa Taifa letu kama shukrani ya mchango wa alichoifanyia Tanzania yetu.

Na eneo/lenyewe alilopewa Ni hapo Sinza lego(karibu na ilipokua dagaa-dagaa), sijui ilikuaje ilikuaje ILA inasemekana kwamba huyu mzee wetu alikuja kurubuniwa na wajanja wa mjini na kuuza eneo hilo.

Sijapata taarifa nyingi Sana juu ya alichokipata baada ya kuuza eneo hilo, but all in all mzee alirubuniwa, maana angeweza kufanya vitu vya maana ambavyo vingeisaidia familia yake akiwa hai na baada ya kutangulia mbele za haki kutokana na eneo hilo au pesa baada ya kuuza eneo hilo.

Inafurahisha kujua kwamba hii nembo hakuibuni "just out of the blue", ni kwamba alichora picha za watu halisi waliokuwepo katika zama zake, na mmoja wa wachorwa hawa Ni huyu "Bibi" tunayemuona katika nembo ya taifa ambapo mpaka dakika hii naandika Uzi huu yupo hapo Mwananyamala akiendelea kufurahia hewa mwanana ya mwenyezi Mungu.

Kwa mantiki hiyo Si vema kuilaumu serikali kwamba ilimterekeza mzee huyu, ni yeye mwenyewe tu hakutumia utashi wake. Ingawa si vema kumsimanga marehemu lakini katika hili haitokua vizuri kuilaumu serikali maana iliweka karata yake mezani na Mzee mwenyewe akaamua kuichana karata hiyo.

Mwisho kabisa niseme, Maisha ni safari, ni vema kuchagua njia sahihi na kufuata sheria zinazohusika barabarani ili kufika salama safirini, ukipanda shubiri habadani- hasirani huwezi kuvuna Asali.

"Bastola ya nini tena jamani!!!!"-(Kwa sauti ya Mzee Tupa tupa wa Lumumba)
 
Sheria ndio inafanya nembo kuwa apecial. Bendera ya Japan ni kidoti chekundu tu ila inaheshimika. Nothing so special kwenye uchoraju
 
Back
Top Bottom