Si rahisi kwa kiongozi wa chama cha ushindani kuwa rais tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si rahisi kwa kiongozi wa chama cha ushindani kuwa rais tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Oct 17, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  .....HAIWEZEKANI kwa mazingira ya sasa mpaka haya yafanyike:
  • TUME HURU YA UCHAGUZI
  • KUKOMESHA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA WALIPA KODI
  • MAREKEBISHO YA KATIBA KUPUNGUZA MADARAKA MAKUBWA YA RAIS
  • ELIMU NA UELEWA KUWAFIKIA WANANCHI

  .....na mengine mengi unaweza kuongeza............
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  NA HAYO YOTE HAYTAWEZEKANA MPAKA KIONGOZI WA UPINZANI AWE RAISI

  and
  It can be done, Play your part-JK NYERERE
   
 3. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  subiri miujiza 31st October, maana hata Kikwete mwenyewe atampigia kura DK. Slaa.

  KATIKA YEYE YOTE YATAWEZEKANA!!!!
   
 4. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Yatakayotokea yatawashangaza hao TUME wenyewe.
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,949
  Trophy Points: 280
  Hii imetulia na nimeipenda
   
 6. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakika HAYO YOTE hayawezekani hasa kwa watu waoga, juu ya mabadiliko ya kiuongozi, kisiasa, kifikra, kiutamaduni n.k

  KIUONGOZI:
  Uongozi siyo maumbile kusema kwamba haiwezekani kubadilika, au pindi yakibadilika yaweza kuleta madhara ya kudumu. (Permanent Defomation) Uongozi ni uwezo binafsi au wakati mwingine ni kipaji cha mtu alichozaliwa nacho. Hivyo inawezekana kukawa na viongozi mbalimbali tena wenye uwezo mbalimbali na mitazamo tofauti katika kuongoza na kuleta tija zaidi katika suala zima la kiuongozi. Hivyo sioni sababu ya watanzania kuwa waoga juu ya mabadiliko ya kiuongozi katika nyanja zote za kimaisha.

  KISIASA:
  Mabadiliko mengi katika nchi yoyote ile duniani hutokea chini ya mwevuli wa kisiasa. Hivyo siasa imekuwa ni jambo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile dunia, hivyo sii vyema kabisa kulipuuza suala la mfumo wa siasa za nchi. Hii ni kwasababu viongozi wa kisiasa ndio wasimamizi wakuu wa maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi. Mambo haya yanaposhindwa kufanyika kwa ufanisi, taifa huishia kuwa duni na watu wake kuishi kwa kukosa haki zao za msingi. Hivyo pendekezo KUU na BORA zaidi kukabiliana na hili ni kubadili mfumo wa kisiasa ilikupata kie kilichokuwa kinapelea ama kukosekana kabisa.

  KIFIKRA
  Wapo watu wengi sana wanaoishi na fikra potofu juu ya mustakabali mzima wa maisha yao wenyewe. Ikumbikwe kuwa mafanikio ya kimaisha huanzia kwa mtu mwenyewe. Hivyo ni lazima mtu kuwa na fikra sahihi juu ya kile anachoamini au anachofikiri kukifanya. Wapo walioamini kuwa Tanzania bila Nyerere haiwezekani, lakini sasa imewezekana. Wapo wanaoamini kuwa Tanzania bila CCM haitawezekani hizi i fikra potofu maana hata vyama vilivyoleta uhuru katika nchi mbalimabali za Bara Africa, kama vile KANU na n.k havipo tena madarakani na leo hii nchi hizo zinaendelea na zipo mbele ya Tanzania Kiuchumi, kielimu na hata kimaendeleo licha ya kuwa na rasilimali finyu kuliko Tanzania. Hivyo sio sahihi kuishi chini ya fikra za Dume na za kitumwa namna hiyo.

  KIUTAMADUNI
  Tamaduni nzuri ni zile zinazo muacha raia katika uhuru wake. Siku hizi tunaona tamaduni za jamii husika zinaingiliwa na zikibadilishwa waziwazi na wakati mwingine hubadilishwa ili kulazimisha watu kuacha mfumo fulani na kuingizwa katika mfumo mwingine kwa maslai ya watu wachache. Ni lazima kufika sehemu na kuacha tamaduni za kiukandamzaji ili kuwa huru katika maamuzi bila kuogopa mfumo wa kisiasa, vitisho au hata watu fulani wenye nguvu kifedha au kisiasa.

  Endapo watu watajua ni nini zilizo haki zao katika muhimili wa kisiasa, kimaendelea, Kijamii, kielimu au hata kiuchumi, vyote vilivyotajwa hapo katika Post #1 vinawezekana, maana uoga utawekwa kando na watu wote watainuka na kutaka mfumo wenye ubora zaidi katika maisha yao na maendeleo ya Taifa lao. Katika hili ninashawishika kuamini kwamba kuwa na mtazamo mwingine juu ya siasa za Tanzania ni jambo linalopaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mwenye anayepumua.

  Asanteni kwa leo.
   
 7. M

  Msharika JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ustahadhi pole sana, mwaka huu lazima watanzania tumkabidhi Jk , 31.10.2010 State house leaving certificate, tumechoka kufanyiwa majaribio
   
 8. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I consider this as one of the best comments since I joined JF. You are a great person, truly you are.
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  hata mkioga, mjini hamuendi ng'oooo
   
 10. M

  MUSINGA JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  achana nao hao kwanza hawafiki hata alfu,pili kama kura zao zapigwa humu maana hawako TZ,wamesahau kuwa wamefunga banda wakati farasi keshatoka wapiiiii
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,005
  Trophy Points: 280
  "Steriotypical rhetoric"
   
 12. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mdharau mwiba...
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hii imependeza sana
   
 14. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nafikiri tunahitaji Katiba Mpya kama Kenya, Pili kuna umuhimu wa kuwa na Mabunge mawili kama Congress na Senate ili moja litazame sera na maslahi ya Taifa kama kuteua watendaji wa vyombo mbalimbali vya dola, majaji, wakuu wa vyombo vya usalama na tume huru ya uchaguzi pamoja na kuwa na uwezo wa kumfukuza Rais, wakati Congress ni kusimamia budget na kazi za kila siku za serkali?
   
 15. A

  AMOKSILINI Member

  #15
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Porojo za misikitini hizi.............................
   
Loading...