Si lazima uwe na Pesa ili uwe na Maendeleo: Elimu ya Matumizi ya Choo

Mzee Tumbo

New Member
May 15, 2014
1
0
Doro aliimba stimu ya Kuber ndo imeshaleta matata

Yeye ndo anajua jinsi ipi alikua na demu mkali ila umaarufu akauweka pembeni

Akatia usanii mbele kama ule wa Prof Jize, na skills za Weusi jinsi ambavyo walimshirikishaga Chin Bees mnyama ilihali wao pia wanaimba. Na unaeza cheki skills za Joh au G WaraWara. Ibra da Hasla mzee baba Afande wa Moro, tumejuzwa HipHop tokea kitambo hiko mpaka sasa wakina Mr. Romantic wanaipiga kwenye ushairi, ulizia kwa Michael Ntunga.

Ndo mimi Mzee Tumbo,

Niko hapa kuchana.

Tanzania haina elimu ya choo.

Kama unabisha jaribu kupanda bus la daraja la kati kama wanavyoita Sumatra ama Latra.

Banwa na haja.

Afu uone utajisaidia wapi.

Wabaguzi wao wanajisaidia huku wanasoma magazines vyoo vikavu hata peku unaingia.

Ile mwaka 2014 nilikua nikihadithia raia kwamba wasomi ni watu nadhifu, makini na ndo mfano wa kuigwa.

Sasa yaliyonikera ni jinsi wasomi walivyo wazito kusafisha vyoo.

I can guarantee more than 50% wanaongea kiingereza kama mimi,

Wanapiga mswaki walau mara nne kwa wiki,

Wanaoga,

Na wananawa mikono wakati wa kula ugali.

Lakini hao wote hakuna miongoni mwao anaesafisha choo anachokitumia walau mara nne kwa wiki.

Si ulemavu,

Ni priorities tu.

Lakini pia nazidi kumuelewa hayati Baba wa Taifa alivyosisitiza kwamba si mara zote pesa huambatana na maendeleo.

Unaweza kua huna pesa lakini kila iitwapo leo unasafisha choo unachokitumia,

Manake unaweza tembelewa pia na wageni.

Wageni ambao ni wazee wa mkono.

Ukizikalia je?

Tafakari na endelea kuchukua hatua chanya.

Pia usitumaindi,

Sisi tunaandika tu.

Hatuna ugomvi na wewe.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom