Si lazima mpaka wa nchi uwe katikati ya ziwa. Tutumie usomi wetu Tusimame kwenye ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si lazima mpaka wa nchi uwe katikati ya ziwa. Tutumie usomi wetu Tusimame kwenye ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Aug 7, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Lengo ni sisi tutatafakari sana suala la mppaka wa Malawikwa mapana yake. Maana tunaweza kuwa tunaburuzwa kijanja

  Tuumbuke ugomvi wa miezi michache iliyopita wakati Tanzania ilipoomba kuongezewa eneo la maji. Kumbukeni Zanzibar walimlaani sana mwenzao Shamhuna na Jussa alimponda sana Tiabijuka.

  Kama ni suala la kuongezewa basi kwa nini kuongezewa huku hakukutaja maji ya ziwa Malawi na badala yake kulitaja Indian Ocean pake yake. Kumbuka kwamba unapoongezewa ni kwamba ulikuwa na sehemu, lakini kama hukuwa na sehemu basi huna cha kuongezewa. Hivyo, hata Wizara ya ardhi ilijua wazi kuwa water zone tuliyo nayo ni ile ya east na west hatuna chetu.

  Ukiangalia Lake Natron, mpaka wa Tanzania upo kwenye coordinate (S2.58670 E36.00408). One point of this lake iko Kenya kwenye coordinate (S2.10114 E36.03787). Ncha ya ndani kabisa iliyoko Tanzania iko kwenye (S2.58670 E36.00408).

  Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kutoka mpakani kwenda ng'ambo ya Kenya ni 1.5km yaani kama kutoka Ubungo kwenye mataa hadi Kituo cha Utawala cha University of D'Salaam. Wakati kutoka mpakani kuja ncha ya mwisho ya ziwa kwa upande wa TZ ni 52.5km yaani kama kuanzia Mbezi_Louis hadi Ruvu bridge.

  Kwa maana hiyo kwenye Lake Natron mpaka wa Kenye na Tanzania hauko katikati bali ratio yake yaani Tanzania:Kenye ni 35:1. Nime-calculate eneo nikakuta hii Lake Natron ina 554sq.km Kenye inachukua 1.6 sq.km na sisi tunachukua 552.4 sq. kms. Kwa maana hiyo sisi tunachukua 99.711% ya hilo ziwa lote na Kenya wanachukua 0.289% ya ziwa hilo.

  Tuje kwenye Lake Turkana ambalo liko north of Kenya. The most northen point of this lake is at {N4.65145 E36.16082} yaani 23.2km ndani ya Ethiopia. WHile the most southern point is at coordinate {N2.40027 E36.55652} yaani 232km ndani ya Kenya. Hivyo utaona distance toka mpakani kwenda kwenye furthest point Kenya ina advantage kwa Ethiopia by 10:1.

  Wakti huohuo kwa hili Lake Turkana, the closest point from South Sudan border ni {N4.62853 E35.94680} ambayo ni 5km toka joint boundary ya South Sudan, Kenya na Ethiopia. Hivyo riparian advantage Sudan inaweza kupata kwa Lake Turkana. Riparian ni eneo lililo karibu na ziwa au mto ambalo effect ya maji inafika.

  hata ukiangalia border yetu kwenye Lake Victoria, humo mpaka wetu na Kenye na Uganda uko kwenye coordinate {S0.99426 E33.92751}. The eastmost point ya Kenya toka hapo ni {S0.27608 E34.85068} yaani 130km ndani ya Kenya.

  Jinja is the most north part of Victoria in Uganda na iko kwenye coordinate {N0.49723 E33.36409} na kutokea hapo hadi pale kwenye common border ni 159km.

  Sisi Tanzania the southmost part kwenye Lake Victoria iko kwenye coordinate {S3.08704 E32.77124} na hapo panaitwa Mabale. Kwa maana hiyo kutoka hapo hadi kwenye ile common border ni 265km.

  Kwa maana hiyo ukipanga ratio ya Tanzania: Uganda: Kenya in terms of distance from border inakuwa hivi: {2.04:1.22:1}. Hivyo, umbali wetu toka mpakani ni mara mbili ya wenzetu Kenya na Uganda ambao wanakaribiana!


  Hivyo, ile hoja kwamba mpaka huwa ni katikati ya maji yaani ziwa au bahari si hoja ya kudanganya watoto tena watoto ambao hata hawasomi atlas au ramani yoyote ya dunia hii.

  Si rahisi kuleta hoja hii wakati ukijua kwamba mimi nimetaja maziwa matatu tu lakini kuna maziwa na bahari nyingi tu tu zikoshared na huwezi kusema mpaka uko katikati ya hilo ziwa.

  Mipaka yote iwe iliyopita ziwani al la kulikuwa na treaty fulani iliyoiweka. Huwa tunasema sana Berlin Conference kuwa ndiyo iliyoweka mipaka huku Africa. Lakini tunaofuatilia history tunajua kwamba hata mipaka mingi ya Ulaya iliwekwa miaka 16 kabla ya hii Berlin Conference. Mipaka ya Ulaya iliwekwa kwenye Vienna Congress of 1815.

  Hivyo tangu wakati huo kama hakuna updated ratification ya mipaka basi mipaka ilibaki hivyohivyo. Concept inabaki kwamba kama ukatikati ungekuwa ni hoja basi mifano niliyotoa ingekuwa yaani Natron, Trukana na Victoria ingefanya kazi.

  Zaidi tukijikita na hoja hiyo, basi majirani zetu wawe na wasiwasi precedence ya Malawi, kwamba ukina mwenzi ananyolewa basi wewe tia maji.

  Sikubaliani kabisa na ujanja huu wa kujifanya tunadai sana Lake Malawi hadi tusahau mambo ya msingi kumbe inaweza kuwa ni janja ya serikali tujione tuko wamoja wakijua suala hili litachukua muda mrefu na Tanzania hatuna haki hata chembe ya Lake Malawi halafu tusahau kabisa masuala ya Ulimboka, migomo ya walimu, madaktari, NSSF na maisha magumu kwa kila mtanzania.

  Namalizia tena, si lazima mpaka wa ziwani uwe katikati ya maji kama tunavyoaminishwa. TUna akili na sisi tunasoma.

  UPDATE AS AT AUG 08, 2012 AT 14:26:

  NImesoma post zote nikidhani kuna hoja inifanye niungane na wanaotofautiana na mimi. Nimeachana na hoja za humu nikanunua RAIA MWEMA ili nisome hotuba ya bernard Membe aliyotoa bungeni kuhusu hili suala la Malawi.

  Wakati nanunua gazeti nilitumaini kabisa Membe atakuwa na hoja ya ku-convice kwani humu JF mnaongea tu kama mimi. Kwa wale waliosoma RAIA MWEMA wafungua attached paper kwenye ukurasa wa iv. Ndipo anaeleza msimamo wa Serikali kuhusu mpaka wa Ziwa Malawi.

  Nakiri kwamba hata wakati naleta thread hii, nilitumaini Bernard Membe atakuwa ameongelea findings ambazo zingetushawishi na mimi nisingesita kuungana kwenye nia ya kukidhi madai haya ya Lake Malawi.

  Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.

  Siku moja nilifanya hesabu ubaoni nikapata jibu na baadaye nikaongeza madoido mwalimu akanikata maksi akasema "Kujitawaza kwingi mwisho unashika kinyesi". Naona ndugu yetu Waziri Membe kaingia katika mtego huu. Kwa nini nasema hivi? Ninanukuu majibu yake kama ifuatavyo:


  ****
  Mheshimiwa Spika,
  Lipo tatizo la muda mrefu kati yetu na nchi jirani ya Malawi linalohusiana na mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Tatizo lenyewe ni kwamba Malawi wanadai kwamba ziwa lote kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa mwaka 1890.

  Mheshimiwa Spika,
  Tanzania kwa upande wetu tunasema kuw ampaka wa kweli kati yetu na malawi unapita katikati ya ziwa hivyo kufanya
  eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati Latitude digrii 9 na digrii 11 kuwa mali ya Tanzania kwa mujibu wa mkata huouo wa Heligoland wa mwaka 1890 ambao ulikubali kuwa kwa vile kuna maeneo ya mpaka ambayo hayana mantiki, pande zinazohusiana zikutane na kurekebisha. Aidha tunazo ramani ambazo waingereza wenyewe walipitisha mpaka katikati kama ulivyo mpaka kati ya Msumbiji na Malawi.
  ****

  Nimemalizia hapa kwa sababu mengine yanayofuata ni diplomatic process. Sasa hapa tuchambue hotuba hii ya Membe. Binafsi nimeusoma mkataba wote wa Heligoland na wala si alichokisema Membe. Kama membe anataka kuikomboa Tanzania walau tupate sehemu ya Ziwa basi washauri wake wamempotosha kutumia mkataba ule ambao hautetei hoja yake hata kidogo.

  Lakini pia Membe ni mmoja wa wanaodhani watanzania wa sasa hawajui kufukua mambo na ndiyo maana kwenye thread yangu nimesema tutumie usomi wetu. Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.

  Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}.

  Ukiangalia coordinate hizi maana yake ni kwamba Ziwa Malawi linaishia kwenye Latitude 9.49214. Sasa hapa Membe anasema eti ni kuanzia Latitude 9. Kwa maana hii ya Membe kama Ziwa ni letu kuanzia latitude 9 maana yake ni kwambaMmembe kafanya makosa kwa kulirefusha ziwa hili kwa umbali wa 54.4km kuelekea kaskazini!

  Watu mnaotoka kusini hasa Mbeya mnafahamu sehemu iitwayo Matamba. Hapa coordinate zake ni { S9.01171 E34.09959}. Kwa mujibu wa Membe, hii Matamba ingekuwa imeguswa na Ziwa hili!

  Hakika waliomletea Membe hizi data wamemvuruga kuliko kulietengeneza suala hili. Ziwa Malawi au Nyasa linaishia kwenye Latitude 9.49214 kama nilivyosema hapo juu. Hapa membe kadanganya Bunge na kadanganya watanzania kasi kwamba sijui sasa ni nani mwenye nguvu ya kulitetea hili.

  Tuje sasa kwa upade wa kusini yaani unaotambuliwa na membe kama sehemu yaetu ya Ziwa. Membe anasema sisi mali yetu ni mpaka kwenye latitude 11. Sijui wangapi mmeona kosa hili la mwaka. Unaposema kwamba unaishia hapa kwenye Latitude 11, je mnaotetea hoja hii mnaelewa madhara yake? Kama hamyajui basi mimi nayasema hapa.

  Kama Membe kasema Bungeni kwamba tunaishia kwenye Latitude 11 basi maana yake pale ni kaskazini ya sehemu iitwayo Liuli ambayo iko { S11.05023 E34.63908}. Kumbe, Mwanakijiji wa Liuli haruhusiwi kuvua samaki kwenye ziwa lile kwa sababu ni sehemu ya Malawi, kwa mujibu wa Waziri Bernard Membe!

  Yaani mwanakijiji huyu wa Liuli, anakuwa amekiuka mpaka kwa kilomita 6.6 kwa mujibu wa Serikali anayoshiriki membe wala si kwa mujibu wa Serikali ya Malawi!

  Nimeanza na mfano huo wa Liuli ambao najua wengine hampaju ahapo. Sasa tuje kwenye mfano ambao wengi mnaujua na mmeutumia kunipinga humu na kuniita mimi ni mmalawi.

  Mfano wenyewe ni wa Mbamba Bay. Ndiyo maana nimesema kajipangeni hii kesi tutajikuta tunasambaratika tukidhani tunatetea huku tunajiangamiza. Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.

  Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Mbamba Bay haiko katika eneo linalotambuliwa na Waziri Membe kwa latitude degree 0.30519!

  Uki-convert hizi latitude kwenda kwenye kilomita basi maana yake Membe haitambui Mbamba Bay kwani iko 33.7km nje ya eneo ambalo Tanzania tunamiliki ziwa!

  Waziri membe pia inaelekea kuwa hajui mpaka unavyopita pale Msumbiji. yeye anasema kule ni nunu kwa nusu lakini wote fungueni ramani muone kama hilo nalo lina ukweli. Mpaka wa Msumbiji ni nusu kwa nusu kuanzia kwenye latitude 11 had 13 lakini kuanzia hapo keuelea kule chini kusini ziwa lote liko sehemu ya Malawi na linaishia kwenye coordinate {S14.44635 E35.23539} ambako ni latitude 14.44635.

  Ndiyo maana tangu mwanzo nimesema, tujenge hoja zinazojikita kwenye ukweli na tusishabikie mambo kama vile Simba na Yanga. Hapa hatufanyi ushabiki. Hapa tunasaidia kujenga na kupima hoja kama kweli tunaweza kuisaidia nchi yetu kupata sehemu ya ziwa hili.

  Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
   
 2. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,127
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  ndo tatizo la kujifanya akili kubwa kumbe kilaza!!!
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Yanapokuja masuala ya nchi uzalendo ni muhimu haijalishi ni hoja gani.Hoja yako ya kuilaumu serkali eti inataka kutusahaulisha matatizo ya nchi nadhani haina mantiki.Cha msingi tuungane wote tujue mwisho wa hili ni nini.Na inawezekana unaongea hayo maneno vile wewe hauishi kyela...
   
 4. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Soma hoja zangu zote kisha unga mkono au pinga kutokana na uongo au ukweli nilioandika. usitunge!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pumba zingine hizi. Sijaona huo mchele uko wapi?
   
 6. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Fafanua, nani kajisema ana akili kubwa. Binafsi sijasema wanaounga au kipinga mkono haja ya Malawi wana akili kubwa au ndogo.

  Nimeleta findings zangu na nitafurahi kama kuna mtu atazi-prove wrong.
   
 7. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Lete hoja tujadili na tufaidike. Hayo niayoyajua na niliyoyaweka humu ni kwa sababu kuna watu waliweka hoja nikasoma mahala hoja zao nikaridhika nikaziweka humu.

  natumaini mnaojibu tutapata hoja zaidi na si vinginevyo.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Nimechanganyikiwa na Maelezo yako lakini Umekubali kitu kimoja hayo Maziwa yote Turkana,

  Natron yote Nchi Wahusika wana Uhuru wa kuyatumia hayo Maziwa bila matatizo; Tanganyika na

  Ziwa Nyasa hatuta weza Kufanya Uchunguzi wa GAS na OIL kwa Upande ambao uko karibu na

  Nchi yetu; hapo ni tatizo - Hata Wananchi wa Tanganyika hawawezi kuvua kwenye hilo ziwa...
   
 9. b

  baajun JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilikaa sehemu moja inaitwa Lituhi.wakati wa tatizo la sukali nilikuwa naona kuna meli kubwa zinatoka amlawi kuleta sukali huku kwetu,na pia nafikiri wote tukubaliane kuwa sukali kwa kiwango kikubwa ilikuwa inatoka Malawi wakati ule.Sasa kama meli ilikuwa inakuja vile polisi walikuwa wapi,jeshi lilikuwa wapi,?????????.mimi naona kuwa kuna ukweli ziwa lote ni la wamalawi.Alafu wakaacha tulitumie kwa meli zetu kutoka mbambay to kyela.Nani ni jirani mwema hapo?tuangalie kwa mapana sana ndugu zangu.Na tusikimbilie vita tu.Wamalawi wanashida kweli ,na sisi pia tunashida kweli,sasa tuingie kununua silaha kuwaangamiza wanandugu hawa kweliiiiii?????????????????.Hii tatizo tunaweza kukaa na kulitatua bila tatizo lolote lile.Kwani tuendako mbele tuna mpaka hizi nchi zote kuwa nchi moja sasa tatizo la nini???????????MUNGU BARIKI WATU WENYE HEKIMA NA KUTAZAMA MBELE.EPUSHA VITA ,LAKINI UTUIMARISHE KUPINGANA KWENYE VITA HII YA KUMWONDOA FISADI HAPA TANZANIA.
   
 10. c

  chama JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Najaribu kupitia jiografia ya sehemu mbalimbali lakini mpaka wakati huu sijaona kituko kama hiki cha walawi

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  [h=6]MALAWI FIGHTER JETS HIZI HAPA CHINI
  [/h][​IMG]
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  moja wapo ya akili fupi sana, unajua humu ndani kuna wamalawi wengi tuu ambao walilowea huku kwetu, tukawalisha tukawasafisha na kuwavisha nguo, wamepata akili na elimu sasa wamekuwa mashushushu wa nchi yao...unapoongelea suala la mipaka ya nchi ya tz, hasa kuhusu ziwa nyasa, usilinganishe kabisa na natron au tanganyika...kwasababu natron hatujawahi kuwa na ugomvi na kenya...utofauti wake na nyasa ni kwamba, nyasa imekuwa kwenye mtafaruku tangu tupate uhuru, na mtafaruku huo haujawahi kutatuliwa....hivyo kusema kwamba kwasababu natron mpaka haupo katikati basi na nyasa hivyohivyo ni upungufu wa akili, na inaonyesha wazi wewe si mtanzania, ni mmalawi unataka kutupiga changa la macho watz hapa.....je? kuna mtafaruku wowote tangu uhuru tuliwaipata na kenya kuhusu natron? au ziwa lingine lolote lile? hapana.....ila suala la nyasa lina mtafaruku na halijawahi kutatuliwa once and for all, sasa mmoja akisema anatafuta mafuta mle wakati suala halijatatuliwa ni uchokozi na dharau......tz tumekuwa tukitumia ziwa lile kwa muda, tumejenga bandari mle pale mbambabay na kyela, tumekuwa tukisafirisha bidhaa zetu kwa meli toka mbinga hadi ludewa hadi kyela, tumekuwa tukivua samaki tupendavyo hadi katikati ya ziwa,...sasa leo kwasababu kuna mafuta na wao kuona kuwa hatukutatua mgogoro ndo waseme ziwa lote lao, kwasababu sisi hatupo au wametudharau?......akili za mbayuwayu...
   
 13. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nngu,

  Kama tumeamua kuondokana na tatizo la Lake Malawi basi toeni hoja ili tujue kinachotupeleka huko ni nini. Mimi ninavutwa na hoja kwamba lile ziwa si letu hata kwa sababu hizi ndogo nilizoeleza humu na kwenye thread zingine.

  Lakini kichekesho kiko kwenu mnaotetea kuwa ziwa lile ni letu. Kichekesho ni jinsi ambavyo hata wenyewe mnaona wazi mlivyoparaganyika bila kuwa na hoja moja thabiti na mnajikuta mnatamka neno uzalendo lakini mkiulizwa kidogo tu kila mtu anajibu kwake.

  Ona kama wewe unavyojibu. Unasema hayo maziwa niliyotaja yanatumika na nchi jirani. Mimi sijajenga hoja ynagu kwa msingi huo na hakika hukua na sababu za kuleta hilo wazo lako kama umesoma thread yangu vizuri.

  MImi nimesema kuwa kuna percentage kidogo kwenye zone za hizo lake hata kama ni 0.2%. Nimetoa mfano Lake Turkana ambako South Sudan haiwezi kuleta ubishi kama mnaoleta kwamba na yenyewe ifaidike kwenye ziwa hilo kwa sababu tu iko kilometa tano toka Lake Natron.

  Hoja yangu inabaki palepale kwamba concept ya mpaka kuwa katikati ya maji au wengine mnavyoitw nusu kwa nusu ni uongo.

  Kama kuna anayesema ni ukweli basi aniumbue.
   
 14. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,497
  Likes Received: 5,975
  Trophy Points: 280
  umejitahidi kutoa ushahidi lakini umesahau kwamba mgawanyo wa sehemu ya maji unategemea pia urefu wa shore yako mfano mgawanyo wa caspian sea kati ya iran, urusi na azerbaijan kama sikosei. halafu ujasema unafikiri mpaka uwe wapi? au ndio ziwa lote liwe la wamalawi!! ebu fikiria zaidi ya 50% ya maji ya ziwa nyasa yanatoka mto ruhuhu wa ruvuma ukiongeza kiwira na songwe tanzania inachangia karibu asilimia 70% ya maji je wakichukua ziwa nasisi tukiweza kupampu maji na kujenga artificial lake itakuwaje? mifano uliyotoa ni kwamba nchi zilizopata eneo dogo pia zina shore fupi kenye hilo ziwa mfano kenya kwenye victoria au ethiopia kwenye turkana lakini kwa tanzania bila hata kuchanganyana na maholligolland treaties mpaka unatakiwa uwe katikati ya ziwa
   
 15. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Mtafaruku si tamaa zako? Kwani ni lini uliwahi kumiliki hata sentimita moja? Kutafuta mafuta ni moja ya shughuli nyingi za kiuchumi walizowahi kufanya Malawi.

  Soma kwanza concept ya riparian zone ndipo ujue kwa nini Mbamba bay iliweza kujengwa.
   
 16. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  no wonder nilikuita mmalawi, sikukosea. mtajibeba mwaka huu manake mtapigwa hadi hamtakujamrudie tena fyokofyoko. mabwabwa nyie, ndo maana mmegawa mmatako kwa wanaume wenzenu.
   
 17. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Usidanganye watu na nyingi mnaokurupua na ndiyo mnadhani mnaisaidia Tanzania kumbe mna lengo la kuiumbua kwa mgogoro ambao tunasaid kuonyesha ni vipi itashindwa.

  lake Malawi ni rift valley Lake hivyo haiko katika category unayoitaja. Kuhuus nisema mpaka uwe wapi inaonyesha mlivyo kutaka kujua mapenzi ya mtu ama mumshambulie au kumu-applaud wakti tunachotaka ni kujadili chanzo cha yote haya.

  Hebu pitia blogs za wamalawi hata zile zilizoletwa humu uone kama kwa akili hii mtawatoa nje.

  Nashukuru kwa sentensi yako ya kwanza kwamba nimejitahidi kuleta ushahidi. Sijaleta, nimeangalia ramani ambayo hata mtoto wa darasa la sita anaweza kufanya na akaandika haya niliyoandika humu.

  Wenzako wana concept ya nusu kwa nusu. Mimi hiyo ndiyo nimeipinga kwa nguvu zote na ndiyo ninayoongopa kwam tutaaibika tutakaposhindwa maana ni dhahiri.
   
 18. c

  chama JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Una wazimu sana wamalawi wanakufa njaa hawana hata uwezo wa kununua Chakula nje wanategemea kulishwa na WFP uwezo wa kununua ndege watautoa wapi acheni mambo kucopy na kupaste kupotosha watu

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 19. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  kanawe uso mkuu
  ....
   
 20. A

  August JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  concept ya nusu kwa nusu ni kwa sehemu inao pakana na shore ya tanzania yaani mpaka upo katikati ya ziwa na hiyo shore ya tanzania,
  kuhusu kusoma kwako nk unaonekana umesoma lakini hukuelimika, kufuatana na hizo cordinates za north , south, east, west nk, kwa sababu mipaka inapowekwa inatokana na umbali wa shore yako na ya yule jirani yako, lakini kutokana na maziwa au bahari kutokuwa na mstari ulio nyoka , basi ni wazi mwingine atapata kidogo ikiwa sehemu yake ya ukanda wa maji ni sehemu iliyo nyembamba kupakana na wewe.
  rudi shule mwalimu wako wa geography akufundishe vizuri. ili siku nyingine ukitumwa kwenye mikutano ya kimataifa usitoe point za kitoto
   
Loading...