Si kweli? Watanzania wachambwa: Kiingereza, Wizi, Viongozi kujipendelea... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si kweli? Watanzania wachambwa: Kiingereza, Wizi, Viongozi kujipendelea...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  25/10/2012
  0 Comments


  Awali ya yote namshukuru mwenye twitter ID ya "Mabala The Farmer" @Decenttz kwa kuni-tag kwenye tweet-video ambayo imepachikwa hapo chini.

  Kwa ufupi, katika video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, Novemba 14, 2010 na hadi sasa ninapoiweka 'post' hii, imeshatizamwa mara 81 tu, msikilize anayejitambulisha kwa jina la
  Marie Francis, mwasisi-mwandaaji Mbio za Marathon za Mlima Kilimanjaro akizungumzia Kilimanjaro Marathon anayoiandaa.

  Katika mambo aliyoyazungumzia, kwa mtizamo wake anadhani chaguo la Watanzania kutumia Kiswahili punde tu walipopata Uhuru lilikuwa la makosa. Ametolea mfano wa watu wanaokwenda kuomba viza za kusafiria kuwa wanazungumza Kiingereza kibovu au kutokuweza kabisa kujieleza katika lugha hiyo, katika mfano wake, amewalinganisha na majirani zao wa Kenya wanaowapiku.

  Pia amezungumzia tabia ya udokozi na wizi wa hata chupa za maji.

  Vile vile amezungumzia tabia ya baadhi ya viongozi kutumia nafasi na nyadhifa zao kuingiza ndugu na jamaa zao katika mbio hizo, ?pengine wa nia ya kujipatia vya bure.


  [​IMG]Mabala the Farmer@Decenttz
  Mmemsikia huyu mama anayemiliki kilimanjaro Marathon? Kawaua watanzania! youtube.com/watch?v=MadUiA…@Chahali@subinukta@JMakamba@zittokabwe


  Preview of Mt. Kilimanjaro Marathon - Running Network - GLSP - YouTube
  Matamshi ya Mary katika video hiyo dakika kwa dakika yanasomeka yamenukuliwa hapo chini. Maandishi haya yanaweza yakawa na makosa madogo madogo kwa kuwa tafsiri (auto transcription) inafanywa na software moja kwa moja na lafudhi huweza kuisababisha software ikabandika neno lisilo sahihi. Nimejaribu kuyarekebisha kadiri nilivyoweza... changanya za kuambiwa na zako... utapata maana kamili tu!
  ---


  Source:
  http://www.wavuti.com/#ixzz2AJ86Q5JS
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  No Comment... KIKULACHO ki NGUONI MWAKO!!!
   
 3. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Sijaisikiliza lakini je kakumbuka Uzinzi? Make hiyo sifa nayo tunayo sana.
   
 4. l

  lengijave Senior Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimemsikiliza huyo mama lakini sijaona kama amekusea sana kwa vile anavyojieleza,ni kweli wakenya wanajua kuongea kiingereza kuliko watanzania na pengine pia watanzania wanajua kiswahili kuliko wakenya,sijaona ubaya wowote, na kwa sisi tunaokaa hapa arusha pia tunaliona hilo,hata kwenye interview mbali mbali wanafeli pia,amesema kuna waizi wa maji lkn mi nilivyomuelewa ni kweli kuna waizi wa vitu vidogo vidogo kama maji,soda,kuku,hela mfukoni,kamera,simu,chakula hawlipi sometime(ndio maana wakati mwingine wezi wanachomwa si kwamba wameiba kitu cha gharama)Pia katika tanzania kuna mikoa imeizidi mikoa mingine kwa mfano Arusha wanaongea kiingereza na kutumia internet kuliko mikoa mingine hii ni kutokana na kazi zao nyingi kuhusisha wageni/watalii.
  Please note:hamaanishi kuwa hakuna wasiojua kiingereza vizuri,ila idadi ya wanaojua na wasiojua wasiojua ni wengi,kwa mfano watumiaji wa jamii forum wengi wanajua,lakini wakazi wa jimbo wanalotoka raisi hawajui,by the way kiingereza inaweza ikawa ni mojawapo wa tatizo kwa watanzania na wana riadha kwa ujumla mi sidhani ni tatizo,tatizo ni mfumo wa utawala ambao haujali maslahi ya wengi.

   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,467
  Trophy Points: 280
  wakati wachina wanajivunia kwenda mwezini na kichina chao, sisi tunalaumiana kwa nini hatujui kiingeleza. Kana kwamba ndio kinaongeza ubunifu.
   
 6. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lugha ya kiingereza sio ishu kubwa sana ya kubeza watanzania.Kwanza nchi nyingi za bara la Africa wanazungumza Kifaransa zaidi kuliko kiingereza.N baadhi ya maraisi wao kiingereza hata cha kuombea maji na maisha yanaenda.Ukienda uchina, Ufaransa, Ujerumani Russia na kwingineko wanatukuza lugha zao zaidi kwa kufundishia na mawasiliano.Kwanza kiswahili kama Lugha kuu ya nchi za afrika mashariki na kati Tanzania ni kinara wao, na bado hatuwashangai.Kama ni wizi na udokozi upo pia kila mahali duniani!
   
 7. n

  ngoshas JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 710
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anafikiri ulaya wote wanaongea kiingereza, uingereza yenyewe hoooi kimaendeleo, ujerumani na kijerumani chao ndo championi wa maendeleo ulaya, kaniudhi huyu, eti watanzania wachambwa
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Unaweza kusema hivi kama una mitaala yako ya maana ya Kiswahili, vitabu vyako, viwanda vyako, watu wa nje wanatafsiri vitabu vyao kwenda kiswahili kwa wingi etc.

  Leo hii hutengenezi hata pini unataka kujilinganisha na China?

  Mchina anaweza kuingia kwenye internet akafanya kila kitu kwa kichina.

  Wewe kutengeneza computer ya Kiswahili tu kazi, sembuse kuwa na e commerce network ya kiswahili kwenye internet.

  Halafu unataka kujilinganisha na mchina?
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwakweli sijui tufanyeje kwani hata mimi wiki jana nimesononeka sana baada ya kushindwa kuaminiwa kuwa nasema ukweli kwakua tu ni mwafirca-mtanzania..Ilibidi waniombe radhi wakafanye utafiti kidogo kujua who is right kati yangu mimi niliye waambia ukweli wangu na huyo mwingine aliyeamua kupinga kwasababu tu ya pre-conceived mind kwamba wengi wetu waongo na hatuko honest...

  It pained me a lot kwani kwa muda mrefu nimekuwa katika hiyo situation ya kutokuwa fully trusted (japo naona wananipa benefit of doubt lakini hawamini kama naweza fanya jambo mwenyewe bila unagalizi wa karibu) nami nimejitahidi kwa nguvu na uwezo kutokufanya hata kitu kimoja kuhalalisha mawazo yao hivyo nimekuwa makini kwa kila usemi tendo hata wakati mwingine kukwepa baadhi ya malumbano ili nisije tia neno kwa hisia nika-justfy hisia mbaya iliyo juu ya watu wa jamii yangu (waafrica na hasa watanzania) kutokana na mawazo yaliyomo ndani ya hawa ninao ishi nao kwa muda...

  Huwezi amini it took something like a week kuamuliwa kwa jambo ambalo lingetakiwa kuwa la dakika mpaka walipothibitisha ndiyo wakanipa go ahead....Najiuliza kama kusingekuwa na evidence kwenye authentic sources ingekuwaje?

  Siwalaumu hawa kwa hisia zao kwani pia kuna mambo ambayo kama nchi tumeshindwa kuyasimamia na hivyo kutoa mwanya wa sisi kutoaminika..Ni juzi hapa jf kulikuwa na andiko lenye neno 'a country with high rent seeking behaviour...' Hivi sijui kama watu wanalielewa hili neno kwa usahihi wake...Kwa wachumi inamaana watu wanaopenda malipo wasiyostahili..Ama hata kupenda vya chee...Its very bad kwakweli ebu tufikie wakati tukataye huu ujinga na tusimame kama jamii kuwapinga wote wanaotuchafulia jina la taifa letu...
   
 10. A

  Ame JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Huko sehemu nyingine wezi hata siku moja hawasifiwi hadharani ama kutolewa matamko kama tukiwashugulikia basi nchi itayumba....Kuna mambo tukubali kuwa yanachangiwa sana na viongozi wetu..Siyo rahisi watu ku-justify wizi mdogo kuwa tatizo kama hawajiliona kuwa ni tatizo kwa wale wanaobeba image ya Taifa....Hili ni dhahiri kabisa nyumba inayoheshimiwa hata kama kuna mwizi humo ndani siyo rahisi watu kujua lakini yenye wazazi ambao hawana heshima katika jamii hata kama mtoto hajakosa pale akionekana kufanya jambo la kawaida kabisa kila mtu atakuwa mwangalifu akidhani ata miss behave kama wazazi wake na ndivyo ilivyo kwa nchi....
   
 11. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Nimeiona hiyo youtube ya huyo Mary ambaye inaelekea ni mjinga mjinga.
  Mtanzania mmoja amenifurahisha hapo kamwita a stupid American.
   
 12. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  red mark! Kama hiyo nia ingelikuwepo mwanzo na watawala wangekuwa na nia njema hakuna ugumu wa kufikia hayo malengo.NA BADO HATUJACHELEWA.Hata Hiyo uchina unayoizungumzia na baadhi ya nchi za asia ya kusini zilizopiga hatua ktk maendeleo ya viwanda, miaka michache iliyopita hali zao za kiuchumi zilikuwa zinafanana tuu na nchi maskini za Afrika ikiwemo TZ.Hiyo ni michango ya wasomi na wataalamu wao wa awali waliosomeshwa kwenye mataifa ya Magharibi na matumizi mazuri ya rasilimali zao. Kama Umekiri uchina wameweza hata TZ wanaweza kufikia huko, Kama TZ itakuwa na nia ya dhati ya kutumia resource zake na hazina ya wataalamu waliosomea fani na ujuzi mbalimbali kutoka vyuo mbalimbali duniani kuyatekeleza hayo yote tungeweza kufika huko. kama tutakuwa na mifumo mizuri ya utawala na Uwajibikaji.Kuepusha Siasa kutafuna Taaluma, Ubinafsi na wizi wa rasilimali! Yanawezekana yote...
   
 13. T

  Tewe JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Umesema kweli. Wakorea, wafaransa, wareno, waarabu, wajapani na wengine wengi hawana issue na kiingereza na mambo yanaenda
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Anza kwa kuacha kutumia maandishi ya Kirumi basi, anzisha maandishi ya Kiswahili, uende kuanzisha na internet ya Kiswahili etc.

  Utopia is good only in the abstract. Try to live it and you will see how quixotic shunning english is.

  Ingawa sikubali utumwa wa mawazo, pia sikubali kwamba inabidi tuwe isolationists ili kuushinda utumwa wa mawazo.

  Ikumbukwe kwamba hawa wanaoongoza chumi za dunia hivi sasa hawajafika hapo kwa kujifungia. Na kwa kweli Mchina bila kujifungia angekuwa mbali zaidi sasa hivi.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kama unakijua Kiswahili kinaasa kuhusu kuiga tembo kunya.

  Hao wote uliowataja wana civilizations zilizonufaika kwa teknolojia, makoloni, mafuta etc. Huwezi kuwaiga kirahisi tu bila ya kufikia level yao ya maendeleo.

  Unataka kumuiga Mkorea na Mjapani mwenzako ana maandishi yake ya maelfu ya miaka, hata akisema aanzishe chake anakiandika kwa maandishi yake.

  Wewe ukikazania sana chako, Kiswahili, hata Kiswahili chenyewe unakiandika kwa Kirumi.

  Let's be reak here.
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Katika habari za "high rent seeking behavior" sie ni wanafunzi tu.

  Watu walikuwa na high rent seeking behavior tangu kwenye biblia huko. Ukisoma/kuona "The Merchant of Venice" mchezo wa Shakespeare utajua nani Shylock aliyetaka ku exact ratili ya nyama ya roho kama rehani.

  Kwa hilo tu hatujawafikia. Ila labda tunaweza kuonekana waroho sana kwa sababu methods zetu za rent seeking ziko crude.

  Huwezi kuniambia tumeipita Wall Street machinery katika hilo.

  Wakati sie tunaongelea kupandisha royalties za uchimbaji wa madini kutoka asilimia 3 kwenda tano, Australia wanaongelea kuongeza kutoka asilimia 25 kwenda 50 huko!

  http://www.theaustralian.com.au/national-affairs/treasury/royalty-hike-puts-mining-in-a-hole-bhp-billitons-jac-nasser/story-fn59nsif-1226473020580
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Uingereza ipi hiyo iliyo hoi kimaendeleo?

   
 18. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Tatizo la watanzania na Tanzania kwa ujumla hususan viongozi na wengi kwenye management kuwadharau watanzania wenzao, hata JK ana hiyo tabia, wanawatukuza wageni pamoja na kujikombakomba sana. Ajira za Watanzania zinaporwa na Kenyans hasa kwenye vivutio ati tu kwa sababu ya lugha. Wanaotaka kuja Tanzania wajifunze kiswahili ni wakati muafaka serikali ilichukulie swala hili kwa umakini na kuwa na wakalimani kila upande na kuwapa ajira Watanzania ambao hiyo kazi wanaiweza. Hawa manyang'au ambao ni makuwadi wa wazungu wanapata kichwa kutoka kwa dhaifu.
   
 19. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nimeshakutana na wachina bongo wanaongea kiswahili kizuri kuliko wanavyoongea kiingereza...sikuamini maskio yangu nilivyowasikia siku hiyo
   
 20. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Kila mtu na mtazamo wake, kwangu mimi kuambiwa kuwa hatujui kingereza huku akikili kuwa tumebobea kwenye kiswahili ni sifa nzuri. kama ilivyo kwake na wazungu wenzake hawajui kiswahili huku wakiwa wamebobea ktk kingereza. Ujinga wetu uko namna hii : mwingereza akiongea kiswahili akachanganya nyakati , viunganishi vibovu na hata matamshi mabaya yenye kupoteza radha ya kiswahli, wa Tz tunamsifu kwa kusema kajitahidi maana kaeleweka. Lakini acha mTz aongee kingereza kwa kuchanganya tenses, kushindwa matamshi, na hata kutumia neno la kingereza mahala pasipo pake, utasikia taanguka na vicheko, kejeli na kusema anatuaibisha hata kama kaeleweka. HUO NI UTUMWA WA FIKRA
   
Loading...