Si kweli kwamba Serikali ya Tanganyika haipo


Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,858
Likes
691
Points
280
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,858 691 280


duni.jpg?w=128&h=85
Na Juma Duni Haji

Mawazo ya jumla waliyonayo ndugu zetu wa Tanganyika ni kwamba Wazanzibari wanafaidika zaidi na Muungano na hivyo malalamiko yao hayana msingi zaidi ya tabia mbaya ya kulialia kwa kisingizo kwamba wao ni wachache na wanatoka katika eneo dogo la Muungano huu. Lakini Juma Duni Haji anaamini kwamba ni kweli Zanzibar inakandamizwa na mfumo wa Muungano uliopo maana “viongozi wa Serikali ya Muungano hawana nia njema na Zanzibar.” Katika makala hii, ambayo ni sehemu ya waraka aliouwasilisha Aprili 26, 2007, kwenye maadhimisho ya 43 ya Muungano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Duni anajenga hoja mpya ya uwepo wa Serikali ya Tanganyika na kuvunja ile dhana kwamba pale mwaka 1964, wakati wa Muungano, Tanganyika ilikufa.

Imekua ni mtindo wa viongozi wa siasa wa Tanganyika kutetea kwa kusema kwamba eti hakuna Serikali ya Tanganyika na hivyo haingewezekana kufanya mazungumzo juu ya mgogoro huu kati ya Serikali hiyo na ile ya Zanzibar. Mimi naamini kwamba hoja hii ni dhaifu. Kila mtu anafahamu kwamba Muungano huu ni kati ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar. Popote penye Muungano, lazima kutakua na washiriki zaidi ya mmoja. Mwalimu Nyerere alisema hayo alipohojiwa na gazeti la Observer la Uingereza tarehe 20 Aprili, 1968:

“If the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the union was prejudicial to their existence, I could not bomb them into submission…The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn.” (Nyerere: London Observer: 1968)

Kwa ufupi, Mwalimu Nyerere alisema kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautokuwepo kama wale walioungana watatoweka au watakuwa hawapo.

Kama Mwalimu ni mtu wa hekima, basi ni vyema kukumbuka yale aliyokuwa akisema na kuandika, kwa hivyo kama hivi sasa hakungekuwa na Serikali ya Tanganyika – na kwa maana ya Mwalimu Nyerere – kungekuwa hakuna Muungano tena tangu hapo aliposema.

Lakini la kujiuliza ni ikiwa kweli Serikali ya Tanganyika haipo na, kama haipo, kaifuta nani na kwa nini. Ukitaka kuelewa hoja hii, ni vyema msomaji akarudia kwenye sheria zilizoamrisha kufutwa kwa serikali hiyo. Makubaliano ya Muungano ya 1964, Kifungu Na. (iv) kinasomeka hivi:

“…and in addition (the Union Parliament) shall have exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika

Hiki ndicho kifungu cha Makubaliano kilichotumika kuanzisha mgongano wa Muungano. Maneno “and in addition” maana yake kwamba Bunge linatekeleza shughuli za mamlaka mbili. Lakini Mwalimu Nyerere akaifanya kuwa mamlaka moja ili ionekane kwamba Bunge la Tanganyika halipo na Rais wa Tanganyika hayupo.

Mara zote tunapotaja Tanganyika, wengi ya wale walio Tanganyika hasa viongozi wa dola na wale wa CCM huwa hawapendi na hutuona sisi kama tunawarejesha nyuma katika ‘kuimarisha’ Muungano. Ukweli ni kwamba jina hilo halipendwi kwa sababu kunafichwa aibu fulani iliyofanyika hapo 1964 ambayo ndiyo kiini cha mgogoro wa Muungano. Katika Makubaliano ya Muungano hakuna kifungu kinachotoa ruhusa kufutwa kwa Serikali ya Tanganyika. Serikali ya Tanganyika imelindwa na kifungu Na.(v) cha Makubaliano hayo kinachosomeka kwamba:

“The existing laws of Tanganyika and Zanzibar remain in force in their respective territories.”
Yaani sheria zilizopo za Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yake (za Zanzibar kwa Zanzibar na za Tanganyika kwa Tanganyika)

Mkataba wa Muungano ndio sheria kuu (grand norm) ya Muungano, kwa upande mmoja, na Katiba ya Tanganyika ya wakati huo ilikuwa ndiyo sheria mama ya Tanganyika. Vyote viwili, Mkataba wa Muungano na Katiba ya Tanganyika havijaagiza kufutwa kwa serikali ya Tanganyika. Kwa hivyo, Katiba hiyo ya Tanganyika inapaswa iwepo na viongozi wa Tanganyika wawepo ili kusimamia mambo ya Tanganyika ambayo si ya Muungano. Na la kujiuliza hapa ili kujiridhisha kwamba kumbe Tanganyika hasa ilikuwepo na imekuwepo ni kwamba kama hakuna Katiba, sheria hizo zingetumikaje katika Tanganyika isiyo Katiba?

Lakini inasikitisha sana kuona baada ya makubaliano hayo Bunge la Tanganyika lililokaa kupitisha sheria ya kukubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa makusudi, lilikubali kuifuta katiba ya Tanganyika na hivyo kuifuta Serikali yenyewe. Maana ukishafuta katiba hizo sheria nyingine za Tanganyika zitasimama kwa katiba ipi? Katika sheria hiyo kifungu chake cha 7 kinasomeka hivi:

“On the commencement of the Interim constitution of the UnitedRepublic, the Constitution of Tanganyika shall cease to have effect for the Government of Tanganyika as a separate part of the UnitedRepublic

Yaani “Mara tu itapoanza kutumika katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katiba ya Tanganyika itasita kutumika kwa ajili ya Serikali ya Tanganyika kama ni sehemu mbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.”

Hili lilifanyika kwa maksudi ili viongozi wa Tanganyika kujipa nafasi ya kujikweza na kuikweza serikali yao iliyojibadili na kuwa ndiyo Serikali ya Muungano. Kwa Kiingereza ni kwamba: The government of Tanganyika underwent metamorphosis to become a Union Government.

Huu ndiyo udanganyifu kwa kutumia kalamu ulivyofanyika hapo 1964. Sheria Na. 22 ya 1964 inayoitwa Union of Tanganyika and Zanzibar Act 1964 ilipitishwa na Bunge la Tanganyika 25/4/64 kabla Muungano kuanza. Wakati huo na siku ile kulikua hakuna Bunge la Muungano maana lililazimika liundwe baada ya sheria hii kupitishwa na wawemo wabunge wasiopunga 32 kutoka Zanzibar (wajumbe wa Baraza la Mapinduzi).

Makubaliano ya Muungano kisheria hayawezi kubadilika au kubadilisha katiba ya Tanganyika. Kufuta katiba ya Tanganyika hakuna uhusiano wowote na Makubaliano yale. Na hata kama katiba hiyo ndiyo iliyotumiwa kuweka Katiba ya Muda ya Muungano, lakini baada ya kufanyiwa mabadiliko ilipatikana katiba ya muda ya Muungano na kuiacha ile ya Tanganyika pekee.

Hakuna mahali katika Makubaliano palipoagiza kufutwa katiba hiyo wala kumuondoa Rais wake wa Tanganyika. Muda wote wa utawala wake, Mwalimu Nyerere alistahiki kuwa Rais wa Tanganyika na Rais wa Jamhuri ya Muungano kama ambavyo Mzee Abeid Karume alivyobaki kuwa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar. Maelezo haya yanaweza kufananishwa na hali ya Rais Kikwete hivi sasa, ambaye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama chake cha CCM hakumfanyi asiwe rais wa Jamhuri, maana hizi ni dhamana mbili tafauti.

Kitendo hiki ndicho kilichotumika kuharibu utaratibu na mfumo mzima wa mwenendo wa uatawala katika shughuli za Muungano kwa miaka 42 sasa. Siku ile ile wafanyakazi wote wa Serikali ya Tanganyika wakawa wafanyakazi wa Muungano, Mahakama ya Tanganyika ikawa ndiyo ya Muungano, na Majaji wake wakawa ndio majaji wa Muungano, muhuri wa Tanganyika nao ukawa ndio Muhuri wa Muungano (Public Seal). Kwa nini udanganyifu huu? Ni kwa sababu ya ukosefu wa nia njema.

Katika sheria ile Na. 22 ya 1964, Rais wa Tanganyika amejipa madaraka ya kutunga kanuni zilizompa uwezo wa kutoa maagizo yanayohusu mambo ya Muungano kwa kutumia decrees za sheria ya Tanganyika. Pamoja na kupewa madaraka hayo na Makubaliano ya Muungano, lakini kanuni hizo zilikuwa zitungwe na Bunge la Muungano siyo Bunge la Tanganyika.

Siku ilipopitishwa sheria hii Na 22 pia zilipitishwa decrees mbili zilizotokana na kifungu Na. 5, 6 (3), na kifungu cha 8 cha sheria hii. Decrees hizo The Provisional Transitional Decree 1964 na ile ya The Interim Constitutional Decrees 1964, zote, hazikua halali maana ni decrees zilizopitishwa na Bunge la Tanganyika zilizotokana na sheria ya Tanganyika.

Kifungu Na 3 (i) cha Provisional Transitional Decree kinasomeka hivi:

“Every person who holds office in the service of Republic of Tanganyika immediately before the Union Day, on union day be deemed to have been elected, appointed or otherwise selected to the corresponding office in the service of the United Republic.”

Yaani “wafanyakazi wote wale waliokua wanafanya kazi katika Serikali ya Tanganyika kabla Muungano watakua wamechaguliwa au kuteuliwa moja kwa moja na kuwa watumishi wa Serikali ya Muungano.”

Mwaka 1993, wabunge wa Tanganyika waliojiita G55 walijaribu kurejesha Serikali ya Tanganyika kwa Azimio la Bunge. Mhe. Njelu Kasaka, mmoja wa viongozi wa kundi hilo, alieleza kwa ufasaha kabisa hoja hii. Amri ya Mwalimu Nyerere, ambaye wakati ule hakuwa mbunge, spika wala rais, ikazuia Azimio la Bunge kutekelezwa. Kama hili ni Bunge la wananchi, kwa nini maamuzi yake yanafutwa na mtu ambaye hana nafasi hiyo kisheria.

Eti sababu ikatolewa kwamba kurejesha Serikali ya Tanganyika ni kinyume na Sera ya Chama cha CCM. Lakini katika Makubaliano ya Muungano, hapana mahala ambapo chama cha ASP au TANU vilishiriki ingawa vilikuwepo wakati Muungano ukiwekwa sahihi. Makubaliano yalikuwa kati ya Rais wa Tanganyika kwa niaba ya Watanganyika na Rais wa Zanzibar kwa niaba ya Wazanzibari.

Kwa hivyo tangu 1964 mara tu baada ya kuwekwa saini makubaliano ya Muungano yamekuwa yakichafuliwa kwa makusudi na kutoa nafasi kwa upande mmoja wa Muungano kujinufaisha chini ya kivuli cha kuimarisha Muungano, huku upande wa pili ukididimia. Prof. Shivji, katika moja ya mihadhara yake juu ya Muungano, anasema hivi:

“One of the essential features of that scheme was and is the distribution of Power between the Union Parliament and the Zanzibar Legislature. That scheme was implicitly made immutable and a fundamental condition of the association of the two states. To tamper with those provisions is the surest way to destroy the legal foundations of the Union. Addition to and subtle alterations of the reserved list on union matters is like hammer-blows delivered to the core of those foundations. The moral and political responsibility of those of us who simply watch the blows is probably greater than those who deliver them.” (Prof. Shivji: 1994: University of Dar es Salaam)

Hapa Prof. Shivji anasema kwamba kuivuruga misingi ya makubaliano bila kuitetea ni sawa na kutizama mtu akipigwa ngumi na wewe unachekelea. Wajibu wa wale wanaoyaona hayo na kunyamaza kimya ni sawa sawa na wa yule anayeyavuruga makubaliano hayo.

Kwa hivyo matatizo ya sasa ya Muungano ni matatizo ya kujitakia yaliyotokana na vitendo vya makusudi vya kijanja dhidi ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964. Serikali ya Tanganyika ilipandishwa daraja na kujifanya ndiyo bwana wa Zanzibar chini ya mtazamo wa Big Brother’s Attitude.

Tabia hii imejenga jeuri kwa wale wasioelewa mwanzo wake na hufika kuthubutu kulinganisha makubaliano haya kama kwamba ni ndoa. Ndio maana wanauliza kwa dharau: “Vipi nyinyi Wazanzibari munauliza uhalali wa baba yenu baada ya miaka 43 ya ndoa?”

Tabia ya ukubwa imejenga himaya na kufika hadi kusahau kwamba zilizoungana ni nchi mbili. Wengi utawasikia wakihoji: “Huwaje watu 1,000,000 wawe na wabunge 50 katika Bunge la Muungano!” Au: “Eti wabunge wanaotoka katika Vitongoji kule Pemba wanataka wawe ndiyo wakuu wa Upinzani Bungeni!” Anasema Mbunge wa Tanganyika tena wa chama cha upinzani. Leo udogo na uchache wa Wazanzibari unaaza kuhojiwa kwamba hauna haki ya kupata kikubwa. Huko si kusahau na kukejeli maamuzi ya Mwalimu Nyerere na Mzee Karume ya kukubali ukweli kwamba wameungana wakijua kabisa kwamba mmoja ni mdogo na mmoja ni mkubwa lakini yote ni mataifa yaliyokua huru?

Hawa wanaosema haya, bado wanakubali kwamba China ina watu milioni 1,500 lakini ina kiti kimoja tu katika Umoja wa mataifa (UN) sawa na Solomon Islands yenye watu laki moja (100,000) tu. Kwamba Ushelisheli na Sudan, ambapo ya kwanza ni ndogo sana na nyengine ni kubwa sana, zote zina kiti kimoja kimoja tu katika Bunge la Afrika. Kwao wao hilo ni sawa, lakini si sawa kwa Zanzibar kuwa na haki sawa na Tanganyika katika Muungano ambao umeunganisha mamlaka mbili huru na kamili na sio ukubwa wa eneo wala wingi wa watu!

Lakini kote huko ni kukosekana kwa nia njema. Ndiko huko huko kulikosababisha kufutwa kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambako nako kumetokana na kiburi hiki cha kujiona Tanganyika ndiyo Tanzania na kwamba kuletwa kwa Mgombea Mwenza katika uchaguzi ni kwa dhamiri ya kuuwa nafasi hiyo ya Rais wa Zanzibar.

Juzi Mhe. Amani Karume ameapishwa kuwa waziri asiye wizara maalum katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Huwaje Rais awe waziri wa Serikali nyingine? Huaje waziri wa Muungano awe waziri bila kuwa mbunge kama alivyo Mhe. Karume? Kwa kupenda madaraka, masikini, naye amekubali hilo.

Kukamilisha nukta hii ya kuwepo au kutokuwepo kwa Tanganyika, ambapo kwa msimamo wetu ni kwamba ipo, nataka nikumbushe jambo moja la muhimu kthibitisha hoja yetu. Hapo mwaka 1964, neno “Jamhuri” lilitafsiriwa kisheria kwa maana kwamba kila lilipo katika katiba ya Tanganyika lisomeke kwa maana ya “Jamhuri ya Muungano.” Lakini neno hili hili lilibadilishwa maana na kutakiwa litafsirike kila penye neno Jamhuri katika katiba na sheria zote zilizopitishwa baada ya Novemba 1972 lijulikane kwa maana yake mpya ambayo ni Jamhuri ya Tanganyika maana hiyo inajumlisha popote pale palipoandikwa Jamhuri ya Muungano. Katika sheria hiyo Na. 30 ya 1972 inasomeka hivi:

“All acts and all Public documents made or issued before or after November 1972 “The Republic means the Republic of Tanganyika and including “United Republic “ (Section 3 of the Interpretation of Laws and General clauses Act 1972 (No. 30 1972)

Hii maana yake ni nini, kisheria? Ni kwamba, hii tuliyonayo si Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika. Sasa, je, tunakosa gani tukisema kwamba dhamiri halisi ilikua ni kuunda Tanganyika mpya yenye jina jipya na mipaka mipya – The UnitedRepublic of Tanganyika?
 
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,315
Likes
736
Points
280
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,315 736 280
Zanzibar kama hawataki muungano basi wapigane kwa nchi wanayoaamini ni yao na inahujumiwa!. Maneno yasiyokuwa na msingi kila siku hayasaidii. Hakuna nchi ya zanzibar wala Tanganyika inayotambuliwa ulimwenguni kuna nchi ya Tanzania.
 
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
30
Points
135
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 30 135
Nimeipenda hii nakala. Japo sikubaliani na kila kitu ina ukweli ndani yake na mtu ana jifunza mengi akisoma hii nakala. Ukweli ni kwamba Watanzania tulio wengi hatujui historia ya nchi yetu kiundani na wala hatuijui katiba yetu. Wengi wetu maoni tuna toa kutokana na aidha hisia binafsi au kutokana na tulicho sikia au kuambiwa na mtu mwingine. Nakala ni ndefu ila nita jitahidi kuichambua haswal pale ninapo on dosari.

Kifungu Na 3 (i) cha Provisional Transitional Decree kinasomeka hivi:

"Every person who holds office in the service of Republic of Tanganyika immediately before the Union Day, on union day be deemed to have been elected, appointed or otherwise selected to the corresponding office in the service of the United Republic."
Ukweli ni kwamba muungano wetu ulikua wa haraka haraka na wala haukua systematic. Ndiyo maana hapa tunaona wafanya kazi wote wa Tanganyika na mali za umma za Tangayika zikawa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini ukweli ni kwamba kwa ajili muungano ulikua wa haraka haraka kuanza kila kitu from scratch isingewezekana. Ndiyo maana hapa unaona ili kusave time and money kilicho kuwa cha Tanganyika kikawa cha Tanzania. Sisemi ilikua sahihi au la ila ndiyo likely scenerio kutokana na maoni yangu.

Hakuna mahali katika Makubaliano palipoagiza kufutwa katiba hiyo wala kumuondoa Rais wake wa Tanganyika. Muda wote wa utawala wake, Mwalimu Nyerere alistahiki kuwa Rais wa Tanganyika na Rais wa Jamhuri ya Muungano
Tukiassume kwamba kweli mamlaka ya Tanganyika haikufa kwa maana hiyo kiuhalisia Mwl. Nyerere alikua ni raisi wa Tanganyika na Tanzania kwa wakati mmoja basi hii dosari pia ime wanufaisha wa Zanzibar. Kutokana na hoja ya Juma Duni Haji basi ina maana raisi yoyote wa Tanzania kutoka Zanzibar pia ni raisi wa Tanganyika na Tanzania kwa wakati mmoja. Kwa hiyo hapa siyo sisi Watanganyika ndiyo tulalamike kuwa Zanzibar wana raisi wao lakini Mzanzibar akiwa raisi basi pia ni raisi wa Tanganyika? Hii inamnufaisha nani?

Hawa wanaosema haya, bado wanakubali kwamba China ina watu milioni 1,500 lakini ina kiti kimoja tu katika Umoja wa mataifa (UN) sawa na Solomon Islands yenye watu laki moja (100,000) tu. Kwamba Ushelisheli na Sudan, ambapo ya kwanza ni ndogo sana na nyengine ni kubwa sana, zote zina kiti kimoja kimoja tu katika Bunge la Afrika. Kwao wao hilo ni sawa, lakini si sawa kwa Zanzibar kuwa na haki sawa na Tanganyika katika Muungano ambao umeunganisha mamlaka mbili huru na kamili na sio ukubwa wa eneo wala wingi wa watu!
Hapa muandishi ana commit a logical fallacy. Uta chukuaje shirika la kimataifa kama UN na AU na kuilinganisha sawa na mamlaka ya nchi? Kwani China na Solomon Islands au Susan na Ushelisheli zimeungana? Hauwezi kulinganisha shirika la kimataifa na mamlaka ya nchi. Kama muandishi ange taka kutoa point ange linganisha nchi mbili zilizo ungana ambapo moja ni ndogo na moja ni kubwa. Huu kidogo ni upotoshaji na ina wezekana ni uelewa mdogo tu wa muandishi.

Ila nakubaliana na muandishi. Serikali ya Tanganyika iliuliwa kiunyemela maana kila kilicho kuwa cha Tanganyika kikawa cha Jamhuri ya Muungano lakini kila cha Zanzibar kikabaki cha Zanzibar. Sasa hapa sijui nani kadhulumiwa. Wazanzibar kama anavyo dai muandishi au Watanganyika?

Kudiscuss hii katiba yetu ya sasa ni kupoteza pumzi. Dawa iliyo baki kwa sasa ni kuunda tu katiba mpya. Katiba ambayo ita kuwa ya wananchi na si mawazo tu ya viongozi wachache. La sivyo tutaendelea kubishana kuhusu muungano pasipo jawabu.
 
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2008
Messages
2,713
Likes
493
Points
180
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2008
2,713 493 180
Zanzibar kama hawataki muungano basi wapigane kwa nchi wanayoaamini ni yao na inahujumiwa!. Maneno yasiyokuwa na msingi kila siku hayasaidii. Hakuna nchi ya zanzibar wala Tanganyika inayotambuliwa ulimwenguni kuna nchi ya Tanzania.
Mkuu usikurupuke kutoa judgement. Hebu soma btwn the lines. Haya ni mageni yenye msaada.
 
takashi

takashi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2009
Messages
909
Likes
1
Points
35
takashi

takashi

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2009
909 1 35
Zanzibar kama hawataki muungano basi wapigane kwa nchi wanayoaamini ni yao na inahujumiwa!. Maneno yasiyokuwa na msingi kila siku hayasaidii. Hakuna nchi ya zanzibar wala Tanganyika inayotambuliwa ulimwenguni kuna nchi ya Tanzania.
Nchi ya Zanzibar ipo na Nchi ya Tanganyika ipo vile vile... kama hupendi kuitwa Mtanganyika hamia Kenya.
 
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
13,259
Likes
2,000
Points
280
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
13,259 2,000 280
MwanaFalsafa 1,

Baada ya wewe kuisoma makala iliyobandikwa hapa na Kakke, unakusudia bado kuimalizia ile mada yako inayohusu Muundo wa Muungano unaoupendelea uwepo nchini? yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tan-Zan-ia)!

Yes, Historia katika Tanzania yetu inafichwa, au inaandikwa kukidhi malengo fulani, haiandikwi kama historical fact!

Wenye kunufaika na kutosikika kwa Tanganyika wanataka Watanganyika waamini kuwa huwezi kuwa na utaifa wa daraja mbili, lakini wamo katika mchakato wa kuruhusu uraia wa nchi mbili. Ninaelewa kuwa mafahali wawili wapiganapo ,ziumiazo ni nyasi. Vile vikundi viwili vinavyotawala Tanganyika na Zanzibar vinapolumbana, (in fact sio kulumbana, wanapocheza mchezo wao wa kuigiza) wanaoumia ni sisi wananchi wa kawaida katika Tanganyika na Zanzibar. Na ndio tunaoishia kutunishiana misuli , wao wanaenjoy life, mbele kwa mbele.

Kwa bahati mbaya wengi wetu huwa tunaingia kwenye mijadala bila ya kuwa na back ground info ya mada.

Lakini nausubiri kwa hamu mchango wako juu ya Muundo wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Ulisema unaumalizia, take as much time as you need to research, no stress, Mkuu.
 
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
30
Points
135
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 30 135
Mkuu Nonda,

Mpango huo ninao sema kila niki taka kutundika mada mtu mwingine ana niwahi na kubandika topic hiyo hiyo na sitaki tujaze jukwaa na mada ambazo zina zingumizia swala moja. Anyway nadhani hata hapa naweza toa dokezo kidogo au pendekezo kuhusu hili swala.

Mimi na advocate scenario mbili ambazo ni aidha muungano uvunjwa kabisa au tuwe na serikali moja ya kitaifa. Labda nizungumzie tu hilo la serikali moja kwa sasa.

Mkuu ukweli ni kwamba ukiwa na serikali mbili kama ilivyo sasa au serikali tatu lazima kuwe na elements za kuna sisi na kuna wao haswa kama serikali hizo zote zita kuwa na mamlaka ya kama nchi huru. Ili kuleta umoja zaidi na Utanzania ni bora tuwe na serikali moja. Ila hili swala la serikali moja Wazanzibar inaelekea wanaliogopa kwa sababu wanaona Zanzibar ita mezwa na kubaki kama mkoa ndani ya jamhuru. Ila kiukweli ni kwamba administratively Zanzibar ni kama mkoa. Hata sasa hivi Zanzibar inaendeshwa kama mkoa sema wame danganyika na kupewa raisi wao na bunge lao. Ila hebu fanya tathmini. Leo hii Shamsi Vua Nahotha ambae alikua waziri kiongozi (kama waziri mkuu) kwa Zanzibar lakini leo hii kapewa uwaziri. Hii inaonyesha relatively speaking viongozi wakuu wa Zanzibar ni kama mawaziri tu.

Ila sijui kwa nini wenzetu wa Zanzibar hawaoni kwamba serikali yao ni gelesha tu ambao theoretically ina individual powers ila practically ni subset ya serikali ya muungano. Wenzetu kuona kiongozi wao kuitwa raisi basi wanadhani kweli Zanzibar ina autonomy. Hawana autonomy yoyote. SMZ exists at the mercy of SMT and that is the fact.

Kwa hiyo mimi mfumo ambao ninge pendekeza ni serikali moja ambayo ni federal system. Katika hii federal system wakuu wa mikoa wana chaguliwa na wananchi na si raisi kama ilivyo sasa. Na haya majimbo si lazima yawe mikoa kama ilivyo sasa. Mikoa kadhaa inaweza ungana na kuwa jimbo moja chini ya gavana mmoja. Majimbo yana weza kabisa yaka zingatia rasilimali ambapo ile mikoa yenye madini yana kuwa under one administrative region ina yale karibu na ziwa yana kuwa under one administraive administrative etc. Zanzibar ina weza nayo kuwa jimbona ikawa hata special administrative region ambao governor wake na wote ndani ya regional government ya Zanzibar lazima wawe Wazanzibar. Lakini watambue kwamba hamna Mzanzibar anaeweza kugombea kwenye any administrative region Tanzania bara kama wakitaka Zanzibar iwe hiyo special administrative region. Ila kwa bara sisi mtu wa region yoyote ana weza kugombea kwenye any region ndani ya Tanzania bara.

Tukija kwenye serikali kuu Bunge lina kuwa na two chambers. House of Representative lita zingatia idadi lakini kwenye Senate kila administrative region ita toa senators wa idadi fulani bila kuangalia population ya hizo regions. Kwa hiyo regions ndogo kama Zanzibar hazita kuwa at a disadvantage yoyote.

Of course hapa nimeandika kiufupi sana na maeneo mengine ili kuelewa zaidi ina hitaji nifafanua zaidi lakini this is the basic of my idea.
 

Forum statistics

Threads 1,238,898
Members 476,226
Posts 29,336,079