Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,459
- 29,153
Wewe unaongea pumba tu, na pengine ndio wale wale waliotapeli au hujui kilichotokea..Naonaga watu wengi sana wanalalamika wameambiwa wafuge sungura na mwisho wa siku wanao wahamasisha wanaingia mitini.
Ufugaji wa Sungura ni kwamba wafugani wameshindwa ku tengeneza demand, wameshindwa kutengeneza soko. Watu wengi hawana utamaduni wa kula nyama ya Sungura na kuna wanao wafananisha na paka.
Sasa kinacho takiwa ni kitengeneza huo utamaduni, inawezekana kabisa kutengeneza utamaduni wa kula Sungura na watu wakawa wanawala tena sana kuliko hata kuku. Shida iko kwa wafugaji wanataka ready Market, hawataki kuumiza vichwa kabisa kutengeneza demand.
Hii nchi imejaa foreigner kibao na wana uramaduni tofauti tofauti then mtu anakuambia hakuna soko? Unazani kuna atakae kufuata shambani kwako anunue? No lazima umshawishi lazima umwambie ni kwa nini anunue nyama ya sungura.
Wafugaji wa sungura tengenezeni demand achaneni kulalamika
Hao waliowauzia Mbegu ya Sungura ndio waliosema watakuja kununua Sunngura wakikua wakubwa, lakini mwishowe wakaingia mitini wasinunue, vipi tena uwatetee?