Si kwamba ufugaji wa Sungura ni utapeli, no ni uwezo wetu wa kuwaza umeisha

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,913
Naonaga watu wengi sana wanalalamika wameambiwa wafuge sungura na mwisho wa siku wanao wahamasisha wanaingia mitini.

Ufugaji wa Sungura ni kwamba wafugani wameshindwa ku tengeneza demand, wameshindwa kutengeneza soko. Watu wengi hawana utamaduni wa kula nyama ya Sungura na kuna wanao wafananisha na paka.

Sasa kinacho takiwa ni kitengeneza huo utamaduni, inawezekana kabisa kutengeneza utamaduni wa kula Sungura na watu wakawa wanawala tena sana kuliko hata kuku. Shida iko kwa wafugaji wanataka ready Market, hawataki kuumiza vichwa kabisa kutengeneza demand.

Hii nchi imejaa foreigner kibao na wana uramaduni tofauti tofauti then mtu anakuambia hakuna soko? Unazani kuna atakae kufuata shambani kwako anunue? No lazima umshawishi lazima umwambie ni kwa nini anunue nyama ya sungura.

Wafugaji wa sungura tengenezeni demand achaneni kulalamika
 
Hio mkuu si ni kazi ya zaida kuzalisha na kutafta wateja kazi bado kutengeneza demand mi naona hio kazi zingefanya departments za kilimo na mifugo kufungua nyanja za biashara na kupromote watu wafanye production pia kufundusha jamii faida n.k kuhusu sungura.
 
Mkuu unazalishaje bidhaa halafu ujui hautauza wapi?Kula mwenyewe basi badala ya kulalamika hakuna masoko
 
Haha mkuu market mpya kama nyama ya sungura ambayo sio tamaduni za watanzania wengi kwny mara nyngi vinahitaji kupromotiwa kwa suport mbalimbali ili hata kurahisisha masoko maana watu wakua aware ndipo watakapo zidi kua na uhitaji mwsho soko litanoga mfano mdogo kuku wa kisasa mwanzo wameingia sokon wengi awakutaka hata kuwasikia lakn sahv ni kitu cha kawaida tu
Mkuu unazalishaje bidhaa halafu ujui hautauza wapi?Kula mwenyewe basi badala ya kulalamika hakuna masoko
 
Mkuu ipo hivi CHASHA FARMING
Inakuja kampuni inakuambia wanasoko la uhakika la sungura kwa bei kubwa sana ila wanataka wafugaji wawasaidie kuzalisha maana wamezidiwa na soko

Wanakupa mchanganuo wao wa biashara na unaona hapa nakua milionea

Unaingia nao mkataba wanakuuzia vifaranga vya sungura kwa bei kubwa
Watakuuzia madawa na chanjo kwa bei kubwa
Watakuuzia chakula lishe kwa bei kubwa
Na watakutoza gharama za ushauri wa kitaalamu

Utafanya haya yote na kuingia gharama kubwa kwasababu katika mkataba wao ndio wauzaji wa kila kitu na wao ndio watakao nunua hao sungura na kuwapeleka huko kwenye soko lililo wazidia(Hapa ndipo wanapo piga hela kuuza bidhaa kwa bei isio halisi na ni lazima ununue kwao)

Utamu unakuja baada ya kuwa umeingia gharama zote hizo kwa matarjio ya mkataba wa kuwauzia wao..jamaa wanaingia mitini unabaki na sungura wako

KAMA KATIKA HILI HAUONI KUNA UTAPELI BASI UNAPASWA KUJITAFAKARI UPEO WAKO WA UFAHAMU MKUU

Hivi nimekwisha danganyika hadi gharama ya sungura mmoja ameisha tumia labda zaidi ya laki moja kwa minajili ya kuja kuuza tuseme laki 2 halafu mnunuzi kapotea
Nawewe unakuja hapa jukwaani unaandika sijatapeliwa hapo na kwamba eti nitafute soko......kumbuka bei halisi ya sungura wala sio hiyo ilikua ni kunihadaa tu ili nione ntapa faida

Sasa kweli ntaweza kumuuzia mtu ambaye anamuona sungura kama paka kwa laki2 kweli jamani?

Yaani nianza kusaka soko kumshawishi mtu asinunue jogoo kwa elfu5 na kumuuzia mtu sungura kwa laki2 ili kucover hela niliotapeliwa ya vifaranga madawa chakula nk

Kumbuka tatizo kubwa la wakulima na wafugaji ni soko, jamaa wamekuhakikishia soko halafu wamesepa unarudi kule kule

Naweka hapo chini aina ya mikataba ya kitapeli
 
Mkuu CHASHA FARMING hii ndio miundo ya mikataba walioiona fursa ya kuwatumia wakulima kwa kujua tatizo letu kubwa ni soko
Wasome hawa na ukivuna hizo pilipili hawana habari na hasara wakati wameisha kuuzia madawa na mbolea yao "maalumu"

*GHARAMA MUHIMU ZA KILIMO CHA MKATABA, ZAO LA PILIPILI KICHAA, NA MAKARU AGRO LIMITED, TANGA, TANZANIA*

*Kilimo hiki kama kampuni ya makaru AGRO limited, cha mkataba tumekianza mwaka juzi (2018) AUGUST, Na kwa sasa tuna wakulima Tanga, Dar, Morogoro, Mbeya, songwe, Moshi Na Arusha, Mwanza, Njombe, Songea, Bukoba Na maeneo mengine*

*Ni baada ya kuanza kuzalisha kisha kama kampuni kutokana na kupata quality nzuri iliyopendwa Na nchi kama Kenya (ambaye ndo tuliingia nae mkataba wa kwanza August 2017), Sudan Na India kuchukua sample Na wakaipenda. Kisha wakaomba mZigo mkubwa zaidi ya tani 5.5-39 kwa Mwezi wakati kama kampun peke yetu hatuwezi kufikisha kutokana na eneo tulilokuwa nao Na changamoto kubwa ya vibarua tuliyokumbana nayo mkoani Tanga*

*Ikawa kama kampuni tunahitajika kuwa Na wakulima wadogo wadogo katika mkoa wowote wenye eneo lenye maji, Na wenye eneo pia lisilotoamisha maji Na wenye kuweza kulipia gharama za kuwapa elimu, Madawa , Mbolea Na mbegu kuwapa ruhusa kwa kuwapa mkataba ili walime kisha tutaenda kununua kwao ili kuweza kufanikisha order hizo kubwa.*

*Kumbuka kilimo hiki cha kimataifa, Mkulima anahitaji kutumia Dawa maalumu tu na sio kila Dawa , hata Mbolea Pia ndo maana mambo haya yoote kama kampuni tukayasimamia ili tuweze kupata kile kinachohitajika, Na tunashukuru tayari kuna wakulima tuliowasimamia wamefanikiwa hayo, so far wengi wanatuuzia na store yetu ipo TANGA MJINI, ambapo mizigo kutoka Kwa wakulima wetu hukusanywa mikoani walipo Kwa gharama zetu mpaka tanga, ambapo hupack Na kusafirisha nje*

*Tumefanikiwa mpaka sasa kuwa Na wakulima japo bado tunahitaji wakulima.*

*Kwa Mkulima yeyote Yule ambaye atapenda kujiunga mlango bado upo wazi kikubwa aangalie gharama Hizi vyema kama ataweza. Kisha utanitafta Kwa ajili ya kuanza Na ukifanikiwa kuanza tu utawekwa pia katika group la wenzio walioanza tayari*

*Awamu ya kwanza:-*

*TUNAITA AWAMU YA UANDAAJI KITALU MAANA UTAPEWA ELIMU YA KITALU*

kuna kuwapo Na gharama hizi:-
1. Mbegu ekari moja 150,000/-
2. Madawa 50,000/-
3. Visits 135,000/-

*Jumla kama 335,000/-*

Hiyo namba 3 itabadilika kutokana Na eneo. Mfano mbeya sio 135,000 ni 290,000/- ila Moshi, Dar, Morogoro, Arusha koote ni hiyo 135,000/-

Kisha tutakutembelea awamu ya kwanza Na vitu vifuatavyo:-
1. Mkataba
2. Kitabu cha kuweka kumbukumbu
3. Kitabu (katasi mbili) cha kumsaidia kufanya revision
4. Mbegu
5. Dawa ya wadudu (mills 100) Kichupa kimoj
6. Dawa ya ukungu, fungal and other infection (1kg).

Awamu ya kwanza Na ya pili inatenganishwa Na siku 30-45

Then awamu ya Pili
Tunaita awamu ya kuhamisha:-
Utalipia gharama Hizi:-
1. Mbolea 2 kg @ 25,000/- 50,000/-
2. Pesticides 500 mills 125,000/-
3. Fungicide 2 kg @25,000/- 50,000/-
4. Visits 135,000/-

*Jumla kama 360,000/-*

Hapo tutakufanyia design ili miche iingie mingi, pamoja Na kutoa elimu ya kuhamisha ikiwa ni pamoja Na kuangalia maendeleo ya kitalu. Na utafunzwa namna ya kuweka kumbukumbu Na kuweka dawa.
Utakuwa free kupata utaalamu kila mara unapohitaji pamoja Na kushare Na wenzako walioanza mwaka jana. Ambao washaanza kuvuna. Tukija tunakuja Na hizo Dawa Na Vitu vyoote ulivyolipia.

Awamu ya pili kwenda ya tatu ni baada Ya siku 30-45 pia

Awamu ya tatu

1. Mbolea 2 kg @ 25,000/- 50,000/-
2. Pesticides 500 mills 125,000/-
3. Fungicide 2 kg @25,000/- 50,000/-
4. Visits 135,000/-

*Jumla kama 360,000/-*
Haina tofauti Na awamu ya pili.
Kwa ufupi Madawa utakuwa ukilipia Na kuchukua kwetu kila yanapokuishia.

Tunaita awamu ya kukausha. Hapa tukija utapata elimu ya namna ya kujenga nyumba ya ukaushaji, Pamoja Na namna ya kuvuna Na kukausha Na kuhifadhi kwa ujumla.

NB:-
*1. KUHUSIANA NA GHARAMA*

*_GHARAMA HIZI ZINAWEZA KUONGEZEKA HASA KATIKA MBOLEA NA MADAWA, MAANA MPIGA DAWA NA MUWEKA MBOLEA NI MKULIMA PEKE YAKE NA ENEO LAKE_*

*2. KUHUSIANA NA MAVUNO*

*_MKULIMA ATAVUNA MFULULULIZO BILA KUPUMZIKA KWA MIAKA MITATU, MAVUNO KWA MWEZI YANAWEZA KUFUATA MAKADIRIO YETU, YANAWEZA KUONGEZEKA ZAIDI AU YAKAPUNGUA KUTOKANA MA WAVUNAJI, HALI YA HEWA, AU SABABU NYINGINE ZA KIMAZINGIRA_*

*KuanZia hapa mwezi wa tatu ndipo utapoanza kuvuna KAMA UNA VIBARUA WA KUTOSHA UNAWEZA KUVUNA KUANZIA KILO 1000 ZILIZOKAUSHWA (Sawa Na kilo 2000 mbichi, sawa na vibarua 10 ndani ya ekari moja kila mmoja kuvuna kilo 10 Mbichi kisha kilo moja unampa kuanzia 285-500/- lNDANI YA MWEZI UTAKUWA NA TANI MOJA ILIYOKAUSHWA AU ZAIDI NA SISI KILO MOJA TUTANUNUA KWA 3500/- UTAPATA 3,500,000/-*

*3. KWA UFUPI IPO NAMNA YA KIPEKEE YA SISI KAMA KAMPUNI KUKUHUDUMIA KIMKATABA, ILI TUWEZE KUNUNUA LAZIMA UKUBALIENI NA KUTEMBELEWA AWAMU TATU NA UFUATE MAELEKEZO YETU PASI NA KUJALI KUWA UNA MTAALAMU WAKO, KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA MKATABA*

*MAVUNO HAYA HATUJAKADIRIA TUNALO SHAMBA NA TUMEONA KWETU*

*Kwa mawasiliano zaidi namna ya kujiunga piga simu hapa*

0652359818
0767359818
*Mwl Abuu*

MAKARU Agro Limited
P. O box 1805,
Tanga,
Tanzania

*Endapo yoote yaliyopo hapo juu umeyaelewa Tuma ujumbe kukiri umeelewa Na upo tayari kuanza, utapata invoice ya awamu ya kwanza,utayolipia ndani ya siku mbili, kwa ajili ya mbegu, madawa, Na kutembelewa Na baadhi ya document muhimu*

*NJOO ULIME NA WANAOLIMA PIA KWA GHARAMA NAFUU NA SOKO LA UHAKIKA, ACHANA NA MADALALI*
 
Naonaga watu wengi sana wanalalamika wameambiwa wafuge sungura na mwisho wa siku wanao wahamasisha wanaingia mitini.

Ufugaji wa Sungura ni kwamba wafugani wameshindwa ku tengeneza demand, wameshindwa kutengeneza soko. Watu wengi hawana utamaduni wa kula nyama ya Sungura na kuna wanao wafananisha na paka.

Sasa kinacho takiwa ni kitengeneza huo utamaduni, inawezekana kabisa kutengeneza utamaduni wa kula Sungura na watu wakawa wanawala tena sana kuliko hata kuku. Shida iko kwa wafugaji wanataka ready Market, hawataki kuumiza vichwa kabisa kutengeneza demand.

Hii nchi imejaa foreigner kibao na wana uramaduni tofauti tofauti then mtu anakuambia hakuna soko? Unazani kuna atakae kufuata shambani kwako anunue? No lazima umshawishi lazima umwambie ni kwa nini anunue nyama ya sungura.

Wafugaji wa sungura tengenezeni demand achaneni kulalamika
Nenda ubenani mkuu. Uzuri wa wabena hawajafuta akili ya wakoloni wazungu na warabu eti kuchaguliwa chakula,huo ujinga hawajaufuata hivyo ukifuga chochote chenye nyama wao ni chakula.Hao sungura peleka Ubena utauza wataisha wala huitaji promo watajipromo wenyewe.
 
Mkuu ipo hivi CHASHA FARMING
Inakuja kampuni inakuambia wanasoko la uhakika la sungura kwa bei kubwa sana ila wanataka wafugaji wawasaidie kuzalisha maana wamezidiwa na soko
Wanakupa mchanganuo wao wa biashara na unaona hapa nakua milionea

Unaingia nao mkataba wanakuuzia vifaranga vya sungura kwa bei kubwa
Watakuuzia madawa na chanjo kwa bei kubwa
Watakuuzia chakula lishe kwa bei kubwa
Na watakutoza gharama za ushauri wa kitaalamu
Utafanya haya yote na kuingia gharama kubwa kwasababu katika mkataba wao ndio wauzaji wa kila kitu na wao ndio watakao nunua hao sungura na kuwapeleka huko kwenye soko lililo wazidia(Hapa ndipo wanapo piga hela kuuza bidhaa kwa bei isio halisi na ni lazima ununue kwao)

Utamu unakuja baada ya kuwa umeingia gharama zote hizo kwa matarjio ya mkataba wa kuwauzia wao..jamaa wanaingia mitini unabaki na sungura wako

KAMA KATIKA HILI HAUONI KUNA UTAPELI BASI UNAPASWA KUJITAFAKARI UPEO WAKO WA UFAHAMU MKUU

Hivi nimekwisha danganyika hadi gharama ya sungura mmoja ameisha tumia labda zaidi ya laki moja kwa minajili ya kuja kuuza tuseme laki 2 halafu mnunuzi kapotea
Nawewe unakuja hapa jukwaani unaandika sijatapeliwa hapo na kwamba eti nitafute soko......kumbuka bei halisi ya sungura wala sio hiyo ilikua ni kunihadaa tu ili nione ntapa faida

Sasa kweli ntaweza kumuuzia mtu ambaye anamuona sungura kama paka kwa laki2 kweli jamani?
Yaani nianza kusaka soko kumshawishi mtu asinunue jogoo kwa elfu5 na kumuuzia mtu sungura kwa laki2 ili kucover hela niliotapeliwa ya vifaranga madawa chakula nk
Kumbuka tatizo kubwa la wakulima na wafugaji ni soko, jamaa wamekuhakikishia soko halafu wamesepa unarudi kule kule

Naweka hapo chini aina ya mikataba ya kitapeli
Ni ujinga kushawishiwa kitu kisicho halisi.Yaani jogoo ni elf 30000 wewe uambiwe laki3.Were mi zoba was kutupwa.
Kuna bata wanawaita bata bukini ukienda Ktk maonesho ya nane huwauza 100000.Mimi huwa nawashangaa wanaowanunu.Najiuliza hao bata wanataga dhahabu!
 
Mkuu hii dunia wajinga hawatakuja kuisha..
 
Nazungumzia Sungura nyama, swala la Bata bukini na hao wengine huko siko na by the way wale huwa ni Ornament Birds, au ndege wa mapambo mkuu sio wa kwa ajili ya kula,

Na pia Kwenye Maonyesho nikupe siri, ukiina kitu kinauzwa ghari sana jua anaue uza hataki kinunuliwe na labda anauo hicho tu so njoa pekeee ni ku hike price
Ni ujinga kushawishiwa kitu kisicho halisi.Yaani jogoo ni elf 30000 wewe uambiwe laki3.Were mi zoba was kutupwa.
Kuna bata wanawaita bata bukini ukienda Ktk maonesho ya nane huwauza 100000.Mimi huwa nawashangaa wanaowanunu.Najiuliza hao bata wanataga dhahabu!
 
Kwa nini unaingiza Tangazo lako sehemu ambayo sio? Ai nifichue usanii wa hizi vilimo? Make najua in and out usaniii huu na jinsi upigaji ulivyo. Mayu,
 
Kwa nini unaingiza Tangazo lako sehemu ambayo sio? Ai nifichue usanii wa hizi vilimo? Make najua in and out usaniii huu na jinsi upigaji ulivyo.
Umesoma lakini mabandiko yangu hapo juu au umekimbilia kujibu mkuu

Huo mkataba si kampuni yangu bali ni kampuni ya kitapeli inayotapeli watu kama walivyofanya kwenye sungura

Ufugaji wa sungura ulipoingia kampuni zilikuja na mikataba kama huo unao uona hapo juu

Naomba rudi usome bandiko langu No 10 na kisha angalia na huo mkataba kisha nishawishi niamini ni wafugaji ndio wameshindwa kubuni soko na sio wameingizwa mkenge
 
Mkuu MAYU, mie ni mhusika mkuu wa Makaru AGRO Limited, na wengine Pia watakuja very soon. Tunaomba udhihirishe mkuu wangu wapi tumemtapeli mkulima. Itapendeza ukaweka namba yake na mkataba wake na sisi. Sina account JAMII FORUM ila wakulima wangu ambao wanavuna Na kuutuuzia pilipil ndo wamenitumia maelekezo haya. Tafadhali mkuu THIBITISHA KAULI YAKO. Otherwise kwa wataopenda kutufuatilia muone kazi zetu lakini pia chukuen mawasiliano yangu niwape wakulima mkoa wowote uliopo mkawatembelee kujiridhisha. Nimesikitika sana Mayu kutuita matapeli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom