Si kila Mtanzania ni kichwa cha panzi. We have made progress under Magufuli (For sure more needs to be done)

''Bongolander'' yapo mambo unajichanganya sana. Umetueleza uwepo wa ''tangible outcome'' katika TAMISEMI. Halafu unasema huna takwimu za ku-back up hoja zako
Baada ya hapo unatueleza yapo maendeleo katika maji, umeme, shule na zahanati
You're all over the place!!

Pili, kuna kitu hukielewi kuhusu demokrasia. Unaitazama demokrasia kwa mtazamo mfupi.
Demokrasia imeelezwa vema na watu wa political science
Demokrasia si uchaguzi ! Ni mfumo ambao uchaguzi ni mchakato ndani yake

Demokrasia ina tafsiri pana sana lakini kwa ufupi inahusu kushirikisha watu katika maamuzi yanayowahusu, kufuata utawala wa sheria na muhimu zaidi ni kulinda haki za Raia

Tatu, dhana kwamba demokrasia imetoka magharibi si kweli, ni ufupi tu wa mawazo au kujifunza hasa kwa kuangalia historia yetu.

Machifu na Watemi walikuwa na mifumo ya demokrasia,kuanzia utawala, kushirikisha watu, kuwa na mambaraza ya maamuzi na kutoa haki kwa mtindo wa sheria.

Kilichotokea ni ku-modernize na ndipo unajichanganyikiwa ukidhani ni kitu kipya

Viongozi wasiotaka demokrasia siku zote hukerwa na element mbili za demokrasia ambazo ni utawala wa sheria na haki za watu

Labda nikuulize hivi akina Mwalimu Nyerere na waliofuata unaaminisha hawakuona haja ya maendeleo? Na kwanini basi walikubali kubeba dhana zote mbili, demokrasia na maendeleo!
Walikuwa wajinga! hawakuwa na ufahamu! au hawakuwa na maono!
 
''Bongolander'' yapo mambo unajichanganya sana. Umetueleza uwepo wa ''tangible outcome'' katika TAMISEMI. Halafu unasema huna takwimu za ku-back up hoja zako
Baada ya hapo unatueleza yapo maendeleo katika maji, umeme, shule na zahanati
You're all over the place!!

Mkuu Nguruvi3 nakuelewa vizuri. Kilichopo ni kuwa sijapata takwimu concrete, sikutaka kuleta kitu ambacho hakijatimia. Ninachotaka kusema ni kuwa kuna kazi nzuri ambayo binafsi naifurahia kutoka TAMISEMI, kwamba inagusa maisha ya watu, yaani maendeleo ya kutoka hatua moja kwenda ya pili (sio yale ya kuzuga watu). Shule kujengwa zikiwa zimeborshwa, zahanati na vituo vya afya kujengwa zikiwa na improvement, my meaning ni kuwa baadhi ya huduma za jamii kwa umma zinaonekana kupewa kipaumbele kiasi na zinafika kwa umma ndio maana nimesema maji, umeme, shule na zahanati. To me these are tangible, nikita na concrete stats ya idadi ya shule, health centres zilizojengwa kwa katika miaka hii mitatu ntaziweka hapa. Nikiwa na stats za ongzeko la idadi ya yatu wanaotumia umeme na kupata maji ya uhakika pia ntaweka. I really do care about this.

Nilifikiri kwa kutoa mifano hiyo unaweza kupata undani wangu kuwa ni nini nakijali zaidi, baada ya kuwa frustrated na demokrasia tunayodanganywa kila siku. Nimekuwa naona kama ni mchezo wa wanasiasa kupata wanachotaka, na sisi kura washangiliaji wakati hatuna umeme, maji, shule, hospitali...

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa viongozi waliotangulia walitoa kipaumbele kwa vyote maendeleo na demokrasia, walikuwa na busara. Hakuna ubaya wa kutoa kipaumbele kwa vote. Lakini pia nataka tuangalie facts. What do facts tell us, they tells us Democracy to us is just fantasy. Chaguzi tunafanya kupoteza hela na muda, kwa kuwa matokeo yanakuwa predetermined long before election. So why waste our money and our time? Kuwafurahishwa watu wa magharibi? or just to have the label that we are a "democratic" country? Just look at mchezo wa kilichoitwa mkutano wa katiba, how much time and money have we wasted? Zile hela zingetumika kujenga shule au hospitali, leo tungekuwa na kitu tangible. All what we have now is "we had a democratic process". My point here, is ideas and facts do not match.

Kimsingi nakubali kuwa demokrasia ni jambo la muhimu, ni muhimu sana. Ni kweli kuwa haiishii kwenye chaguzi tu, ni ushiriki wa watu kwenye mambo yote yanayowahusu. CCM siku zote inajitahidi kusema viwili vinaenda pamoja, lakini angalia uhalisia wa nchi yetu tangu wakati wa uhuru. Demokrasia iko limited kwa wanasiasa tu, ndio maana unaona wahandisi, madaktari, wasanii etc wanaacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa.

I
 
Tujaribu kuangalia ni nini kilikuwepo before JPM, na sasa tukoje. Miaka minne iliyopita sio mbali sana. Kuna ukweli kuwa baada ya hela za dawa za kulevya kuondolewa mitaani, na baada ya hela za ufisadi kupungua sana mitaani, hali iko tofauti. Ndio maana baadhi ya watu wanasema bora wakati wa JK maana hela ilikuwa nje nje, lakini tunasahau kuwa ile hela ilikuwa chafu. Kumbukeni kuwa Eddo alikimbizwa U-PM kutokana na uozo wa madili ya ajabu, Mh Pinda alikuwa kwenye hati hati sababu kasi yake ya kudeal na mambo yanayogusa kutatua taabu za wananchi ilikuwa ndogo. Licha ya changamoto zilizopo sasa mambo yamebadilika sana.

Our country was in verge of becoming a banana republic, we averted that. So we need to do better than throwing cheap shots.


Mkuu unamanisha wafanyakazi wa serekali nchi hii walikuwa mafisadi au wauza madawa?
 
"Bongolander, post: 31908412, member: 3997"]Nilifikiri kwa kutoa mifano hiyo unaweza kupata undani wangu kuwa ni nini nakijali zaidi, baada ya kuwa frustrated na demokrasia tunayodanganywa kila siku.
Hivi unapataje watu wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kama si kwa njia ya demokrasia? Tunadanganywa na nani kuhusu demokrasia?
Demokrasia ni kitu kigeni nchini?
Nimekuwa naona kama ni mchezo wa wanasiasa kupata wanachotaka, na sisi kura washangiliaji wakati hatuna umeme, maji, shule, hospitali...
Hapa unalaumu uwepo wa bunduki.

Sidhani Bunduki na mabomu ni tatizo. Tatizo ni jinsi watu wanavyotumia vitu hivyo.

Badala ya kutumia bunduki responsibly watu wanatumia kushambuliana katika hadhara
Badala ya kutumia mabomu kulipua miamba ya madini na njia za usafiri, watu wanalipuana

Kwa nchi nyingine demokrasia nakuwa practiced bila tatizo hata kidogo
Hatuwezi kusema sasa ndio mwisho wa demokrasia , kwa kigezo na utaratibu gani
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa viongozi waliotangulia walitoa kipaumbele kwa vyote maendeleo na demokrasia, walikuwa na busara.
Halafu soma hapa chini unavyojichanganya .
What do facts tell us, they tells us Democracy to us is just fantasy.
!!
Chaguzi tunafanya kupoteza hela na muda, kwa kuwa matokeo yanakuwa predetermined long before election. So why waste our money and our time? Kuwafurahishwa watu wa magharibi? or just to have the label that we are a "democratic" country?
Sijui kama unafuatilia mjadala, demokrasia si uchaguzi ndugu yetu!!.

Uchaguzi ni moja ya element za demokrasia, nyingine ni utawala bora na haki za binadamu.

Unapokataa demokrasia kwa maneno mengine unakataa rule of law and human rights.

Demokrasia ndiyo inatupa ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo yao

Bila demokrasia unaishia kuwa na utawala la kiimla.
Sifa ya utawala la kiimla ni kuamua mambo na kuya impose kwa watu wake.

Hilo ndilo linazaa neno IMLA ambalo kwa kiingereza ''dictate''
Mtu anaye dictate ni Dictator. Labda utusaidia mfumo upi utakuwa mbadala wa demokrasia
Just look at mchezo wa kilichoitwa mkutano wa katiba, how much time and money have we wasted? Zile hela zingetumika kujenga shule au hospitali, leo tungekuwa na kitu tangible. All what we have now is "we had a democratic process". My point here, is ideas and facts do not match.
Katiba haikuwa na tatizo hata kidogo.

Tatizo ni CCM waliokataa maoni ya wananchi wakihofia katiba mpya kuwa mwiba kwao

Hivyo hakuna uhusiano kati ya demokrasia na uhuni wa CCM ambao wewe hutaki kuusema

Kwa taarifa yako,CCM walioko madarakani ndio walikuwa ndani ya Bunge la katiba

Ni nani miongoni mwao alifikiri kuwa mchakato ule ulikuwa wa ujinga na kusema!!
Bongolander: Kimsingi nakubali kuwa demokrasia ni jambo la muhimu, ni muhimu sana.
halafu
Bongolander :Nimekuwa naona kama ni mchezo wa wanasiasa kupata wanachotaka, na sisi kura washangiliaji wakati hatuna umeme, maji, shule, hospitali..
anamalizia
Bongolander: democracy to us is just fantasy
!!!

I'm out, good luck
 
Mkuu unamanisha wafanyakazi wa serekali nchi hii walikuwa mafisadi au wauza madawa?

Hapana mkuu sio maana yangu. Ila maana yangu ni kuwa vitendo hivyo vilishamiri sana kiasi kwamba vilifikia hatua ya kufanya tuwe na uchumi wa ajabu sana. Ndio maana unaona serikali ya JPM ilijua kabisa kuyachekea mambo haya ni kuitia kitanzi jamii ya Tanzania na kuhatarisha usalama wa nchi.
 
Nguruvi3, Mag3 takwimu nilizopata zinaonesha kuwa tangu mwaka 1961 hadi mwaka 2015, tulikuwa tumejenga vituo vya afya +200 na tangu JPM aingine madarakani kupitia TAMISEMI vimejengwa vingine +200. (Suala la ubora tuweke pembeni) Kwenye upande wa elimu (shule ya msingi), Katika miaka mitatu iliyopita enrollment imeongezeka kwa zaidi ya 100 kwa wakazi wa mijini.

Wizara ya maji wamejitahidi sana kwenye usambazaji wa maji, nadhani kwa sisi wakazi wa Dar tunaweza kuona improvement kwa kiasi kikubwa.

Wizara ya nishati wamejitahidi kwenye umeme kupita REA, sasa hivi vijiji zaidi ya 7000 vina umeme. (Juhudi zilianza awamu ya nne). Nadhani JPM amepunguza gharama na kuwa rahisi sana kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

Kwenye suala la Stigler nadhani katika siku za karibuni huu ni mradi ambao naweza kusema ni wa maana sana na ni wa kimkakati, japokuwa kuna watu wanaukosoa lakini tukiangalia nchi zite zilizoendelea, before maendelea walikuwa na mradi au miradi mikubwa ya umeme.

Tukiangaza kuangalia haya yamefika vipi hatua hii, vtunaweza kuwa na mjadala mkubwa ambao utakuwa na wakosoaji wa njia iliyotumika, na waungaji mkono wa njia iliyotumika. Lakini mwisho wa siku tumepata hivyo.
 
Mkuu hizo paragraph zako za mwisho zime ni shangaza na kunisikitisha sana

Mkubwa, unajua kuna mahali tukubali kuwa we are damn when we do, and damned when we do not. Sasa kwa maoni yangu ni bora tuwe damned tukiwa na kitu kuliko kutokuwa na kitu. Hali halisi ni vigumu sana kubadilikwa kwa mazingira ya sasa. Usije kudhani mimi nasema kwa furaha. Mara nyingi huwa nasikitika sana. Kuna siku niliuliza watu zaidi ya 60 kuhusu katika wengine walisema wamewahi kuisikia, lakini hawajui umuhimu wake ni nini, na wengi hata ukiwauliza kama wanajua demokrasia ni nini na kama wanajali, ukisikiliza majibu utacheka sana.
Unaweza kuona kuwa reality ni tofauti sana na tunachokitamani kiwe. nadhani kazi yetu kubwa ingekuwa ni kuwaelimisha watanzania wote maana ya demokrasia na wajibu wao kwa taifa. Watakapaomka wengi, then i would go for that path. Otherwise, i will still be skeptical.
 
Tuna phobia ya FIKRA NGUMU, na huo ndio MTEGO wetu.
Amani ya nchi imekuwa excuse ya kila mvutia kwake.

Katiba ni MBOVU, yaani hai-guarantee moja kwa moja Ustawi wa Umma hata ikifuatwa kiukamilifu 100%. Hilo sidhani kama kuna ambaye hakubaliani nalo.

IKIWA WAPO WAKIUKAO KATIBA ILI KULINDA MATUMBO YAO, U WAPI UBATILI WA KUKIUKA KATIBA ILI KULINDA MASLAHI YA UMMA? TENA AMBAYO TUNAKUBALIANA KUWA NI DHAIFU!

MTEGO WA FORMALTIES NI MGUMU MNO KWA MTU MWEUSI.

KATIBA SAHIHI ni Mantiki iliyoko kati ya Nyakati na Mazingira ya eneo husika.
Walituhadaa wakidai wanafuata Katiba, tusisahau hilo.


Muhimu ni Mfumo Mpya, lakini lazima tutambue haupaswi kufanywa kuwa Msaafu. Na tutambue pia kuwa, si jambo sawa na kubadilisha mke. KUSUKA MFUMO SAHIHI NI HESABU NDEFU.

Mungu wetu yupo Kazini tayari, Afrika.
 
Mkuu watu wengi wanafikiri kuwa mwarobaini wa matatizo yetu yako kwenye katiba mpya. lakini ukiangalia kwa undani utaona kuwa tatizo ni kubwa kuliko katiba. Tuangalie mfano wa Kenya na Afrika Kusini, utaona kuwa wameacha kuaddress matatizo ya kweli, wamevamia matatizo ya kufikirika au yale mepesi mepesi. It is too professorial and unrealistic to think that it is all about the Constitution..

Kwa Tanzania ningesema kwanza tuitekeleze kikamilifu katiba ya sasa. Tuiheshimu vilivyo na kuona weaknesses. Hapo hoja ndio itakuwa inaeleweka. Kwa sasa hivi tatizo kubwa liko kwenye mentalities, sio kwenye katiba.

Ni sawa na mtu anayepambana na maji yasiyo ya mvua yaliyojaa hadi magotini kwa kujifunika mwamvuli. Sioni kama hiyo ni njia sahihi, ya kutumia approach ya kujikinga kwa mwamvuli wakati maji yanatoka chini.
 
Ndio Maana nimemuomba Definition ya Banana republic, Maana nionavyo mimi hiko hapo juu ndio BABA Republic yenyewe na sasa tupo kwenye hiyo kitu.
 
Bongolander
Unaweza kunisaidia Definition ya Banana republic au Characteristics za banana republic ?

Mkubwa kama ukiangalia toka mwanzo nimesema kuwa "more needs to be done". Bado hatuko perfect lakini ukiangalia ni nini tulikilalamikia sana huko nyuma, tunaweza kuona kuwa serikali ya sasa imejibu yaleee tuliyokuwa tunayachukia.

"Jamhuri ya ndizi ni ka nchi ambako viongozi wake ni wezi, kanatawaliwa na kionmgozi ambaye amenunualiwa na wafanyabiashara, wababe wa vyombo vya usalama na wanasiasa wenye sauti. Na kunakuwa na kundi la matajiri na wenye fedha maifsadi ndio wanaoamua mwelekeo wa uchumi kwa manufaa yao"

Hizo ni baadhi tu ya sifa za jamhuri ya ndizi, ikiwa ni pamoja na kutegemea chanzo kimoja cha mapato kwa uchumi wake. Ukiangalia Tanzania ya sasa bila shaka bado ina changamoto nyingi sana, lakini hizo nilizotaja hapo zimepungua sana, kwa hiyo si jamhuri ya ndizi. Najua pia kuwa tunalima ndizi.
 
Mkubwa kama ukiangalia toka mwanzo nimesema kuwa "more needs to be done". Bado hatuko perfect lakini ukiangalia ni nini tulikilalamikia sana huko nyuma, tunaweza kuona kuwa serikali ya sasa imejibu yaleee tuliyokuwa tunayachukia.

"Jamhuri ya ndizi ni ka nchi ambako viongozi wake ni wezi, kanatawaliwa na kionmgozi ambaye amenunualiwa na wafanyabiashara, wababe wa vyombo vya usalama na wanasiasa wenye sauti. Na kunakuwa na kundi la matajiri na wenye fedha maifsadi ndio wanaoamua mwelekeo wa uchumi kwa manufaa yao"

Hizo ni baadhi tu ya sifa za jamhuri ya ndizi, ikiwa ni pamoja na kutegemea chanzo kimoja cha mapato kwa uchumi wake. Ukiangalia Tanzania ya sasa bila shaka bado ina changamoto nyingi sana, lakini hizo nilizotaja hapo zimepungua sana, kwa hiyo si jamhuri ya ndizi. Najua pia kuwa tunalima ndizi.

Bongolander

Shukrani GT.

Ila nionavyo mimi ulichokiandika ni kilekile kinachoenelea sasa nchi hii au wewe huoni au hutaki kudadisi?

Ngoja nikusaidie na wewe utanisaidia kama nimekosea:-

1."Jamhuri ya ndizi ni ka nchi ambako viongozi wake ni wezi,- Kwenye hili Mkuu inasemekana tumeibiwa maTRilioni ya Kodi zetu kw amuijibu w aripoti ya CAG

2.kanatawaliwa na kionmgozi ambaye amenunualiwa na wafanyabiashara, - Hili Mfano mzuri ni kinahoendelea Moa wa DAR wewe hali unaionaje toka list ya Madawa mpaka kuwa ndio marafiki wa mwana mpendwa? unataka kusema baba hausiki?


3.wababe wa vyombo vya usalama na wanasiasa wenye sauti. -- Hapa kuna la kuhoji? Mafno mzuri ni wasio julikana naamini wajua hilo.

4.Na kunakuwa na kundi la matajiri na wenye fedha maifsadi ndio wanaoamua mwelekeo wa uchumi kwa manufaa yao"
Hili ndugu sijuhi ila tender nyingi zinazoendelas nchi hii zina harufu ya hili.
 
Mkuu kusema kweli sifahamu lolote kuhusu hizo trilion. Lakini naweza kuwa nina imani kuwa fedha hizo hazijaibiwa. Inawezekana zimetumiwa na serikali kwa manufaa ya nchi kinyume na taratibu za kihasibu. Lakini kusema kuwa serikali ya Magufuli imeiba pesa hizo, kidogo ninapata shida kuamini. Lakini naweza kuwa na wewe kuwa kama CAG alisema hazijulikani zimeenda wapi...basi kuna mahali zimeenda. Mifukoni mwa watu? Serikali ya Magufuli???? Vigumu kuamini.

So kwa Tanzania tafisiri ya viongozi nadhani iko kwenye watu chini ya 10. Are they thiefs? Kwa kweli siamini hata kidogo. Angalia top leaders 10 wa awamu ya JPM, tuseme yupi ni mwizi, ameiba nini ameweka wapi. Siamini kama kuna mmoja kati ya top ten ni mwizi.

Mkuu Jamhuri ya ndizi demokrasia ya kufanya ujinga ipo sana, lakini uwajibikaji kwa taifa ni 0. Lakin i ya uwajibikaji unategemea msimu wa ndizi tu. Ili waweze kuuza ndizi. Zikiuzwa tu, mambo holela.

Mkuu kama tukitaka kuikosoa serikali ya JPM tuweke nondo za kweli. Wewe uinajua kuwa jamaa wa serikali wanasoma kila siku hapa. Sasa tukianza kuandika ukosoaji hewa, watapuuza hata kama tukiwa na ukosoaji makini.

Kumbuka ukosoaji kwenye issue ya dawa za kulevbya. Ulikuwa very genuine, na haikupita muda tukasikia JPM ameteua mtu competent kwenye issue hiyo. Kwa hiyo tunaweza kuweka mawazo yetu na yakasikilizwa.
 
JPMi ni kiongozi mzuri ingawa siyo politician au economist mzuri. Anachofanya inaitwa a bitter pill that heals. Unfortunately mtoto akizaliwa huwa haanzi kukimbia papo hapo; itachukua miaka kabla ya watu kuona matunda ya juhudi hizo. Inaweza kuwa ni muda ambapo JPM hatakuwa madarakani tena.

Politicians wametuuza sana, so we can say that we are better without them for now. Wengine hata hatujui what they stand for. Sasa tukiangalia nchi letu naona linasonga, japo kama unavyosema mkuu itachukua muda kuona matunda, at least dalili ziko wazi kabisa. Hata JPM akimaliza muda wake, for a very long time we will see his marks.
 
Tatizo la Watanzania wengi ni chuki binafsi walizokuwa nazo kwa JPM. Wengi walitegemea angeshindwa kuongoza na kwenda kupiga magoti DC au London ili aweze kubebwa. JPM kitu alichofanya ni kuamini kwamba Tanzania ni nchi tajiri ambayo haina sababu yoyote ya kwenda kupiga magoti huko kwa wale ambao wamejenga culture ya kuabudiwa na kujiona wao ni bora zaidi kuliko binadamu mwingine yeyote.

JPM alianza kwa kuangalia BOT inavyofanya kazi zake na kuhakikisha kwamba hakuna mwanya wa wizi vile vile kuhakikisha hakuna wizi au mbinu kwenye financial sectors zote. Unakumbuka jinsi maduka ya Forex yaivyokuwa yamejaa kama utitiri na kufanya biashara zao kutumia Serikali. Baada ya kuziba nyufa ndio akaanza kupata pesa za kufanya mavitu ambayo Tanzania kwa miaka nenda ilikuwa haiwezi kufanya pamoja na kutumbua tumbua wazembe. Tanzania tupo vizuri sana na nidhamu ya kazi imerudi, sina wasi wasi na JPM atakapoacha urais wake tutakuwa tupo kwenye anga zingine kiuchumi na kimaendeleo. Kujenga nchi hakuchukui miaka mitano au kumi etc kujenga nchi ni kuweka misingi thabiti ambayo itawezesha ngazi kujengwa kufika kileleni. Every step counts, make your part.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom