Si kila Mtanzania ni kichwa cha panzi. We have made progress under Magufuli (For sure more needs to be done)

Kwa hiyo mwenye mawazo tofauti na hoja ya kuwa tumepiga hatua kimaendeleo chini ya JPM ni KICHWA PANZI?

Hapana mwenye mawazo tafauti sio kichwa cha panzi, ni halali kuwa na mawazo tofauti na kukosoa. Mkubwa naomba unielewe vizuri. Hoja yangu kuu ni kuwa we have made some progress, tofauti na wanaosema kuwa mambo mabaya. Nakubali kuwa kuna matatizo, hata mimi nayaona na naweza kuyataja, lakini pia naona baadhi ya mambo ambayo nilikuwa mkosoaji mkubwa wa awamu iliyopita yamefanyiwa kazi. Kwa hiyo kusema hakuna lililofanyika sio sahihi kabisa.

Mawazo tofauti ni halali, lakini yawe na facts. Kupinga ni halali lakini kule na basis.
 
"Bongolander, post: 31861380, member: 3997"]
Mimi sioni kama ni vibaya kumkosoa Magufuli.
Hata yeye mwenyewe huwa anajikosoa, na pale anapoona amekosea anajaribu kubadilisha.
Tupe mfano mmoja ili wote tusome ukurasa ule ule ''same page''
Uongozi wa kufuata sheria na unaoheshimu katiba kweli unafaa sana, kama haufanyi usanii. Nadhani wengi tunapenda tufike huko, ambako bado hatuajafika. Iwe ni sababu ya kuwa na mashaka na katiba yenyewe, au iwe ni sababu ya mianya ndani ya katiba, au kukosa muundo imara wa kulinda na kutetea katiba. Tatizo langu mimi kwenye issue hii ni kuwa, kuna wale ambao wanatumia katiba kutuibia au kutufanya tuwe duni, na wengine wanatumia katiba kwa maslahi binafasi na sio maslahi makuu ya taifa.
Katiba inayotoa fursa ya kuiba, kutufanya tuwe duni, kutumika kwa masilahi binafsi siyo katiba inayofaa.

Ironically, katiba inatakiwa ilinde umma dhidi ya mambo hayo.
Suluhu si kuiacha ibaki kama katiba ili tuonekane tuna katiba.

Fikra hizo ndiyo ' real kichwa cha panzi''.
Una kidonda mguuni badala ya kutafuta tiba unakiacha kioze kwasababu tu upo bize kupanda mnazi ili upate madafu. Hapo ndipo ''kichwa cha panzi 'kilipo.

Suluhu ni kukaa chini na kutengeneza katiba inayokwendana na wakati , matakwa na mahitaji ya nyakati. Hapa unaunga mkono hoja yangu kuwa hatuna mwelekeo kwasababu hatuna mwongozo ambao ni KATIBA.
Hapa ni wote wana CCM na wapinzani.
Mkuu unaonekana kuwa obsessed sana na Wapinzani.

Hivi kweli unaweza ku-equate wapinzani na chama tawala!

Hawa wapinzani hawajawahi kutawala nchi hii hata kwa masaa machache, wapi unapata ushahidi wa kusema wanatumia katiba kutuibia, kutifanya tuwe duni na kwa masilahi yao?

Kwanini unatafuta balance hata kwa jambo lilowazi kama hili!

Hebu nionyeshe ni kwa namna gani Wapinzani wametumia katiba kutuibia, kutufanya tuwe duni au kwa masilahi yao. Kuna uwezekano kabisa lipo jambo nisilo lijua. Tafadhali tusaidi
Lakini kuna wengine ambao ndio nawalaani zaidi, wanapenda kujionyesha (kwa nchi za magharibi) kuwa wanafuata katiba lakini gharama yake kwa taifa ni kubwa, ni kama tunagharamia mchezo wao.
Kama tunatumia katiba kufanya uchaguzi, kupata viongozi, kuwaapisha viongozi na kuunda serikali kuna ubaya gani kuonyesha kuwa sisi ni nchi yenye kufuata katiba tuliyo nayo?

Kwangu mimi binafasi maendeleo ni kitu cha kwanza na cha msingi kabisa.
Hili nalirudia kila mara.

Watanzania hawaelewi kabisa kuwa Maendeleo si kontena la bidhaa linalotengenezwa au kuagizwa kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Maendeleo ni mchakato wa fikra na matendo.
Huwezi kuwa na maendeleo bila mawazo na kama huwezi kuyafanyia kazi mawazo hayo.

Lakini si hivyo tu, mawazo ya kufanyia kazi yanahitaji nidhamu.
Nidhamu si kibuyu cha pombe ya ndaza, ni utaratibu maalumu unaotoa fursa kimpangilio.

Hivyo nidhamu lazima iambatane na sheria ambayo chimbuko lake ni mkusanyiko wa mawazo na mipango katika mfumo wa katiba.

Kitu cha kwanza hakiwezi kuwa maendeleo, lakini matokeo ya mpangilio wa fira, matendo na nidhamu ndiyo unazaa kitu kiitwacho maendeleo
MImi binafsi kutokana na kiwango cha maendeleo ya nchi, nisingependa kitu chochote kinizuie kuleta maendeleo ya nchi, iwe katiba, iwe chama au hali yoyote.
Katiba inayokupa haki ya kuleta maendeleo inawezaje kuwa kikwazo tena? I mean hapa sielewi kabisa
Lakini nachukia watu wanaojaribu kutumainisha kuwa JPM anavunja katiba as if Mwalimu, Mzee Ruksa, Mkapa na JK hawakufanya hivyo. Ukiangalia kuna cases nyingi tu ziliwahi hata kufikishwa mahakani kuhusu ukiukaji wa katiba. That is not the issue for Tanzanians. Issue kwa sasa ni maendeleo.
Maana ya uongozi, ni kupanga, kuonyesha na kufanya yaliyo bora.

Mkuu utetezi kuwa Mwl, AH, BWM walifanya abcd hivyo ni halali kufanya tu ni mawazo hafifu na ya hatari sana na sijui kama kuna mtu mwingine anaweza kukuelewa,SIJUI

Huwezi kulinganisha ubaya kwa ubaya hata siku moja.usisahau kipimo cha uzuri ni ubaya.

Sasa kama unalinganisha ubaya na ubaya uzuri utaupata wapi?

Tena ukimlinganisha Mwalimu na viongozi wote waliofuata , Mwl ana advantage kubwa sana

Mwalimu hakuwa na template, kila kitu kilikuwa cha kwanza na kigeni

Sasa kiongozi akiwa na template halafu akafanya sawa au vibaya kuliko Mwl, unatueleza nini?
 
good is never enough where better is possible. .

Mkubwa umeweka rondo nyingi sana hapa. Nimependa mawazo yako na ukaripiaji wako. Ni kweli Good is never enough, wherever better is possible let us go for the better one. Kissing ninachoona kwenye post yako ni kuwa tulenge juu zaidi, tupige hatta zaidi. Hili ni jambo zuri.

Lakini ukumbuke kuwa kuna matatizo mengi sana kwenye nchi yetu. We must start somewhere, or we have to have something to start with. Hili swali hata hapa kwenye jukwaa la great thinkers hatuwezi kuwa na jibu moja. Let us appreciate the mess JPM inherited. Ni kwenye jukwaa hili hili tulikuwa tunaonyesha hasira zetu. Lakini hata JPM hawezi kuondoa matatizo yooote ni one or two terms.

Issue ya katiba ni ngumu sana, ukumbuke kuwa ni moja ya misingi muhimu ya Tanzania yetu. Naweza kusema katiba ina mianya mingi sana ya kufanya ufisadi, kama kuna kiongozi fisadi. Kwa hiyo inategemea will ya aliye madarakani. Hakuna mahali inaposema inaruhusu ufisadi, lakini bado ina mianya inayoruhusu allocation of funds ambazo wananchi inawezekana tusipende. Kwa hiyo kweli katiba ina tatizo. Lakini ni tatizo kubwa kuliko umaskini? Ni kipaumbele kwa sasa kati ya changamoto za Tanzania? ... Kuna mtu yoyote anaruhusiwa kuvunja katiba? NO NO NO. Kumekuwa na vitendo via ukiukaji wa katiba ya nchi? za vyama? YES YES YES. Ni jambo zuri? NO NO NO. Hili ni jambo linalojadilika kabisa.

Mkubwa unajua kuna kukosoa, kukejeli na kutukana. Sasa watu wakijikita kukejeli na kutukana, inakuwa vigumu kujua wana lengo gani. Au mtu anaanza kuwa na ideas zinazofanya nchi yetu iwe vulnerable kwa unyonyaji na kutugawa, kidogo inakuwa vigumu kuelewa kama anakosoa au anahatarisha.

Jambo moja ninaloona kuwa wote tunakubali kuwa tunahitaji maendeleo.
 
Mkuu Mag3 karibu katika maendeleo. Nimeanza mbali na Bw ''Bongolander'' nikimkokota taratibu . Kuna mambo ya msingi ya mjadala anakwepa kuyajadili
Yale anayo yajadili ukisoma 'between the lines' utaona yana UTETEZI kwa kuuma na kupulizia

Leo anatuambia Wapinzani wanatumia katiba kutuibia, kutufanya tuwe duni na kwa masilahi yao
Unaweza kuona jinsi hoja zinavypindishwa ili kuwahukumu Wapinzani ambao hata kwa dakika moja hawajaapa au kutawala taifa hili.

Kitisho ni pale asipoamini uwepo wa katiba na kutoelewa dhana ya maendeleo

Hivi kwanini Watanzania wanaamini maendeleo ni kama gunia la ubuyu unaloweza kulisafirisha kutoka Uyui kwenda Ubungo? Hakuna kitu kinachoitwa kuleta maendeleo! kutoka wapi!

Nilijaribu kumtahadharisha katika bandiko moja kuwa kosa linalofanywa na CCM ya leo ni kutuma watu mitandaoni wasiojua kujenga, kubomoa au kutetea hoja

Nilimpa mfano wa issue ya kupunguza gharama ilivyogeuzwa na kupoteza maana yake ya asili
 
Ntaendelea kusisitiza kuwa Katiba sio perfect, ina weaknesses nyingi tu. Kuna udhaifu kwee kuitekeleza, kuilinca na hata kuielewa. Hili sikatai, lakini licha ya halo, sioni busara tukiendelea kujikita kwenye tatizo hilo tu. Na tukipiga usité wa mtatizo yetu kama nchi, hili sio zito sana.

Mkuu hiyo ya "real kichwa cha panzi" made my day. ..... Maana yako ni kuwa msingi uko kwenye katiba, kama tukiweka mambo sawa huko, kwingine tutaendelea vizuri. Kwenye hiyo point una mantiki nzuri, hapa napenda tukubali kutofautiana. Ningependa hii issue ya katiba tu deal nayo balaye. Ila naomba minazi yangu iote haraka, kabla kidogo hakijaoza.

Ila naomba uelewe moja mkuu, mwanasiasa ni yuleyule. Awe CCM au Mpinzani. Wapinzani wakiingia madarakani watakuwa CCM, na CCM wasipokuwa madarakani watakuwa wapinzani. So wapinzani are no angels, au CCM hatubadilika kuwa angles kama tukiwa upinzani. Sipendi kuiangalia nchi yetu kwa hadbini ya vyama, napenda tuangalie mbali zaidi ya hapo. You have to remember that A MAN IS A POLITICAL ANIMAL and will show his true colors once he is in power.

Unajua hakuna kiongozi aliye Malaika, not in Tanzania not anywhere. Hata Mwalimu aliwahi kusema utawala wake ulikuwa na mazuri na madhaifu yake, alichukia watu walioiga mabaya. Issue ni kuwa kiongozi anatakiwa kuhakikisha gari anayoendesha inakwenda mbele.
 
Issue ya katiba ni ngumu sana, ukumbuke kuwa ni moja ya misingi muhimu ya Tanzania yetu. Naweza kusema katiba ina mianya mingi sana ya kufanya ufisadi, kama kuna kiongozi fisadi. Kwa hiyo inategemea will ya aliye madarakani.
Mkuu, sasa hapa si ulisema Wapinzani wanaitumia kutuibia, masilahi binafsi na kufisadi?
Lini Wapinzani waliwahi kuwa madarakani na kutumia mianya ya katiba?
Unaona tatizo la kujaribu kutafuta justifications kwa ku balance story. Hapa ni wazi unaji contradict
Hakuna mahali inaposema inaruhusu ufisadi, lakini bado ina mianya inayoruhusu allocation of funds ambazo wananchi inawezekana tusipende.
Katiba haina kifungu kinachozungumzia allocation ya fund. Hakuna.

Katiba hii hii ya 1977 na ubovu wake haina kifungu hata kimoja.
Katiba ina vifungu vinavyoeleza mgawanyo wa kazi na hapa Bunge
Bunge ndilo linaloidhinisha matumizi ''allocation ya fund''

Mkubwa unapotuambia katiba yetu ina allocate fund, unatukatisha tamaa kwakweli
Labda nikupe benefit of doubts, nionyeshe kifungu cha katiba kinachoeleza allocation ya fund

Tunaelewa hoja yako, kwamba, hakuna sababu za kuhoji matumizi ya serikali kama wanavyofanya wapinzani.

Tunakuelewa vema umelenga nini na utetezi wako umeegemea wapi, lakini hatukuelewi ni kusingizia katiba ! Hapa hueleweki kabisa
Au mtu anaanza kuwa na ideas zinazofanya nchi yetu iwe vulnerable kwa unyonyaji na kutugawa, kidogo inakuwa vigumu kuelewa kama anakosoa au anahatarisha.
Mkuu tuwe vulnerable kwa unyonyaji kutoka wapi na kwa vipi.

Nadhani hapa unaongelea hoja yako ya wale wanaotumia nchi za magharibi kuzungumzia katiba. Kuhusu kuwa vulnerable nadhani pia ile 'chuki' ya watu ulioisema inaingia.

Tunaomba utufahamishe, ni akina nani wanatufanya tuwe vulnerable?

Kuhusu kuligawa taifa, tafadhali hii hoja iachie hapa! tafadhali iache maana huwezi kuitetea. Hatuwezi kugawanyika zaidi ya tulivyo leo
Jambo moja ninaloona kuwa wote tunakubali kuwa tunahitaji maendeleo.
Hapana hapa sikubaliani nawe kabisa.

Hatuhitaji maendeleo kwasababu moja kubwa
Maendeleo ni tukio la maisha ya mwanadamu kila uchao iwe katika familia, kaya au taifa
Maendeleo si hitaji ni ulazimu wa asili, ni mchakato endelevu, hauna chaguo hata siku moja

Hakuna siku katika taifa hili tulisema hatuhitaji maendeleo na kwamba sasa ndio wakati
Maendeleo.

Narudia ni takwa la maisha halihitaji kukubaliana wala kuelezwa, linatokea iwe iwavyo.

Tunachohitaji ni misingi imara ya kuyafanya maendeleo yawe bora.

Tufuate taratibu tulizojiwekea, tuheshimu utu wa watu, na tuwe pamoja kama taifa kufikia malengo yetu

Usijaribu kutuaminisha kuwa sasa ndio msimu wa maendeleo!

Tumekuwa na maendeleo kuanzia mkoloni hadi sasa .
Ni mchakato wa maisha na ni kitu endelevu
 
Nguruvi3, Mag3 naelewa sana hoja zenu. Sio kama nauma na kupuliza. Issue hapa ni kweli kabisa kuwa Katiba ni tatizo. Lakaini mimi siamini kuwa hata tukiwa na katiba mpya, iwe nzuri kama ya India itatatua matatizo yetu. Mimi sina imani sana na wanasiasa wa CCM na hata wa upinzani, most of politicians are driven by personal interest. Ndio maana siamini kama wapinzani ni malaika, ni wale wale tu. Uzuri ni kwamba ndani ya CCM tumeweza kuona kuna mafisadi kwa kuwa wako madarakani, lakini hata wapinzani wakiwa madarakani tutaona true colours.

Mimi sikubaliani na watu wanaoingia mtandaoni kutetea ujinga, au kukejeli wengine bila kuwa na hoja. Mimi issue yangu kubwa ni kuwa siwezi kuchelewesha maendeleo eti kwa sababu katiba mbovu, au usimamizi wa katiba ni mbovu. Let us do other things first wakati tunaweka vichwa vyetu sawa kuhusu katiba. Nikiangalia mfano wa Kenya au hata Afrika Kusine, naona kama katiba mpya imewazuga watu, the status quo is same as it was before new constitution. So the whole debate around Constitution to me is just white noise. Hapana ntaendelea kupa tofauti na wewe hadi kesho, lakini argument yako naielewa vizuri kabisa, and it is very genuine and natural.
 
Kimsingi naona wote tunataka maendeleo, wewe unataka maendeleo bora, lakini mimi nikizingatia hali halisi ya siasa zetu, naona kwa dakika hii ni bora maendeleo. Kimsingi nina hasira sana na tatu waliopoteza na kula hela zetu kwenye issue ya katiba, ambayo matokeo yake ni 0. Zile hela zingeenda kwenye maendeleo labda zingekuwa na matoneo tangible.

Ok let us look at this and try to see make a sense of it. The government has the authority to raise wages of government employees, and it is the parliament which has to give the government a go ahead if it wishes to do so. Otherwise watumishi wataendelea kubebembeleza sana. Angalia wabunge.... wakitaka marupurupu zaidi wanakaa wao wenyewe na kuamua kujiongezea as they wish. They will tell the government we need this increment and if not, then we will give you the hardest time in the parliament. And when it comes to voting, all will vote YAY.... (wa chama tawala na wapinzani) Wana mamlaka ya kikatiba kufanya hivyo... How do you explain this? Kwanini tusimwambie Mufti na Askofu mkuu ndio waamue mishahara yao?
 
Ok let us look at this and try to see make a sense of it. The government has the authority to raise wages of government employees, and it is the parliament which has to give the government a go ahead if it wishes to do so. Otherwise watumishi wataendelea kubebembeleza sana. Angalia wabunge.... wakitaka marupurupu zaidi wanakaa wao wenyewe na kuamua kujiongezea as they wish. They will tell the government we need this increment and if not, then we will give you the hardest time in the parliament. And when it comes to voting, all will vote YAY.... (wa chama tawala na wapinzani) Wana mamlaka ya kikatiba kufanya hivyo... How do you explain this? Kwanini tusimwambie Mufti na Askofu mkuu ndio waamue mishahara yao?
Bado hujajibu hoja. Wapi kufungu ndani ya katiba kinacho allocate fund kiasi kwamba katiba inakuwa dude baya sana hata kulizungumzia ?
 
Bado hujajibu hoja. Wapi kufungu ndani ya katiba kinacho allocate fund kiasi kwamba katiba inakuwa dude baya sana hata kulizungumzia ?
Katiba haina kifungu kinacho elekeza namna ya kuallocate fund. I accept kuwa sijieleza vizuri. Nilichokuwa nasema ni kuwa baadhi ya taasisi zetu zimekuwa na mamlaka ya kujiamulia mambo kwa maslahi ya taasisi au watumishi wake. Kitu ambacho naona kina utata kidogo.
 
Bado hujajibu hoja. Wapi kufungu ndani ya katiba kinacho allocate fund kiasi kwamba katiba inakuwa dude baya sana hata kulizungumzia ?
Mkuu Nguruvi3, siyo kwamba sikutaka kuingilia huu mnakasha awali, hapana, nilikuwa bado najaribu kumwelewa huyu Bongolander...kwa nini aanzishe mada yenye maudhui kama alivyofanya...eti; Si kila mtanzania ni kichwa cha panzi - we have made progress under JPM (For sure more needs to be done.

Mwanzoni niliposoma hicho kichwa cha habari sikutaka kabisa kushiriki kwa maana kwamba kama unaoga mtoni akaja kichaa akakwapua nguo zako na wewe bila takafuri ukatoka mtoni na kuanza kumfukuza, watazamaji hawataweza kujua tofauti kati ya hawa vichaa wawili wanaokimbizana wakiwa watupu!

Mpaka dakika hii bado natafakari Bongolander alitaka kufikisha ujumbe gani lakini natoka kapa au ni kwa sababu mimi ni kichwa panzi! Wapinzani hawajawahi kuwa madarakani ndani ya taifa hili lakini Bongolander yuko tayari kuwabebesha lawama na kuwahukumu kwa matatizo yaliyosababishwa na CCM akidai wote ni binadamu, nanukuu;
Mimi sina imani sana na wanasiasa wa CCM na hata wa upinzani, most of politicians are driven by personal interest. Ndio maana siamini kama wapinzani ni malaika, ni wale wale tu. Uzuri ni kwamba ndani ya CCM tumeweza kuona kuna mafisadi kwa kuwa wako madarakani, lakini hata wapinzani wakiwa madarakani tutaona true colours.
Akichoka kuwabebesha lawama wapinzani anarukia katiba, anaibebesha Katiba lawama na kuihukumu kwa matatizo yaliyosababishwa na CCM kwamba Katiba si lolote si chochote, nanukuu;
Mimi issue yangu kubwa ni kuwa siwezi kuchelewesha maendeleo eti kwa sababu katiba mbovu, au usimamizi wa katiba ni mbovu. Let us do other things first wakati tunaweka vichwa vyetu sawa kuhusu katiba. So the whole debate around Constitution to me is just white noise. Hapana nitaendelea kuwa tofauti na wewe hadi kesho, lakini argument yako naielewa vizuri kabisa, and it is very genuine and natural.
Mkuu Nguruvi3, tatizo la nchi hii kiini chake ni watu kama Bongolander na kwa bahati mbaya wametamalaki wakiamini wanajua kumbe hakuna chochote wanachojua.

Wanataka kujenga nyumba bila msingi imara wakiamini kujenga msingi imara si muhimu kutachelewesha ujenzi! Tunaopiga kelele kudai msingi imara tunaitwa vichwa panzi!

Wako usukani barabarani wakiendesha gari lililojaza abiria lakini wanaona kufuata sheria za barabarani kutawachelewesha kufika huku tunaowapigia kelele tukiitwa vichwa panzi!

Kwa leo naishia hapo...
 
"Mag3, post: 31879147, member: 10873"]
Mkuu Nguruvi3,'' Si kila mtanzania ni kichwa cha panzi - we have made progress under JPM (For sure more needs to be done''

Mpaka dakika hii bado natafakari Bongolander alitaka kufikisha ujumbe gani lakini natoka kapa au ni kwa sababu mimi ni kichwa panzi! Wapinzani hawajawahi kuwa madarakani ndani ya taifa hili lakini Bongolander yuko tayari kuwabebesha lawama na kuwahukumu kwa matatizo yaliyosababishwa na CCM akidai wote ni binadamu, nanukuu;
Mkuu ukimsoma vizuri lengo lake ni 'kupiga debe' si maendeleo bali watu

Mwenzetu anatuaminisha matatizo ya nchi hii yanatokana na Wapinzani

Amefika mahali pa kusema '' wapinzani wanatumia katiba kuiba, masilahi binafsi na kufisadi''

Hapa ana maana nzuri tu, anachotaka ni kujenga narrative vichwani mwa watu wawachukie

Lengo kuu ni kuhalalisha hatua zote zinazochukuliwa dhidi ya Wapinzani bila kujali chochote

Lengo la pili ni kuhalalisha mambo hata yaliyokinyume na sheria.
Anajenga narrative kuwa hatuhitaji katiba, wala Bunge. Kuna mahali kasema
'' watu wanatumia katiba kufisadi na kuiba, na kwamba taasisi kama Bunge si muhimu fedha zinaweza kupangwa na watu nje ya mfumo''

Lengo lake ni kuwaamisha watu hatuhitaji taasisi kama Bunge, fedha na kodi zao zinaweza kutumika vyovyote ili mradi maendeleo

Katika kuhakikisha anafikia lengo, ''Bongolander'' anawafanya Wapinzani wawe sawa na CCM ili kuweza kuficha uchafu wa CCM kwa ku-balance.
Ndivyo pia anavyowatumia akina Nyerere, BWM, AHM n.k.

Ukitaka kujua ana malengo fulani, kaleta hoja kuwa kuna ''tangible outcome'' zinazoonekana TAMISEMI, siyo mahali pengine!!!

Nimemuuliza atuwekee hapa tujadili hakuweza kutetea hata mstari mmoja.

Hii maana yake ''alipewa'' maagizo bila kuuliza details sasa hajui details zake
tatizo la nchi hii kiini chake ni watu kama Bongolander na kwa bahati mbaya wametamalaki wakiamini wanajua kumbe hakuna chochote wanachojua.
Nilimtahadharisha awali kabisa, kwamba, hili wimbi la CCM kutuma vijana mitandaoni bila kujua wanawatuma nini na wao kutojua wanatumwa nini ni jambo la hatari sana
Wanataka kujenga nyumba bila msingi imara wakiamini kujenga msingi imara si muhimu kutachelewesha ujenzi! Tunaopiga kelele kudai msingi imara tunaitwa vichwa panzi!
Ningeshauri arejee mabandiko yote na hoja zake zilivyobomolewa kwa hoja kisha abadili kichwa cha habari.

Wasomaji watachanganyikiwa nini na ni nani hasa kichwa cha panzi
 
Swali na mwisho uliloniuliza kama naweza kusema ni swali gumu kwangu. "Kukiuka katiba kwa nia nzuri??" MImi binafsi kutokana na kiwango cha maendeleo ya nchi, nisingependa kitu chochote kinizuie kuleta maendeleo ya nchi, iwe katiba, iwe chama au hali yoyote. Kipaumbele ni Maendeleo. Lakini nachukia watu wanaojaribu kutumainisha kuwa JPM anavunja katiba as if Mwalimu, Mzee Ruksa, Mkapa na JK hawakufanya hivyo. Ukiangalia kuna cases nyingi tu ziliwahi hata kufikishwa mahakani kuhusu ukiukaji wa katiba. That is not the issue for Tanzanians. Issue kwa sasa ni maendeleo.
Haya ni maneno ya hatari mno kutoka kwa Great Thinker🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️

Kwamba somehow ama kwa bahati mbaya au makusudi unashindwa kutambua umuhimu wa katiba na utawala wa sheria katika suala zima la ustawi na maendeleo ya nchi! Kwamba bora tupate maendeleo hata kama inatugharimu utawala wa katiba na sheria vitu ambavyo tukivichezea vinaweza kuleta athari kubwa kwenye amani ya nchi!

Na mbaya zaidi unatumia kisingizio cha Mwalimu, Mzee Ruksa, Mkapa na JK kuwa kwa kuwa nao walivunja katiba basi hata sasa tuendelee njia hiyo hiyo ili mradi tupate maendeleo?

Mnataka kutupeleka wapi jamani??

Nimechoka kabisa!🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️
 
Wakubwa labda nijaribu kujiweka wazi zaidi. Kwanza ninapoingalia Tanzania siiangalii kwa jicho la vyama, au siangalii kwa jicho la mtu. Naangalia nchi kwa ujumla, maana maendeleo ni ya nchi, sio ya mtu au ya vyama. Pili, tukiangalia hali iliyopo Tanzania kwa sasa, hakuna mtu anayeweza kusema upinzani unawajibika kwa changamoto zilizopo ... simply ni kuwa haujawahi kuwa madarakani, huwezi kumlaumu dereva kuangusha gari ambalo hakuendesha. Kwa hiyo naomba msinielewe vibaya kuwa nawalaumu wapinzani. Mzizi wa mismanament ya nchi uko CCM, i believe JPM na Bashiru are working hard on it. Tunamsikia Dk Bashiru mara kwa mara akilia na hilo. Kwa hiyo sio haki kuelekeza lawama kwa upinzani.

Lakini nawalaani wapinzani wanaojaribu kusema kuwa nothing has been done in these three years of JPM administration, simply because watu wanamchukia JPM kwa sababu zao. Nawalaani vilevile wanaCCM wanaojaribu kutuamisha kuwa kila kitu shwari wakati matatizo bado yapo na wote tunaendelea kuyaona. Naomba mlielewe hili.

Nikijaribu kujiweka kitaaluma naweza kusema nhapa ni kupima uwiano wa njia za kwenda kwenye maendeleo. Kwa mstaarabu anaweza kusema njia ya demokrasia ndio inatufikisha kwenye maendeleo. Nadharia nyingi vitabuni zinatueleza hivyo. Lakini mimi nina mashaka sana na njia hiyo, kwa sababu Tanzania haijaleta matokeo hayo. Awamu ya JK ilipoingia madarakani miaka mitano ya kwanza, ilikuwa na mandate ya asilimia +80 ya watanzania, uchaguzi uliowangiza madarakani ulikuwa wa kidemokrasia. Tell me what we got out of it...what did Tanzania get out of that! Wapinzani walitusaidia sana watanzania kwa kututoa tongo tongo.

Mag3 kwanza sioni dalili yoyote ya wewe kuwa kichwa cha panzi. Ukosoaji wako na hoja zako zimekaa vizuri sana, hata tunapokuwa tofauti, zinanielimisha. Cha msingi ambacho hapa nasema ni kuwa hili eneo linaloitwa Tanzania, lazima lisonge mbele. Let us try to look at this in a holistic manner, not atomistic. Labda mimi natumia darubini tofauti na nyie.

Unaposema kuwa "naamini najua kumbe sijui" inawezekana ni kweli. Ndio maana niko hapa jukwaani kubadilisha maoni na thinkers. I may believe that my thoughts are right, it may as well be very possible that yours are correct and better than mine. We have made progress, that is what i said. And i said that based on where we came from. Kama hakuna lolote ninalojua, na nchi inarudi nyuma na sio kwenda mbele, basi nakubali kuamshwa na kufundishwa.,
 
Kwa mstaarabu anaweza kusema njia ya demokrasia ndio inatufikisha kwenye maendeleo. Nadharia nyingi vitabuni zinatueleza hivyo. Lakini mimi nina mashaka sana na njia hiyo, kwa sababu Tanzania haijaleta matokeo hayo. Awamu ya JK ilipoingia madarakani miaka mitano ya kwanza, ilikuwa na mandate ya asilimia +80 ya watanzania, uchaguzi uliowangiza madarakani ulikuwa wa kidemokrasia. Tell me what we got out of it...what did Tanzania get out of that! Wapinzani walitusaidia sana watanzania kwa kututoa tongo
Bongolander, naomba unisaidie kidogo kwa kunielimisha unakoitoa hii dhana ya awamu zilizopita kuwa za kidemokrasia! Je utawala wa Kikwete ulikuwa wa kidemokrasia? Je utawala wa Mkapa ulikuwa wa kidemokrasia? Kama tawala hizo zilikuwa za kidemokrasia kama unavyojaribu kudai basi na huu ni wa kidemokrasia, sawa?

Hebu soma thread hii iliyowahi kuanzishwa na gwiji Mzee Mwanakijiji akipinga utawala wa kidikteta wa Rais Jakaya Mrisho Kiwete...

Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo"

Ndugu yetu siku hizi anakubaliana na kila analotenda Magufuli...naomba ninukuu kidogo baadhi ya maneno ya Mzee Mwanakijiji.

Mzee Mwanakijiji...
Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

Uhuru wa imani - Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.


Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
 
Haya ni maneno ya hatari mno kutoka kwa Great Thinker🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️

Kwamba somehow ama kwa bahati mbaya au makusudi unashindwa kutambua umuhimu wa katiba na utawala wa sheria katika suala zima la ustawi na maendeleo ya nchi! Kwamba bora tupate maendeleo hata kama inatugharimu utawala wa katiba na sheria vitu ambavyo tukivichezea vinaweza kuleta athari kubwa kwenye amani ya nchi!
Huyu bwana sina uhakika kama anafuatilia habari za dunia nyingine.
Somalia walijaribu kutokuwa na utawala wa sheria na wa kikatiba. Kila Bwana alikuwa na eneo lake akiwaletea maendeleo Watwana wake.

Somalia ni tofauti kidogo na nchi kama Tanzania. Wananchi wake wana Koo tofauti lakini wote wanazungumza lugha moja, Kisomali. Ndivyo ilivyo pia katika dini kwamba asilimia zaidi ya 98 ni wa dini moja.

Baada ya kuisigina katiba, kutofuata utawala wa sheria nchi ipo katika ''anarchy' kwa miaka zaidi ya 30. Maendeleo tunayo yaona ni yale ya kulipuana kila uchao.

Huwezi kuongelea maendeleo kama huna amani. Amani inapatikana kukiwa na nidhamu
Nidhamu haipatikana kama hakuna haki. Haki haitendekei kama haikuanishwa kisheria na kukubalika. Hapa ndipo kuna chimbuko la katiba linalojenga utawala wa sheria, kuleta nidhamu, kujenga amani na kuleta maendeleo

Haiwezekani 'kanyaga twende' kwasababu tu tunataka kile bongolander anachosema '' Bora maendeleo'' Ni jambo zuri kwa muda lenye matatizo makubwa kwa muda mrefu
 
Mkuu haya yote ni kweli; na hayajabadilika. Rais hatoi uhuru wowote kama zawadi au hisani. Siyo Magufuli wala siyo Kikwete. Haki watu huzaliwa wakiwa nazo; siyo hisani ya serikali. Mbona hili liko wazi. Kwenye maneno meusi hapo unanilisha maneno na unanidhania. Sijaegesha akili yangu mwenyewe nikaondoka. Nitaweza vipi kukubaliana na "kila analofanya" mtu..?
 
Mkuu Nguruvi3

Nimejaribu kutafuta takwimu za miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na TAMISEMI kama vile shule na zahanati, nimeshindwa kuzipata kwa ukamilifu, ziko sketchy. Kama kuna reliable sources ningeomba jamvi hili linisiaide kutafuta. Hilo ndio eneo moja ambalo naona tumesonga mbele, na maendeleo kuleta maana ya huduma na progress, sio takwimu tu za kusema uchumi wa Tanzania unakua kwa aslimia 7 wakati asilimia ya watanzania wanaotumia maji ya bomba inapungua kwa asilimia 7 kila mwaka. Kwa sasa kidogo kwenye huduma ya maji naona kuna mwelekeo unaoridhisha, umeme nako kuna mwelekeo wa kutuia moyo, afya kidogo hata aspirini na panadol sio tatizo tena. Ningefurahi sana na ntamsifu sana JPM kama siku anaondoka Ikulu asilimia 80 ya watanzania tuwe na umeme, maji na access ya huduma za afya zenye staha.

I am a big supporter of democracy and human rights, i would like all of us to enjoy them. But at the same time i hate when i see politicians use and abuse democracy for their political and economic gains. I choose to be realist on this, not idealist. What Mzee mwanakijiji says, ni kweli kabisa uhuru si zawadi au hisani. Look at the reality, mtu anakuja kujidai kuwa amewapa uhuru wa kuongea, kuimba na kucheza, lakini he is denying you water, food and other basic services.

Nguruvi3, Mag3, Mzee Mwanakijiji tuko kwenye kitabu kimoja, nimeamua kukwepa chapter mnayoiuzungumzia kwa kuwa naona haijalipa, and if we continue with biz as usual hakuna litakaloendelea. I kind have lost hope with democracy as we practice it in Tanzania. It does not deliver anything tangible, ni kama tunshangilia party ya wazungu wanakunywa sisi tunaokota chupa zao. I see it as a mere tool which some of our politicians (if not most ) use it to attain certain positions for their own benefits. And once they get there ni wao wao wao, and forget about Tanzania and Tanzanians... miezi sita kabla ya uchaguzi ndio wanakuja. This is what our constitution says, as long as they are elected...let them be.

Point ya Nguruvi3 kwamba this is dangerous view given happened to Somalia, ni kweli kabisa ni hatari. Lakini kuna wakati taking risks pays. It is 50 - 50 venture, so anything can result to anything.

Mag3 anataka niseme kama kweli tawala zilizopita zilikuwa za kidemokrasia au hapana. Honestly i do not believe they were democratic. We may have chosen our wabunge democratically, but democracy in my view is not limited to elections. But my main out cry is not in that, iko kwenye maisha ya watanzania yaliyoendelea kudunika, hilo ndio lilianza kunifanya nianze kuwa na mtazamo mbadala kuhusu maendeleo.
 
Mkubwa unajua mimi sikatai kuwa kuna changamoto kwenye usimamizi, utekelezaji na ulinzi wa katiba. Nimesema hizi changamoto zilikuwepo toka awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu, na ya nne pia. Kwa hiyo hili sio jipya na sio dogo. Kusema kuwa awamu ya kwanza mpaka ya nne kulikwa na changamoto zake , sio justification ya kutochukua hatua sasa kuondoa hizo changamoto. Ila ni kushangaa kuona watu wanaona hilo ni suala jipya wakati hata jana lilikuwa gumzo. Lakini tukiweka matatizo yetu yote kwenye mizani, kweli hilo ndio zito kuliko yote? I really doubt. Na kama tukitatua suala la usimamizi wa katiba, au hata kuleta mpya, ina maana mengine yote yatakuwa yamekwisha? I really doubt. Kuna ubaya gani suala hili likikaa pembeni wakati linatafutiwa utaratibu makini na sio wa kiubabaishaji, wakati tuna-deal na changamoto nyingine ambazo ni immediate?

Kweli for great thinkers the talk should be democracy and rule of law leads to development. But at some point tunatakiwa kuangalia mazingira halisi ya nchi yetu na siasa zetu.
 
Kweli for great thinkers the talk should be democracy and rule of law leads to development.
Bila shaka sasa uko tayari kukubaliana nasi kuwa ili tupate maendeleo tunahitaji mabadiliko makubwa katika uongozi wa taifa. Mpaka siku tutakapozinduka na kuachana kabisa na tawala za kiimla zisizozingatia sheria, maendeleo yatabaki kuwa ndoto.

Udikteta wa Magufuli ni muendelezo tu wa tawala za nyuma za kiimla...kilicho tofauti ni kwamba katika awamu hii tumeongeza bidii katika kuchota maji kwa lengo la kujaza gunia. Mwisho wa siku hata vyanzo hivyo vya maji si ajabu vikanyauka na kutuacha bila akiba yoyote ya maji.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom