Mwana-G
Member
- Jan 9, 2016
- 45
- 15
Sijawahi skia wala kuona hatasku moja Rais wa Urus Putin na waliomtangulia wakitembelea nchi yeyote ya Afrika, lakin kuna mbunge mmoja kwasababu ya kuzowea kupinga kila jambo akatuma shutuma nzito na ushauri juu eti magufuri asafiri akachangamane na kujifunza uongozi kwakina Putin nasisi kwasababu ya uvyama tunashangilia aibu gani hii! Sjawai ona wala kuskia mkutano wowote wa kimataifa unaojumuisha marais wote kufanyika Afrika lakini leo Kuna mbunge anamshauri na kumshangaa magufuri eti kwann hasafiri, ngoja ni mkumbushe hakuna mkutano wowote wa kidunia unaozifaidisha nchi za dunia ya tatu, hakuna Rais bora wa dunia ya tatu anayeweka urafiki na nchi za magharibi ukiweka urafiki nao basi ukubali wananchi waumie ni principal hiyo. Nyerere alikaa madarakani miaka 24 alisafiri mara 65 sawa na mara 3 kwakila mwaka na alienda kama msemaji bila kuwa msemaji asingeenda na alienda kwasababu ya issue za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika bila hivyo Natumaini asingeenda. Ni bora baadhi ya wabunge wakaendelea kutoa hoja za matatizo ya maji na barabara majimboni mwao haya mambo mengine yaliyowazid vimo muachieni zitto.