Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimesema mara kadhaa, mie sina chama, lakini napenda kuona Tanzania ikiendelea, bila kujali CCM au Chadema ndio wanaoshika serikali.
Nimelaani sana U-CCM na U-Chadema unaoshika kasi nchini, nikisema ni huo ni mbaya na twapaswa kuulani kama tunavyolaani U-dini katika nchi yetu. U-CCM na U-Chadema unaligawa taifa hili na kuleta chuki zisizo za msingi. Hatari za U-dini katika nchi hazina tofauti na hatari za U-Chama.
Nawaomba watanzania wenzangu, tuwe na utambuzi kwamba si kila Mbunge wa au Kiongozi wa CCM ni mbaya na fisadi au gamba. Wapo walio wazuri na wazalendo wa kweli ndani ya CCM.
Na pia si kila Mbunge au kiongozi wa Chadema ni suluhisho la kuleta mageuzi kwa nchi yetu, wapo ambao ni mizigo ambayo haistahili kuwa na uongozi ndani ya Chadema.
Sasa swali ni kwamba, hivi haiwezekani sisi kama Watanzania, bila kujali tuko chama gani, kutoa sifa panapostahili, na kuona uozo panaponuka?
Akili gani tunaonyesha, ikiwa uozo tunaona ni manukato, au manukato tunaona ni uozo, kwa kuwa tu tuko chama fulani?